Sitaisahau siku lift ya ghorofa ilipofail/kwama katikati ya safari nikiwa peke yangu

Sitaisahau siku lift ya ghorofa ilipofail/kwama katikati ya safari nikiwa peke yangu

Mtetezi.com

JF-Expert Member
Joined
Oct 6, 2016
Posts
3,134
Reaction score
3,584
Kumbe hivi vitu vilitengenezwa kwaajili ya wazungu jamani sisi waafrica hatuviwezi!!

Nilikuwa naelekea ofisi fulani ktkt ya jiji la Dar nilikuwa natoka ground to 8th floor sikujua kuwa ilikwama floor ya ngapi ghafla tu nikaona kiza kinene baada ya taa kuzima na joto kali saana kisha baada ya mda kuishiwa nguvu baada ya kukosa oxygen.

Nitaendelea zaidi ngoja leo niishie hapo kwani kuandika uzi huu kumekitonesha kidonda ambacho kilishapoa.

INAENDELEA..........
Nikatoa simu ya smartphone na kuwasha tochi ili nijue nipo wapi mana niliwaza au huenda nipo kaburini!
Kuwasha simu nikagundua bado nipo ktk elevatotor nikaangalia zile butun kuna sehemu ya emergence call na sehemu za alarm but kwakuwa kulikuwa kumezima kabisa havukufanya kazi hata kimoja nikazidi kuchanganyikiwa.

Kupapasapapasa taa mule ndani nikaona sehemu imeandikwa NAMBA YA FUNDI nikaingiza na kupiga Subhanallah siku ya kufa nyani miti yote huteleza simu haikuwa na network kabisa yani kabisa kumbe kwenye lift huwa simu inapoteza network kabisa jamani sikuwahi kujua hilo na mpaka sasa sijajua ni ie siku tu au ndio utaratibu nikarestart simu waaapi washa zima hamna kitu mpaka pale nikajua kabisa sasa kwa akili na uwezo wabinaadamu nimeshafail kikubwa tu niswali swala zangu za mwisho.

Baada ya sala zangu za mwisho na toba nyingi sana za makosa yangu nikawa namkabidhi Mungu roho yangu huku naumia nikisema "Yani nakufa huku najiona" Lakini sikuwa na jinsi nikasimama tochi nayo ikazima baada ya simu kuishiwa charge pale sasa ndio nilipokuwa namuona Israel huyooo anakuja na nikawa nalaumu kwann Israel anachelewa nateseka namna hiyo huku nikiwa bado naogopa kifo hatari jamani kifo kisikie kwa mwenzako usiombe kikukute alafu live unakiona.

Baada ya dk kadhaa nikapata tena nguvu na akili mpya nikaamua kuangalia ni jinsi gani naweza kutumia nguvu zangu kujitetea kutoka mule ndani!
Katika zile kutano za milango pale katikati nikaona kumebana lakini nikisikiliza napata kisikia sauti ya nje hewa inapuliza.
Nikaamua kusikiliza kwa makini huku nikijiona tayari nipo kaburini mana elevator yenyewe bila taa ni kama kaburi usiombe yakukute, sasa wakati nasikiliza pale mlangoni na kusikia sauti ya watu kwa mbaliiii nikasema mm hata nipige yowe au kelele ni kazi bure sauti haitaweza kusikika.

Nikasema ngoja niuvunje huu mlango nitoke potelea mbali liwalo na liwe nikaaanza kupiga ngumi pale ktkt milango inapokutana duh kumbe ni pagumu sana yani hata kutikisika ikashindikana nikasema duh leo ni siku ya kufa ndio maana kila kitu kinagoma nikirefer maandiko takatifu pale yanaposema kuwa magonjwa yote yana tiba ila sio kifo.
Itaendelea baadae kidogo ......

INAENDELEA .....
Baada ya kuona kuwa sifi na hakuna mtetezi nikaanza tena kufikiri je mm siwezi kujitetea jamani!
Unajua binaadamu akiingiwa na woga au hofu kuna hali humjia yani anakuwa kama sio binadamu yani anaweza hata kukwea mti wenye miba bila yeye kujua wala kuumia , ndivyo ilivyotokea kwangu na kwa bahati mbaya yani sijui sikuhiyo kulikuwa na nini mana hiyo lift inakuwaga bussy sikajua kwanini hakukutokea mtu yeyote kuja kupanda sijui lengo lilikuwaje au sijui ndio siku zangu zilifika duh usiombe ikukute.

Baada ya kupata ile hali ya nguvu za ajabu huku nikiwa kama mwili umekufa ganzi nilianza kupiga ngumi pale mlangoni kwa nguvu kiasi ya kwamba hata aliyepita huko chini alistuka na kujiuliza jamani kuna nn kinapiga huko juu kwa nguvu kiasi hicho basi askari/security wote wakaanza kuandamana kusikiliza ni nini hiko na kwa kupitia ilipo lifti wakaelewa kuwa kuna tatizo na kuna watu wamekwama.

Wakajaribu kufungua waaapi ikashinda mana kumbe nilinasa floor ya tatu hivyo ndio maana nilivyokuwa napiga ilisikika sipati picha ningenasa ya nane ingekuwaje.
Basi wakamtafuta fundi na kwa bahati zuri ilikwama ktk kituo yani sehemu ya kushukia au kupandia ktk floor ya tatu hivyo kwa fundi haikuwa tabu kuniokoa kwani baada tu ya kufungua mlango aliniona nikiwa nmebadilika yani nina hasira kama mbogo na baada tu ya kutoka nikaomba nitoke nje nikapunge upepo baada ya masaa kadhaa nikawa sawa japo usiku wake niliteseka sana pindi ile hali ivivyokuwa inajirudia kichwani mwangu.

Kiukweli ktk mambo ambayo sitakaa nikayasahau hili nalo sitalisahau.
Ushauri serikali na mashirika yasiyo ya kiserikali yatengeneze utaratibu wa hizi lift kuwa zinakaguliwa mara kwa mara ili kudhibiti ubora na ufanisi wake wasingoje mpaka watu wafe ndio waunde tume.
 
kwani umelazimishwa kuandika? ila anyways pole sana kwa kujitonesha hilo donda
 
Mie niliwahi kunasa kwa saa nzima pale jengo la ushirika nilikuwa natoka ofisi za TPDC. Zile elevators pale huwa zinajaa sana bahati nzuri siku ile tulikuwa watatu. Mimi, mmakonde mmoja wa chale na mdosi. Tukiwa tunaulizwa mko wangapi tukawa tunajibu tuko 10 ili waharakishe kutupa msaada toka kwa watu wa OTIS.

Basi mmakonde akaanza kutema mate ndani ya elevator acha nimjie juu. Nikamwambia si ustaarabu hata kidogo kutema mate ndani ya elevator. Hakutema tena ila dakika ndiyo zinayoyoma sikuwahi kunasa kwenye elevator kabla wasiwasi umeanza basi ghafla tu baada ya saa moja ikaanza kumove na kusimama katika moja ya floors na kufungua mlango speed ya kila mtu kutoka haikuwa ya kawaida.

Kwenye majengo mengi huwa hakuna jinsi ni lazima upande tu lakini kama ningeweza kuziepuka ningefanya hivyo.

Kumbe hivi vitu vilitengenezwa kwaajili ya wazungu jamani sisi waafrica hatuviwezi!!

Nilikuwa naelekea ofisi fulani ktkt ya jiji la Dar nilikuwa natoka ground to 8th floor sikujua kuwa ilikwama floor ya ngapi ghafla tu nikaona kiza kinene baada ya taa kuzima na joto kali saana kisha baada ya mda kuishiwa nguvu baada ya kukosa oxygen.

Nitaendelea zaidi ngoja leo niishie hapo kwani kuandika uzi huu kumekitonesha kidonda ambacho kilishapoa.
 
Kumbe hivi vitu vilitengenezwa kwaajili ya wazungu jamani sisi waafrica hatuviwezi!!

Nilikuwa naelekea ofisi fulani ktkt ya jiji la Dar nilikuwa natoka ground to 8th floor sikujua kuwa ilikwama floor ya ngapi ghafla tu nikaona kiza kinene baada ya taa kuzima na joto kali saana kisha baada ya mda kuishiwa nguvu baada ya kukosa oxygen.

Nitaendelea zaidi ngoja leo niishie hapo kwani kuandika uzi huu kumekitonesha kidonda ambacho kilishapoa.
Nikajua umenasa tena....pole mkuu
 
Hahaa. Hauko peke ako. Muulize Mkapa alivyonasa kwenye lift wizara ya miundombinu. Lile jengo lilikuwa na lift nzee sana hadi wakaajiri mtu spesho wa kusafiri nayo. Sasa Mkapa alivyokuwa Rais akawa ameenda wizarani sijui kufanya nini. Basi ile kupanda tu, lift ikabuma. Watu wakahaha kumnasua.
NB: hii ni story iliyokuwepo vijiweni, sina uhakika kama tukio lilitokea au lah. Ila nina uhakika kuwa jengo la wizara lilikuwa na lift kimeo. Nadhani watakuwa washaibadilisha.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Leo nacheka tu. Umenikumbusha mbali sana. Kwenye lift ya IFM watu walikuwaga wananasa kila siku. Na lift yenyewe ilivyokuwa inajaza watu nyomi! Ucpime.

Kwa wale waliosoma UDSM na kuishi Hall 2 kukwama kwa lifti ilikuwa kawaida sana. Sijui kwa siku hizi
Hall two walifunga lift mpya!
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Ilinitokea mara moja,kumbe ile lift ina ka tangazo kadogo nje kuwa LIFT MBOVU,mimi sikukaona nikadumbukia ikapanda kidogo nikaona kimyaa,taa zmezima hakuna kinachoendelea giza totoro,nilichofanya ni kuanza kupapasa zilipokuwa butons,yaani kama zali nilichobonyeza ndio kitufe sahihi ikarudi tena chini na mlango ukafunguka.Sikuwa nasikia joto mle ndani ila nilipotoka nikagundua kuwa nimelowa jasho mwili mzima...
 
Kwa wale waliosoma UDSM na kuishi Hall 2 kukwama kwa lifti ilikuwa kawaida sana. Sijui kwa siku hizi
 
Acha kabisa lakini wakati mwingine hakuna jinsi fikiria unaenda ghorofa ya 20. Kuna moja nilisikia zile waya ambazo zinaishikilia zilikatika ikiwa na watu ndani basi ikaporomoka kufika chini kuna watu walikufa na wengine kuvunjika miguu.

mi ndo maana sitakagi hizo mambo, hadi nipande lift labda nishikwe kwa nguvu
 
Acha kabisa lakini wakati mwingine hakuna jinsi fikiria unaenda ghorofa ya 20. Kuna moja nilisikia zile waya ambazo zinaishikilia zilikatika ikiwa na watu ndani basi ikaporomoka kufika chini kuna watu walikufa na wengine kuvunjika miguu.
Duh! Ila nafikiri kupanda lifti na ndege ni sawa sawa tu.
 
Acha kabisa lakini wakati mwingine hakuna jinsi fikiria unaenda ghorofa ya 20. Kuna moja nilisikia zile waya ambazo zinaishikilia zilikatika ikiwa na watu ndani basi ikaporomoka kufika chini kuna watu walikufa na wengine kuvunjika miguu.
Mimi naona afadhali kugoma, hii ya kushuka kwa kasi ni hatari sana, kifo na kuvunjika vinahusika sana
 
Back
Top Bottom