Ile movie ina mapungufu ambayo yameifanya kuwa ya kishamba wakati ilikuwa ni story nzuri tu ya kikomando. Yaani mimi katika scale ya 1 hadi 10 naipa 2 sababu ya makosa ya kiufundi na kiuhalisia ya director.
1. Kuna ile scene yule Sisu alikuwa na farasi wake kwa bahati mbaya akaingia eneo lenye Mabomu ya ardhini, baada ya wale jamaa kumjia lile eneo moshi ukawa hauishi, sikuelewa kwann director alifanya ule "ubongo movie pale".
Hivi inawezekana kweli watu msimame umbali usiopungua hata mita 10 halafu huyu mtu eneo lake tu ndio limetanda moshi hamuoni kitu chochote na jamaa wanasilaha kali wangeza mlenga na kumaliza kazi?
Kuna kipande anafanikiwa kutoroka anaingia chini ya maji kwenye mto, maadui wakiwa ng'ambo moja anawamaliza kwa kuwavuta ndani ya maji kutokea wao maadui wakiwa wanamfuata ndani ya maji yeye akiwa katulia tu chini anawasubiria.
Kiuhalisia yule jamaa alikuwa anakimbizwa, so mapafu yake yatakuwa yamesuphocate oxygen atakuwa anahitaji kukaa open space yenye hewa safi avute hewa, jamaa kazama chini ya maji, huku mapigo ya moyo yakiwa juu halafu katulia how is that possible, okay tuseme inawezekana sababu alijitrain, haya kuna muda akatoka kwenye maji akajitwisha mwili wa askari aliyeuwawa na yule adui kuu sababu ya kumsaidia kuvuka na boti kwenda ng'ambo ya pili, jamaa ajajitwisha mwili ili kujikinga na risasi ambazo zinamiminwa tokea ng'ambo ya pili na maadui hiyo mashine inayomimina inaweza kuchakaza mti na kuukatilia mbali ila mwamba zile risasi haikumpata hata moja[emoji23][emoji23][emoji23] hii ni kwenda kinyume na rules of reality kwenye movie.
Kuna kipande baada ya kurudia ile convoy ya maadui, akaanza kuwachomoa askari kutoka katika ile lori anawatupa mbele ya kifaru halafu ni jua linawaka keupe peeee , imagine kifaru kipo nyuma ya lori ina maana waliopo juu ya kifaru na ndani ya kifaru wanaona mbele otherwise kama hawaoni wangegonga lile lori, jamaa alikuwa akiwachomoa kama kuku bandani anawatupa nje yeye akiwa amening'inia wapi sasa kwa wakati huo? Technically huu ni uongo wa bongo movie.
Zile landmines/ bombs zilikuwa zikilipuka yeye hazimdhuru tena amezikanyaga ila maadui anawarushia zinawadhuru, huu ni udirector wa kishamba sana ambao kwa sasa wamebakia nao waindi tu kwenye movies zao.
Ndege inaruka jamaa amepiga sululu moja kakamatia uvunguni anaruka nayo hivi unajua laws of physics ndege ikiwa inapaa halafu ikafika kimo kirefu kama kile mtu akining'inia nje nini kinampata balaa la upepo linavyokua. Halafu ndege inaonekana ishafika juu na imekaa level jamaa ndio anaanza kutoboa kuingia ndani, no evidence of how ila mbwe mbwe tu za akina amita bachan [emoji23][emoji23][emoji23]
Adui mule ndani ameshamcontain yule Sisu cha ajabu anamuangalia wakati angeweza mtia shaba za kichwa show ikaisha ila anapiga ngumi tu na anajua jamaa anaroho ya paka hafi kirahisi.
Hamna kitu pale yaani afadhalia hata na ya John wick mara mbili ningesifia ni movie kali tena sio hiyo Sisu director amepuyanga sana mule.