Mtetezi.com
JF-Expert Member
- Oct 6, 2016
- 3,134
- 3,584
Kumbe hivi vitu vilitengenezwa kwaajili ya wazungu jamani sisi waafrica hatuviwezi!!
Nilikuwa naelekea ofisi fulani ktkt ya jiji la Dar nilikuwa natoka ground to 8th floor sikujua kuwa ilikwama floor ya ngapi ghafla tu nikaona kiza kinene baada ya taa kuzima na joto kali saana kisha baada ya mda kuishiwa nguvu baada ya kukosa oxygen.
Nitaendelea zaidi ngoja leo niishie hapo kwani kuandika uzi huu kumekitonesha kidonda ambacho kilishapoa.
INAENDELEA..........
Nikatoa simu ya smartphone na kuwasha tochi ili nijue nipo wapi mana niliwaza au huenda nipo kaburini!
Kuwasha simu nikagundua bado nipo ktk elevatotor nikaangalia zile butun kuna sehemu ya emergence call na sehemu za alarm but kwakuwa kulikuwa kumezima kabisa havukufanya kazi hata kimoja nikazidi kuchanganyikiwa.
Kupapasapapasa taa mule ndani nikaona sehemu imeandikwa NAMBA YA FUNDI nikaingiza na kupiga Subhanallah siku ya kufa nyani miti yote huteleza simu haikuwa na network kabisa yani kabisa kumbe kwenye lift huwa simu inapoteza network kabisa jamani sikuwahi kujua hilo na mpaka sasa sijajua ni ie siku tu au ndio utaratibu nikarestart simu waaapi washa zima hamna kitu mpaka pale nikajua kabisa sasa kwa akili na uwezo wabinaadamu nimeshafail kikubwa tu niswali swala zangu za mwisho.
Baada ya sala zangu za mwisho na toba nyingi sana za makosa yangu nikawa namkabidhi Mungu roho yangu huku naumia nikisema "Yani nakufa huku najiona" Lakini sikuwa na jinsi nikasimama tochi nayo ikazima baada ya simu kuishiwa charge pale sasa ndio nilipokuwa namuona Israel huyooo anakuja na nikawa nalaumu kwann Israel anachelewa nateseka namna hiyo huku nikiwa bado naogopa kifo hatari jamani kifo kisikie kwa mwenzako usiombe kikukute alafu live unakiona.
Baada ya dk kadhaa nikapata tena nguvu na akili mpya nikaamua kuangalia ni jinsi gani naweza kutumia nguvu zangu kujitetea kutoka mule ndani!
Katika zile kutano za milango pale katikati nikaona kumebana lakini nikisikiliza napata kisikia sauti ya nje hewa inapuliza.
Nikaamua kusikiliza kwa makini huku nikijiona tayari nipo kaburini mana elevator yenyewe bila taa ni kama kaburi usiombe yakukute, sasa wakati nasikiliza pale mlangoni na kusikia sauti ya watu kwa mbaliiii nikasema mm hata nipige yowe au kelele ni kazi bure sauti haitaweza kusikika.
Nikasema ngoja niuvunje huu mlango nitoke potelea mbali liwalo na liwe nikaaanza kupiga ngumi pale ktkt milango inapokutana duh kumbe ni pagumu sana yani hata kutikisika ikashindikana nikasema duh leo ni siku ya kufa ndio maana kila kitu kinagoma nikirefer maandiko takatifu pale yanaposema kuwa magonjwa yote yana tiba ila sio kifo.
Itaendelea baadae kidogo ......
INAENDELEA .....
Baada ya kuona kuwa sifi na hakuna mtetezi nikaanza tena kufikiri je mm siwezi kujitetea jamani!
Unajua binaadamu akiingiwa na woga au hofu kuna hali humjia yani anakuwa kama sio binadamu yani anaweza hata kukwea mti wenye miba bila yeye kujua wala kuumia , ndivyo ilivyotokea kwangu na kwa bahati mbaya yani sijui sikuhiyo kulikuwa na nini mana hiyo lift inakuwaga bussy sikajua kwanini hakukutokea mtu yeyote kuja kupanda sijui lengo lilikuwaje au sijui ndio siku zangu zilifika duh usiombe ikukute.
Baada ya kupata ile hali ya nguvu za ajabu huku nikiwa kama mwili umekufa ganzi nilianza kupiga ngumi pale mlangoni kwa nguvu kiasi ya kwamba hata aliyepita huko chini alistuka na kujiuliza jamani kuna nn kinapiga huko juu kwa nguvu kiasi hicho basi askari/security wote wakaanza kuandamana kusikiliza ni nini hiko na kwa kupitia ilipo lifti wakaelewa kuwa kuna tatizo na kuna watu wamekwama.
Wakajaribu kufungua waaapi ikashinda mana kumbe nilinasa floor ya tatu hivyo ndio maana nilivyokuwa napiga ilisikika sipati picha ningenasa ya nane ingekuwaje.
Basi wakamtafuta fundi na kwa bahati zuri ilikwama ktk kituo yani sehemu ya kushukia au kupandia ktk floor ya tatu hivyo kwa fundi haikuwa tabu kuniokoa kwani baada tu ya kufungua mlango aliniona nikiwa nmebadilika yani nina hasira kama mbogo na baada tu ya kutoka nikaomba nitoke nje nikapunge upepo baada ya masaa kadhaa nikawa sawa japo usiku wake niliteseka sana pindi ile hali ivivyokuwa inajirudia kichwani mwangu.
Kiukweli ktk mambo ambayo sitakaa nikayasahau hili nalo sitalisahau.
Ushauri serikali na mashirika yasiyo ya kiserikali yatengeneze utaratibu wa hizi lift kuwa zinakaguliwa mara kwa mara ili kudhibiti ubora na ufanisi wake wasingoje mpaka watu wafe ndio waunde tume.