Uchaguzi 2020 Sitaki kuwa mnafiki. WanaCCM awamu hii tunaburuzwa na Mwenyekiti

Kumbuka juzi alivyo mjibu yule mjumbe toka songwe kwamba hao machotara kupewa vyeo ni matakwa yake binafsi.

Kwa sababu hao machotara toka upinzani walitakiwa wapite kwenye mchujo wa kawaida na kura zipigwe kama kawaida ila anancho kifanya maoni yote ya wana ccm anayapuuzi na kuweka yake.
Yaah. Hili limeanzia huko mkuu, tunamuliwa mambo badala ya waccm we nyewe kuamua. WanaCCM hatujaipenda hii.
 

Sio kwamba wanaccm hawaujui ukweli huu, ila wanakaa kimya maana wanajua pia bila madaraka ya huyo mwenyekiti, hata wao kutangazwa washindi itakuwa ngumu. Uzuri hata mwenyekiti mwenyewe wa ccm anajua fika bila kutumia madaraka yake vibaya, ccm hawawezi kutangazwa washindi. Ndio maana hakuna mwanaccm anataka kusikia kitu kiitwacho tume huru ya uchaguzi.

Hapo walipo wanaccm wanaomba usiku na mchana wapinzani wasusie uchaguzi. Wanajua fika iwapo wapinzani watakaza kushiriki huu uchaguzi, watatumia nguvu kubwa kujitangaza washindi, hali itakayoliacha taifa hili na mgawanyiko mkubwa, na sifa mbaya ya utawala wa mabavu.
 
Umezungumza ukweli...ila subiri wasaka tonge waje kukushugulikia kwa mipovu.
 
Hakuna ccm hapo, ccm ndio imekufa hivo.
Wajumbe wanalia dodoma, wazanzibar jana wamelia machozi wengine wanaume.

Ccm iliyo baki ni Chama Cha Magufuli (CCM) na siyo Chama Cha Mapinduzi.
 
Haya hangaikeni na Mwenyekiti wenu ; tuliwaonya ila mkatuona waongo!! Haya sasa!!

Bila kuwa kwenye list yake ubunge utausikia tu kwa majirani.
 
Magufuli kasema bila aibu kwamba atamkata mtia nia yeyote, si kwa katiba, si kwa miongozo, si kwa taratibu, si kwa utamaduni,bali kwa jinsi takavyojisikia alivyoamka siku hiyo.
Hili ndiyo suala linalo nong'onwa Sana hapa Dodoma na wajumbe wa mkutano mkuu. Wengi wanaenda mbali na kusema "wagombea pendwa" tu ndiyo watapitishwa. Na Kuna majimbo wanapelekewa wagombea na kuitaka kamati ya siasa ya wilaya kuwapa ushirikiano. Hatari hii.
 
Nenda kapige kura, then watuoneshe kwa vitendo hiyo kauli yao, talking is always cheap.

Tangu mwaka 2000 nimekuwa mpiga kura mwaminifu. Ila kuanzia mwaka wa jana 2019, niliapa kutoshiriki chini ya utawala wa Magufuli, mtu asiyeheshimu demokrasia na matakwa ya wananchi walio wengi .

Akitoka madarakani, Inshallah! Nitarudi. Huu ni msimamo wangu binafsi.
 
Lini umehama CHADEMA?
 
wewe lazima utakuwa ndiye yule mjumbe wa NEC kutoka Songwe aliyemuuliza mwenyekiti wake swali gumu jana wewe.... si bure!!
 
Nenda kapige kura, then watuoneshe kwa vitendo hiyo kauli yao, talking is always cheap.

Ni vyema kama ni kushiriki kupiga kura watu wahimizwe kwenda na silaha za jadi. Ila kwenda kupiga kura kama wanaenda kwenye nyumba za ibada ni utani. Uchaguzi wa safari hii kama wapinzani wamekubali kushiriki chini ya tume hii, wajiandae kwa machafuko zaidi kuliko kinyume chake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…