‘Sitaki Kuitwa Sponsor’: Uhuru Akanusha Madai ya Kufadhili Upinzani Kuelekea 2027

‘Sitaki Kuitwa Sponsor’: Uhuru Akanusha Madai ya Kufadhili Upinzani Kuelekea 2027

Omu

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2026
Posts
469
Reaction score
95
Aliyekuwa Rais Uhuru Kenyatta amekanusha madai kwamba anafadhili viongozi wa upinzani wanaojiandaa kumpinga Rais William Ruto katika Uchaguzi Mkuu wa 2027, akisisitiza kuwa uamuzi wa nani ataongoza Kenya uko mikononi mwa wananchi.

Akizungumza Kitale wakati wa kumbukumbu ya aliyekuwa Makamu wa Rais Michael Kijana Wamalwa Jumapili, Agosti 23, Uhuru alisema hana nia ya kurejea katika siasa za uchaguzi baada ya kukamilisha mihula yake miwili kama rais.

Uhuru alikuwa akitaja baadhi ya wanasiasa wanaoweza kuwania urais—akiwemo Kalonzo Musyoka, William Ruto, Fred Matiang'i na Edwin Sifuna—alipofika kwa jina la Sifuna na umati kulipuka kwa shangwe.

Reaction hiyo ikamfanya Uhuru ajibu kwa utani:

“Jameni chungeni, sitaki kuitwa sponsor.”

Kauli hiyo ilionekana kulenga madai ambayo Rais Ruto na baadhi ya washirika wake wamekuwa wakitoa kwamba Uhuru yuko nyuma ya baadhi ya wanasiasa na movements zinazompinga serikali. Sifuna pia amekanusha madai kwamba Uhuru anafadhili Linda Mwananchi, akisema movement hiyo inategemea michango kutoka kwa Wakenya na well-wishers.

Uhuru alisema hataki kiti chochote cha kisiasa na kwamba baada ya kutumikia nchi kwa miaka 10, sasa ni wakati wa wengine. Hata hivyo, aliwahimiza viongozi wa upinzani wanaotaka kutoa alternative kwa serikali kutafuta njia ya kuungana na kuheshimiana, akisema ni mtu mmoja tu atakayekuwa rais baada ya uchaguzi.

Kwa hiyo, hata kama Uhuru anasema “sitaki kuitwa sponsor,” wito wake wa opposition kuungana unaendelea kuweka nafasi yake kuelekea 2027 chini ya darubini ya kisiasa.

GUCY5LKL.png

 
Back
Top Bottom