Sitaisahau siku lift ya ghorofa ilipofail/kwama katikati ya safari nikiwa peke yangu

Sitaisahau siku lift ya ghorofa ilipofail/kwama katikati ya safari nikiwa peke yangu

Duuuh hatari acha nibaki tu na ushamba wangu teh....
Siku nlienda kujifungua nna uchungu nesi ananambia tupande lift kwenda leba, nkamwambia hapana sipandi lift mie napanda ngazi, anauliza mara mbili utaweza kupanda namwambia lift sipandi....wala sikupanda
duu!!!
 
Hahaa. Hauko peke ako. Muulize Mkapa alivyonasa kwenye lift wizara ya miundombinu. Lile jengo lilikuwa na lift nzee sana hadi wakaajiri mtu spesho wa kusafiri nayo. Sasa Mkapa alivyokuwa Rais akawa ameenda wizarani sijui kufanya nini. Basi ile kupanda tu, lift ikabuma. Watu wakahaha kumnasua.
NB: hii ni story iliyokuwepo vijiweni, sina uhakika kama tukio lilitokea au lah. Ila nina uhakika kuwa jengo la wizara lilikuwa na lift kimeo. Nadhani watakuwa washaibadilisha.
Mi nlipanda lift Toka magomen had posta we hyo boda inakimbia cjawah ona
 
Kwa wale waliosoma UDSM na kuishi Hall 2 kukwama kwa lifti ilikuwa kawaida sana. Sijui kwa siku hizi
Dah umenikumbusha mbali sana enzi hizo nilikuwa naishi hall 2, floor ya kumi
Nilikwama siku moja, tupo mtu kumi miksa madem wakaanza kuvua nguo dah!(joto kali) halafu ilikuwa kipindi cha test
Ukipiga kelele masela wanakuja wanawauliza mna test?
Ukisema hauna wanakuacha wanakwambia msubiri fundi

Kipindi cha UE ilikuwa marufuku kwangu kupanda lift

Ila afadhali hall 2 ilikuwa ina space unaweza kupumua, hall 5 unaweza ukafa unajiona
 
Back
Top Bottom