Uchaguzi 2020 Sitaki kuwa mnafiki. WanaCCM awamu hii tunaburuzwa na Mwenyekiti

Bora mmeliona ilo maana alishasema hataki mambo ya shikamoo shikamoo kwaiyo msimchagulie mtu wa shikamoo yeye za kila wakati
 
Ni kupoteza muda kumjadili Magufuli na tabia za kidikteta wakati tunajua katiba yetu na mfumo wa uongozi umetoa madaraka yote (absolute power) kwa Rais wa JMT - tangu kupata uhuru. Muasisi mwenyewe wa mpangilio huu, JKN, alikiri hivyo na kudokeza kuwa yeye mwenyewe angeweza kuwa dikteta mbaya sana kwa katiba iliyopo. Aidha, alitahadharisha kuhusu uwezekano wa kupata kiongozi mbaya sana kwa katiba “hii”. Na hakufanya juhudi yoyote kuleta mabadiliko kwa vile hakutaka CCM iondoke madarakani.

Sasa, kilichoogopwa ndio kimetokea. Kaja Rais “wa ajabu kweli kweli”. Tumeishia kumnyooshea kidole na kusahau kuwa tulikuwa tunaishi na hatari hii siku zote. Magufuli ni symptom tu ya uozo tunaolea wa kukubali kuwa na Rais mwenye absolute powers. Akina BWM na JK nao wamelea mfumo huo kwa jeuri na kiburi ingawa, Leo hii, nao wameishia kuhukumiwa na kudharauliwa kwa kuharibu nchi kiasi cha mrithi wao kudai eti anahangaika “kuinyoosha na kurudisha heshima iliyopotea” huku akifanya vituko vya kila aina vingine vikiwa aibu tupu!
 
CCM siku hizi hakuna mjadala ahaaaaaa kuanzia Kamati kuuu ; NEC hadi mkutano mkuuu

Mwenyekiti anachofanya ni “kuuliza”

Wajumbe mnasemajeeeeeeee?

Wajumbe;- sawaaaaaaa

Mwenyekiti ;-haya imepita

Mwenyekiti:- hapa Nina hoja yangu haukupita Kamati kuu

Mnasemajeeee

Wajumbe :- ndioooooooo

Kwenye ccm walizoea mijadala mizito kwenye ngazi ya Kamati kuuu mizito Sana na hizo ndiooooo zilikua mkutano mkuuu Lakini nako mwenyekiti alitoa nafasi ya mijadala miwili mitatu

Lakini leo tunaona ccm ambayo hadi NEC hawapewi nafasi ya kujadilii hoja na hata wanaojaribu kuleta hoja fikirishi kama yule wa Songwe wanazimwa juu kwa juuu na pengine wakitoka hapo watashughulikiwa .....

Mkutano Mkuu “mapandikizi” yanapata muda wa kuongea Lakini sio mijadala

Alafu wanafurahia kumaliza mkutano wa siku mbili kwa masaaa Matatu tu; that’s a joke
Huu ni uburuzaji

Mikutano ya cc ; Nec na Congress ilikua hadi inakesha sio kuwa walikua wajinga bali ililenga kutoa nafasi ya kutosha ya mijadala toka kwa Wajumbe Lakini leo Wajumbe wanaenda kusema ndioooo tu

Pengine mwenyekiti wa Sasa sio mtu wa kuvumilia mijadala mizito hawezi !!!!
 
Nami nauliza kati ya Lumumba na ufipa wapi kuna misukule?

Maana wasiokubaliana na mbowe wanatoka hadharani na kumpinga ila wasiokubaliana na bwana yule yanawakuta mazito wanabaki kujiinamia chini na kupiga mapambio ya kuabudu, wala hawawezi kujikomboa ki fikra kwa kutetea Yale wanayoyaamini.
Anachokitaka ndicho huwa. Na anafanya mambo kwa manufaa yake ya kisiasa. Kwanini nasema haya??

1. Angalia namna mchakato wa uchukuaji fomu za kugombea urais wa JMT ulivyokuwa na figisu. Eti wanaCCM wengine hawaruhusiwi kuchukua fomu. Ni yeye tu.

2. Angalia chaguzi za marudio ktk majimbo ambayo wabunge wapinzani "waliunga mkono juhudi". WanaCCM tulinyimwa kushindana nao. Na hata ktk uchaguzi huu tumepigwa marufuku kushindana nao.

3. Angalia upigaji kura ktk mkutano mkuu, ukusanyaji wa kura ulikuwa wa kimikoa (hii mbinu imewekwa ili iwe rahisi kutufuatilia wale ambao tungepiga kura ya hapana).

4. Kwa kinywa chake mwenyewe amesema kura za maoni za watia nia wa ubunge hazina maaana. Yeye amesema anaweza kumchukuwa hata mtu wa mwisho. Yaani badala ya wagombea kutafuta ridhaa ya wananchi, Sasa wanasubiri maamuzi binafsi ya mwenyekiti.

Demokrasia imezikwa rasmi ndani ya CCM. WanaCCM tunapelekwa pelekwa tu.
 
Sasa wataja iweje, watu wangepigia kura nafasi ya uenyekiti makundi yangeibuka ndani ya chama.
Na hiyo ni hatari, tusubiri 2025.
 
Mwenyekiti anaongoza kikao vile anavyojisikia utazani yuko kwny kikao cha usuluhishi yeye na mkewe anabwata tu
Kikao cha maamuzi mazito ndani ya chama anaendesha kama kikao cha kuvunja kamati ya send-off/harusi. Sijapenda kabisa.
 
Nami nauliza kati ya Lumumba na ufipa wapi kuna misukule?

Maana wasiokubaliana na mbowe wanatoka hadharani na kumpinga ila wasiokubaliana na bwana yule yanawakuta mazito wanabaki kujiinamia chini na kupiga mapambio ya kuabudu, wala hawawezi kujikomboa ki fikra kwa kutetea Yale wanayoyaamini.
Kuna tofauti kubwa kati ya Mbowe na huku kwingine. Mbowe hana vyombo vya "kumshuhhulikia"anaye asi, lkn huku kwingine vipo. Hakuna aliye tayari kuipata shida hii.
 
3. Angalia upigaji kura ktk mkutano mkuu, ukusanyaji wa kura ulikuwa wa kimikoa (hii mbinu imewekwa ili iwe rahisi kutufuatilia wale ambao tungepiga kura ya hapana).
 
Wana CCM Wala hatuburuzwi...kwani siasa NI jambo huria.....

Wana CCM tunauelewa wa siasa kuwa si DINI....kwa hiyo hatujilipui ama kufanya sacrifice kwani;

1.Mwenye USHAWISHI zaidi ya wengine ndiye mshindi.
(Magufuli anaongoza kwa USHAWISHI na katukamata vyema wanachama)

2.Asiye na ushawishi yake huwa ni mawili tu:
(a)Aheshimu maamuzi ya walio wengi.
(b)Ahame chama km Membe ili akatafute nguvu za ushawishi huko nje.

UKWELI NDIO HUO

Ikikukera basi niite KONDOO WA MAGUFULI BIN CCM.
 
Kama umeliona hilo kutokea ndani, basi huku nje ndio kabisaa
 
Anachokitaka ndicho huwa. Na anafanya mambo kwa manufaa yake ya kisiasa. Kwanini nasema haya??

1. Angalia namna mchakato wa uchukuaji fomu za kugombea urais wa JMT ulivyokuwa na figisu. Eti wanaCCM wengine hawaruhusiwi kuchukua fomu. Ni yeye tu.

2. Angalia chaguzi za marudio ktk majimbo ambayo wabunge wapinzani "waliunga mkono juhudi". WanaCCM tulinyimwa kushindana nao. Na hata ktk uchaguzi huu tumepigwa marufuku kushindana nao.

3. Angalia upigaji kura ktk mkutano mkuu, ukusanyaji wa kura ulikuwa wa kimikoa (hii mbinu imewekwa ili iwe rahisi kutufuatilia wale ambao tungepiga kura ya hapana).

4. Kwa kinywa chake mwenyewe amesema kura za maoni za watia nia wa ubunge hazina maaana. Yeye amesema anaweza kumchukuwa hata mtu wa mwisho. Yaani badala ya wagombea kutafuta ridhaa ya wananchi, Sasa wanasubiri maamuzi binafsi ya mwenyekiti.

Demokrasia imezikwa rasmi ndani ya CCM. WanaCCM tunapelekwa pelekwa tu.
Mimi naona mnastahili kuburuzwa, acha awaburure mpaka akili iwakae sawa, kama chama ni chenu na katiba inaeleza wazi (kwa mujibu wa bashiru) kwamba palitakiwa kuwa wagombea watatu ili wapigiwe kura, ilikuwaje mkakubali katiba ikiukwe, anachukua fomu mtu mmoja halafu wakati wa kupiga kura anasimama hapo anawaangalia, nyie kwanini msimtoe awaachie chama ?, Demokrasia ni msamiati mgumu sana kwa sisi waafrika.
 
Back
Top Bottom