Sitaki kuzini: Sijawahi kuona kama ana dalili za kuoa na sitaki kumwambia unioe

kidawisee

Senior Member
Joined
Feb 27, 2020
Posts
143
Reaction score
212
Habari za mida hii ndugu zangu

Nmekuja nipate ushauri maana naona kila ninalotaka kuliweka mezani napangua.

Nimekuwa na mahusiano na kijana mmoja kama miezi miwili hivi au mitatu. Alinikuta sina mtu na tukaanzisha uhusiano (Huyu mtu ananijua na tunajuana maana tumetoka sehemu moja na tumesoma wote primary na alikuwa ananipenda toka primary na baadae huku ukubwani, ila imetokea tumedate mwaka huu.

Mimi ninasali na mwenzangu sio kiivo japo hajawahi kunipa changamoto za mimi kumtafuta Mungu. Nilipoanza nae mahusiano ghafla nkaona kama narudi nyuma kiroho (nimepitia mengi mpaka kujiconnect zaid na Mungu na ndio ilikuwa pona yangu)

Nilirudi nyuma kiroho nikawa namiss mambo mengi ya kanisani japo hakuwahi nizuia. Niseme tu nilirudi nyuma na vita nilivyokuwa napitia mwanzo vilirudi kwa kasi. Nikamuomba anipe space maana nilishindwa kubalance Mungu na mapenzi(alikuja moto maana kunipata aliona kama nini sijui).

Tukaaa week akaniomba kuwa nimpe nafasi atajitaidi kuweka chachu ya mimi kusali, nikarudi tena. Ikaenda nikawa napitia mambo mengi kiroho na kila siku kanisani naombewa na nikaambiwa mlango unaowapa nafasi Adui ni Uzinzi. Nikaletewa ndoto kuhusu uzinzi unavonilostisha(wanaojua mambo ya kiroho wanaelewa) nikaamua kusikiliza na kuacha uzinzi.

Nilichojia hapa ni kuwa niongee vipi na mwenzangu aelewe kuwa sipo tayari kuzini, maana mtu asiyesali ataona kama nachekesha. Asiwaze namuacha kwa sababu nyingine ila sina sababu zaidi ya hiyo.

Ningeweza kusema labda aamue kama ananioa au vipi ila katika story sijawahi kuona kama ana dalili za kuoa na sitaki kumforce wala kumwambia unioe lakini sitaki kuzini. Naombeni ushauri niongee nae vipi.

Ukiona huna ushauri pita tu, Kuna watu wajuaji sana HUMU.
 
Aisee pole Sana . Mbona mwenzetu shetani anakutesea sehem muhimu hivo..... Au ulisha wahi shiriki madhabau za kichawi na kujiwekea nadhiri juu ya papuchi yako.....? Mbona wengine wanapukuchuana na hakuna tatizo .

Ushauri wangu Anza kuanza kujua kwa nini wewe upo hivo na hayo mavitu uliyatoa wapi uyarudishe uendelee kuchakatwa Kama wengine
 
Unapoomba ushauri kwenye social media expect kila aina ya reply. Kwahiyo usiwatishe watu wakati mwenye shida ni wewe. Huu ndiyo ushauri wangu.

Acha uzinzi. Mwambie mfunge ndoa ndiyo mfanye sex (marital sex). Kama hataki achana naye. Pia, acha uzinzi kabisa la sivyo huwezi kumwomba Mungu wakati huohuo uko kwenye uzinzi. Naomba pia nikuulize kitu. Kwani huko makanisani lazima mtu fulani akuombee?Kwani hamuwezi kujiombea wenyewe?Au Mungu wenu anasikia tu endapo utaombewa na mdhambi mwenzio?All the best
 
Asante kwa ushauri...
 
Tunajiombea wenyewe,ila kuna mda mtu anashindwa kuomba kutokana na hali atakayopitia wakati uo.Ndio maana Mungu alisema,popote mtakapokusanyika kwa jina langu,ntakuwepo.Alimaanisha huwezi kuomba peke yako.
 
Una umri gani?!

Wazazi wako, wote wapo hai au mojawapo, kama wote wapo hai je wanaishi pamoja?!

Unaishi mkoa gani?!

Mpo wangapi kwenu?!

Una elimu kiwango gani?!

Unajishughulisha na nini?!

Huyu kijana na yeye upande wake ukimjibia haya maswali yupo vipi?!

Ukiyajibu haya maswali kwa pande zote mbili, then nitaweza kukupa picha.
 
As long as umeshajua kinachokulostisha ni uzinzi, na huyo ulienae hana muelekeo wa ndoa na hakuelewi sababu zako za kukataa uzinzi basi ni simple achana nae Mungu atakuletea mtu sahihi, na kama itakua ndie Mungu aliekupangia basi atarudi na atakuelewa

Alafu ushajua huwezi uzinzi, before hujaingia kwenye mahusiano mueleze mtu kabisa afanye machaguzi ya kubaki au kuondoka akiwa anajua msimamo wako, vinginevyo

Usiyachochee mapenzi mpaka yatakapoona vema yenyewe
 
Binafsi nikiwa najua kabisa siko sawa, hata kanisani siendi kabisa. Inaniwia hukumu sana na kujutia. Naona bora nikae pembeni kwanza.

Amua moja, Kaisari au Mungu, hauwezi kupata vyote kwa pamoja. Chagua kuwa moto au baridi, vuguvugu utatapikwa tu, hakuna namna.

Ulishaambiwa bora ulitoe jicho lako au kiungo chako kinachokukosesha kuuona ufalme wa Mungu kuliko kwenda na viungo vyote motoni.

Maamuzi unayo mwenyewe...

Lakini pia usimsahau Mzee Mwinyi "... Haaapo...ndipo pabaaya.."

Kila la kheri
 
Baelezee baelezee baelewe...vinginevyo badamu batamwagika
 
As long as umeshajua kinachokulostisha ni uzinzi, na huyo ulienae hana muelekeo wa ndoa na hakuelewi sababu zako za kukataa uzinzi basi ni simple achana nae Mungu atakuletea mtu sahihi, na kama itakua ndie Mungu aliekupangia basi atarudi na atakuelewa

Alafu ushajua huwezi uzinzi, before hujaingia kwenye mahusiano mueleze mtu kabisa afanye machaguzi ya kubaki au kuondoka akiwa anajua msimamo wako, vinginevyo

Usiyachochee mapenzi mpaka yatakapoona vema yenyewe
Sawa mkuu,mwanzo sikuichukulia hii dhambi kama inaweza nifarakanisha na Mungu,kwa sasa nmetambua na ndio maana nmeamua kuiacha.
 
Una umri gani?!

Wazazi wako, wote wapo hai au mojawapo, kama wote wapo hai je wanaishi pamoja?!

Unaishi mkoa gani?!

Mpo wangapi kwenu?!

Una elimu kiwango gani?!

Unajishughulisha na nini?!

Huyu kijana na yeye upande wake ukimjibia haya maswali yupo vipi?!

Ukiyajibu haya maswali kwa pande zote mbili, then nitaweza kukupa picha.
Mkuu vita naijua na nnajua na yametokea mengi sana mpaka mimi kusali,Niliomba ushauri jinsi ya kumwambia mwenzangu kuwa sihitaji uzinzi.
 
Binafsi nikiwa najua kabisa siko sawa, hata kanisani siendi kabisa. Inaniwia hukumu sana na kujutia. Naona bora nikae pembeni kwanza.

Amua moja, Kaisari au Mungu, hauwezi kupata vyote kwa pamoja. Chagua kuwa moto au baridi, vuguvugu utatapikwa tu, hakuna namna.

Ulishaambiwa bora ulitoe jicho lako au kiungo chako kinachokukosesha kuuona ufalme wa Mungu kuliko kwenda na viungo vyote motoni.

Maamuzi unayo mwenyewe...

Lakini pia usimsahau Mzee Mwinyi "... Haaapo...ndipo pabaaya.."

Kila la kheri
Aaahaaa,sawa The Monk,nmeamua kuacha uzinzi.
 
Sawa mkuu,mwanzo sikuichukulia hii dhambi kama inaweza nifarakanisha na Mungu,kwa sasa nmetambua na ndio maana nmeamua kuiacha.

Na kama umeamua kuacha acha kabisa na ufunge milango yote unayoweza kuikaribisha hiyo dhambi ndani yako..

Lakini pia usiogope ikitokea umeteleza Mungu wetu ni wa Rehema ukitubu anasamehe, usiogope mchungaji akikwambia Mungu amekukasirikia
 
Asiwaze namuacha kwa sabbu nyingne ila sina sabbu zaidi ya Iyo.Nngeweza kusema labda aamue kama ananioa au vipi ila katika story sijawahi kuona kama anadalili za kuoa na sitaki kumforce wala kumwambia unioe sitaki kuzini.Naombeni ushauri niongee nae vipi.
Kwanza huwezi kumzuia mtu asiwaze kile anachotaka kukiwaza, atawaza na atasema kila anachojisikia kukisema, ni wewe kuamua kumsikiliza au kuamua kumsikiliza MUNGU wako, the choice is yours.
 
Back
Top Bottom