Sitaki habari za simba na yanga: Jiheshimu uheshimiwe

Sitaki habari za simba na yanga: Jiheshimu uheshimiwe

Hivi huko Tanganyika huwa mnasoma somo la nidhamu mashuleni?

Umekutana na mtu, wala hamfahamiani kihivyo, hujui anapenda nini, hujui anavutiwa na nini, unakurupuka tu?

Nani aliwaambia kila mtu ni shabiki au mfuasi wa mpira?

Umekutana na mtu, wala havutiwi hata na mipira, unaanza kuleta mastori ya simba na yanga? Unaugua?

Ati oooh, hivi lile goli la jana la Mayele ulilionaje? Alipiga hat trick....blah blah....

Kwanza huyo Mayele mwenyewe ndio nani? Mimi hata simjui.

Nikikuhurumia sana ili usifadhaike nitajifanya tu kuitikia kwa kuguna mhhhh, mhhhh, yess, oooh yess... ndiwooooooooo.......

Nikikasirishwa na mastori yako ya mayele nakutimua au nakucharaza bakora.

Kabla ya kumrukia mtu hakikisha unajiridhisha kama hicho unachomwambia anakifurahia au kukipenda. Mjifunze kuelewa mipaka ya mazungumzo.

MY TAKE: Tupunguze ushamba na kurukia watu.
Sasa ndo huyo mwamba umekuja kumchambia huku?🤔
 
😂😂😂 Eeeeeeehhhh

Kuna unga fulani pia ulikuwa unatoka marekani unagawiwa kwa wanafunzi mashuleni ulikuwa wa njano haswaaa wanauita YANGA. Juzi tu hapa. Miaka ya 2010. 😉😉

Dokta mwaka 1992 ulikuwa na miaka mingapi 😉😉😉😉
Nilikuwa nina Miaka 20..
Ndo nimeuanza ubaro baro hapo kutwa tunashinda Disco mbowe.....
Maisha ya Ujana matamu sana
 
Back
Top Bottom