Uchaguzi 2020 Sitaki kuwa mnafiki. WanaCCM awamu hii tunaburuzwa na Mwenyekiti

Uchaguzi 2020 Sitaki kuwa mnafiki. WanaCCM awamu hii tunaburuzwa na Mwenyekiti

Alipowabinya wapinzani tuliona raha tukizani sisi WanaCCM tutakula kuku kwa mrija, lkn kumbe muda wetu wa kulia ulikuwa bado haujafika. Hakika Sasa tunajuta.
Muungwana hukiri makosa take,ninacho hofia ni mpango wake wa kutaka kuongezewa muda awamu ijayo. He has to go akimaliza miaka mitano ijayo .
 
Mwaka huu ni kichekesho. Mtaongea kila uongo. Sasa hao wagombea wenu ambao hata udiwani hawawezi kupata unadhani wana Ccm wasingepiga kura zote kwa JPM kwa mambo anayofanya?

Ukiona kiongozi anapigiwa kura na kupata 100%, fuatilia vizuri mfumo wa uchaguzi, utakuta mengi nyuma ya pazia. Na kama kweli kapata 100%, basi jua anaoongoza makondoo.
 
Nilijua una problem kwa kichwa toka mwanzo ndo mana nika ku-quote, mwenzio keshaamka akili, wewe sijui utaamka lini!.

Unazungumzia kwenye TV wakati mwenzio alikuwa eneo la tukio kama mshiriki!.
Mchakato umefanyika kwa uwazi kabisa. WanaCcm wanaimani na JPM ndio maana amepata kura zote. Na huu upotoshaji wa kijinga ndio unawanyima credit.
 
wewe lazima utakuwa ndiye yule mjumbe wa NEC kutoka Songwe aliyemuuliza mwenyekiti wake swali gumu jana wewe.... si bure!!
Swali hill. Ni sawa like swali kwa nini chadem walimruhusu Lowassa kugombania kitu cha Urais kupitia chadema. Au ACT kutaka Membe achukue form hili kugombania ACT Urais.....
 
Ukiona kiongozi anapigiwa kura na kupata 100%, fuatilia vizuri mfumo wa uchaguzi, utakuta mengi nyuma ya pazia. Na kama kweli kapata 100%, basi jua anaoongoza makondoo.
Kondoo? Au kondoo ni watu kama wewe ambao kazi yenu ni kupinga tu hata jambo ambalo mnanufaika nalo. Wanachama wa Ccm wameona kazi aliyoifanya ndio maana wamempa kura kwa 100%. Subiri JNHPP ikamilike ule matunda ya Ccm.
 
Tuliwaonya huyu ni dikteta, mkafikiri udikteta utaishia kubagua wapinzani.

Nyerere alisema dhambi ya ubaguzi ni kama kula nyama ya mtu, ukianza huachi.

Magufuli kasema bila aibu kwamba atamkata mtia nia yeyote, si kwa katiba, si kwa miongozo, si kwa taratibu, si kwa utamaduni,bali kwa jinsi takavyojisikia alivyoamka siku hiyo.

Yani kasema wazi yeye ni dikteta.

Kuna vikao ya kumfukuza Membe, anasema hajapeleka mjadala kwenye kikao aliogopa mjadala wa kikao, kamaliza habari mwenyewe katangaza tu. Haoni hata aibu.

Huyu dikteta ataiharibu sana hii nchi.
Poleni sana
 
Anachokitaka ndicho huwa. Na anafanya mambo kwa manufaa yake ya kisiasa. Kwanini nasema haya??

1. Angalia namna mchakato wa uchukuaji fomu za kugombea urais wa JMT ulivyokuwa na figisu. Eti wanaCCM wengine hawaruhusiwi kuchukua fomu. Ni yeye tu.

2. Angalia chaguzi za marudio ktk majimbo ambayo wabunge wapinzani "waliunga mkono juhudi". WanaCCM tulinyimwa kushindana nao. Na hata ktk uchaguzi huu tumepigwa marufuku kushindana nao.

3. Angalia upigaji kura ktk mkutano mkuu, ukusanyaji wa kura ulikuwa wa kimikoa (hii mbinu imewekwa ili iwe rahisi kutufuatilia wale ambao tungepiga kura ya hapana).

4. Kwa kinywa chake mwenyewe amesema kura za maoni za watia nia wa ubunge hazina maaana. Yeye amesema anaweza kumchukuwa hata mtu wa mwisho. Yaani badala ya wagombea kutafuta ridhaa ya wananchi, Sasa wanasubiri maamuzi binafsi ya mwenyekiti.

Demokrasia imezikwa rasmi ndani ya CCM. WanaCCM tunapelekwa pelekwa tu.

Inawezekana wewe ni B Membe, kuanzi kesho tangaza chama unachohamia.
 
Back
Top Bottom