Ni bonge moja la movie kwa mwaka huu 2023, nimeipa namba 1, nairudia mara zote nikiimiss. Wenzentu wanajua kuigiza na kuandaa movie, hilo halina ubishi.
Huyo Sisu ni mwanaume mmoja hivi mtu mzima sana amefanya action unbelievable, ana roho ngumu sana ya kukataa kifo, pamoja na kukutana na watu makatili sana na wauaji ila yeye bado anapata nafasi ya kuishi licha ya kupaniwa sana.
Kibao kinawageukia wanajeshi wa Kijerumani wanapigika kama watoto wadogo, huyo ndio Sisu. Hii movie inatufundisha kuwa tusiwachukulie poa watu kutokana na muonekano wao.
Ila nikaenda mbali na kujiuliza sisi wabongo tunakwama wapi, hata sijapata jibu zuri.
View attachment 2667058