Uchaguzi 2020 Sitaki kuwa mnafiki. WanaCCM awamu hii tunaburuzwa na Mwenyekiti

Uchaguzi 2020 Sitaki kuwa mnafiki. WanaCCM awamu hii tunaburuzwa na Mwenyekiti

wewe lazima utakuwa ndiye yule mjumbe wa NEC kutoka Songwe aliyemuuliza mwenyekiti wake swali gumu jana wewe.... si bure!!
Yule alikuwa anawasemea wengi mkuu. Tulimtuma na kumtia moyo ayaseme aliyoyasema.
 
Anachokitaka ndicho huwa. Na anafanya mambo kwa manufaa yake ya kisiasa. Kwanini nasema haya??

1. Angalia namna mchakato wa uchukuaji fomu za kugombea urais wa JMT ulivyokuwa na figisu. Eti wanaCCM wengine hawaruhusiwi kuchukua fomu. Ni yeye tu.

2. Angalia chaguzi za marudio ktk majimbo ambayo wabunge wapinzani "waliunga mkono juhudi". WanaCCM tulinyimwa kushindana nao. Na hata ktk uchaguzi huu tumepigwa marufuku kushindana nao.

3. Angalia upigaji kura ktk mkutano mkuu, ukusanyaji wa kura ulikuwa wa kimikoa (hii mbinu imewekwa ili iwe rahisi kutufuatilia wale ambao tungepiga kura ya hapana).

4. Kwa kinywa chake mwenyewe amesema kura za maoni za watia nia wa ubunge hazina maaana. Yeye amesema anaweza kumchukuwa hata mtu wa mwisho. Yaani badala ya wagombea kutafuta ridhaa ya wananchi, Sasa wanasubiri maamuzi binafsi ya mwenyekiti.

Demokrasia imezikwa rasmi ndani ya CCM. WanaCCM tunapelekwa pelekwa tu.

Kama ni kweli mnaona mnaburuzwa, kwa nini unaendelea kukubali kuburutwa? ungepinga kuburutwa yawezekana ungeleta mabadiliko. Yawezekana mwenyekii hajui kama aawaburuta maana ni kawaida ya wana ccm kukubali na kushangilia kila kitu hata kama wanaona ukweli ulivyo
 
1. Angalia namna mchakato wa uchukuaji fomu za kugombea urais wa JMT ulivyokuwa na figisu. Eti wanaCCM wengine hawaruhusiwi kuchukua fomu. Ni yeye tu.

Ulienda ukazuiliwa kuchukua hiyo fomu?.. au ni nyie kupaisha midomo na kuogopeshana na kufanganyana.. na mkaishia mulipo..
 
Mleta mada nawe ni mmoja kati ya wale walotuletea hili janga kwani mlitambua mapema lakini kwakuwa mlikuwa mnapata book 7 kila siku kazi yenu ikawa kusifia kiasi ya kwamba huyo m/kiti wenu huenda hakujua kama hamkupendezwa na alokuwa akiyatenda kwani alisikia vigeregere kila upande alogeuka.

Upinzani walijitahidi kueleza makosa lakini ninyi mliporomosha matusi makubwa makubwa kwamba malaika mtukufu kakosewa nadhani sasa akili zimewakaa sawa, huyu m/kiti wenu mwanzo aliwatupa walomwingiza madarakani na sasa nyie mliompitisha leo

subirini apite nanyi mtatupwa kama ifanywavyo toilet paper na hapo ndipo mtaungana na upinzani ili kumuondoa nduli mliyemfuga
huku mkijipa matumaini kwamba huwezi tishwa na kinyago ulicho chonga mwenyewe mara ooh zimwi likujualo halikuli likakumaliza na tambo nyingine kedekede mlikosea sana mlileta mifano ya kipumbavu na akati mtu mnamkabidhi nchi,
ni sawa na kumkabidhi ndege rubani feki kwa safari ya miaka.
 
Ulienda ukazuiliwa kuchukua hiyo fomu?.. au ni nyie kupaisha midomo na kuogopeshana na kufanganyana.. na mkaishia mulipo..
Tulikuwa tunapigwa biti kuanzia kitaa mpk viongozi wa chama kwamba tusithubutu. Ndiyo maana tukaacha. Mbali ya Membe aliyevuliwa hadi uanachama kwa kutaka kugombea, kuna mwenzetu mwingine alijipanga kabisa (sitamtaja). Akapewa vitisho akaacha. In box naweza kukupa jina lake.
 
3. Angalia upigaji kura ktk mkutano mkuu, ukusanyaji wa kura ulikuwa wa kimikoa (hii mbinu imewekwa ili iwe rahisi kutufuatilia wale ambao tungepiga kura ya hapana
NDIO, ni kweli.

Ukiweka kura ya HAPANA kwenye sanduku la CCM MOROGORO watapeleka fomu ile kwa RPC au RSO wa Morogoro kufanyiwa dusting for fingerprints, halafu anapewa kachero aliyeko NIDA au TCRA au Tume ya Uchaguzi au VODACOM anaambiwa pitia fingerprints zote za wana CCM wa MOROGORO uimachi na hii hapa.

Kumbuka taasisi zote hizo zinazo fingerprints zetu wote, na kote humo Usalama wapo kisheria, na mashine za ku match fingerprints wanazo!

Very very very simple to figure you out!
 
Anachokitaka ndicho huwa. Na anafanya mambo kwa manufaa yake ya kisiasa. Kwanini nasema haya??

1. Angalia namna mchakato wa uchukuaji fomu za kugombea urais wa JMT ulivyokuwa na figisu. Eti wanaCCM wengine hawaruhusiwi kuchukua fomu. Ni yeye tu.

2. Angalia chaguzi za marudio ktk majimbo ambayo wabunge wapinzani "waliunga mkono juhudi". WanaCCM tulinyimwa kushindana nao. Na hata ktk uchaguzi huu tumepigwa marufuku kushindana nao.

3. Angalia upigaji kura ktk mkutano mkuu, ukusanyaji wa kura ulikuwa wa kimikoa (hii mbinu imewekwa ili iwe rahisi kutufuatilia wale ambao tungepiga kura ya hapana).

4. Kwa kinywa chake mwenyewe amesema kura za maoni za watia nia wa ubunge hazina maaana. Yeye amesema anaweza kumchukuwa hata mtu wa mwisho. Yaani badala ya wagombea kutafuta ridhaa ya wananchi, Sasa wanasubiri maamuzi binafsi ya mwenyekiti.

Demokrasia imezikwa rasmi ndani ya CCM. WanaCCM tunapelekwa pelekwa tu.
Hama chama kwani lazima uwe ccm????
 
Siku alipo punguza wajumbe ndio mwanzo wa huu udikteta..
Udiktena hauletwi na raisi bali unaletwa na vyombo vya dola bila vyombo vya dola hakuna dikteta maaana hata akisema fanyeni hivi vyombo vya dola mahakama na bunge vikikataaa huwez endelea kuwa raisi ivo udikteta huletwa na vyombo vyote vya ulinzi bunge na mahakama
 
Ungehama chama uende kusikoburuzwa kuliko kukarahisha nafsi yako
 
Tangu mwaka 2000 nimekuwa mpiga kura mwaminifu. Ila kuanzia mwaka wa jana 2019, niliapa kutoshiriki chini ya utawala wa Magufuli, mtu asiyeheshimu demokrasia na matakwa ya wananchi walio wengi .

Akitoka madarakani, Inshallah! Nitarudi. Huu ni msimamo wangu binafsi.
Ok.
 
Ni vyema kama ni kushiriki kupiga kura watu wahimizwe kwenda na silaha za jadi. Ila kwenda kupiga kura kama wanaenda kwenye nyumba za ibada ni utani. Uchaguzi wa safari hii kama wapinzani wamekubali kushiriki chini ya tume hii, wajiandae kwa machafuko zaidi kuliko kinyume chake.
Silaha ya jadi kwenye kupiga kura sio issue, issue ni kwenye kumtangaza mshindi.
 
NDIO, ni kweli.

Ukiweka kura ya HAPANA kwenye sanduku la CCM MOROGORO watapeleka fomu ile kwa RPC wa Morogoro au RSO wa Morogoro kufanyiwa dusting for fingerprints, halafu anapewa kachero aliyeko NIDA au TCRA au Tume ya Uchaguzi au VODACOM anaambiwa pitia fingerprints zote za wana CCM wa MOROGORO uimachi na hii fingerprint au palm prints.

Kumbuka taasisi zote hizo zinazo fingerprints zetu, na kote humo Usalama wapo kisheria, na mashine za ku match fingerprints wanazo!

Very very very simple to figure you out!
Ni kweli. Mbali na hilo hata humo kwenye ukumbi viongozi walitusihi tusipige kura ya hapana ili mkoa wetu usije kuonekana umeasi, halafu wanachama na viongozi wa chama wakaipata freshi
 
Back
Top Bottom