Uchaguzi 2020 Sitampa kura yangu Dkt. Magufuli kwa sababu hii 'kubwa'

Uchaguzi 2020 Sitampa kura yangu Dkt. Magufuli kwa sababu hii 'kubwa'

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2010
Posts
6,137
Reaction score
17,908
Sina haja ya kusubiri kampeni zianze ili nishawishike. Sina haja ya kuuficha ukweli huu. Mwaka 2015, nilimsambaratisha Lowassa na kumpigia kura mgombea wa CCM yangu Dr.John P. Magufuli. Baada ya miaka yake mitano madarakani, nimekata shauri kuwa SITAMPIGIA KURA. Kupiga au kutopiga kura kwa mgombea, kwa kila mtanzania, kuna sababu yake. Kwangu mimi kinachonivutia ni kuongoza kikatiba, kisheria, kikanuni na kistaha.

Mimi Mzee Tupatupa, kada mwandamizi wa CCM, SITAMPIGIA KURA Dr. Magufuli pamoja na kuwa ni mgombea wa chama changu. Kitendo chake na kauli zake za KUHODHI FEDHA za Serikali kimenifanya nitafakari na kuamua nilivyoamua. Dr. Magufuli amejipambanua kama 'mmiliki pekee' wa fedha za nchi hii zilizopaswa kusimamiwa na Bunge. Kila apitapo, husema kuwa 'ninawapa/ninawaletea' kiasi fulani za fedha kana kwamba fedha hizo ni zake binafsi.

Kitendo cha kuhodhi hivyo kimezalisha watanzania wanafiki na watu wa kujipendekeza. Utawasikia: 'Rais ametuletea shilingi....... kwa ujenzi wa madarasa; Rais amekubali kutuletea shilingi....kwa ajili ya barabara' na kadhalika. tena utawasikia: 'Rais ametujengea…...', 'Rais amejenga…..'.Hapo Rais anachorwa kama aliyehodhi mfuko wa Hazina na fedha zote za Serikali . Hili si jambo la kuliunga mkono wala la kumpa kura mgombea wa aina hii.

Fedha za nchi zina utaratibu wake wa kukusanywa, kutumika na kukaguliwa. Kuhodhiwa na mtu mmoja si jambo jema wala la kuungwa mkono. Kuwa kiongozi wa Serikali hakutoshi kumfamya mhusika kuhodhi fedha zote za umma. Kwa hilo tu, SITAMPIGIA KURA. Haya ni maamuzi yangu binafsi.

Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa jijini Dodoma)
 
Hongera sana mzee Tupatupa na siku zote mimi binafsi Mmawia huwa sina kigugumizi kukusifia hata kama tuna tofautiana kiitikadi.
Akiandika ukweli ule mchungu ukawii kulaumu, napata wakati mgumu kujua wafuasi wa upinzani wanasimamia wapi linapokuja suala la maslahi mapana ya nchi na yenye tija kwa vizazi vijavyo
 
Hii pia ni sababu ya anguko la Magufuli, ile kujifanya bila yeye mambo hayaendi. Yaani anataka kujipa umungu angali yeye ni binadamu. Eti kwamba bila yeye mambo hayaendi.

Wananchi wajumbe tutaongea kwa sauti moja
 
Kila siku nakagua kitambulisho changu cha kupiga kura baada ya kuhakiki jina langu kwenye kituo cha kupigia kura ili kujiweka sawa na siku hiyo.
Sihitaji kampeni ili kutoa maamuzi. Nimekwisha Fanya. Naendelea na kuwahamasisha wengine waniunge mkono kwa kuwanyima kura wagombea wore wa ccm. Sababu ni nyingi, lakini inayonisukuma ni kitendo cha ubaguzi wa serikali hii kuwanyima mikopo ya elimu ya juu baadhi ya waombaji, tena wenye sifa.
 
Hii pia ni sababu ya anguko la Magufuli, ile kujifanya bila yeye mambo hayaendi. Yaani anataka kujipa umungu angali yeye ni binadamu. Eti kwamba bila yeye mambo hayaendi.

Wananchi wajumbe tutaongea kwa sauti moja
Hakuna sauti ya kumtoa Rais Magufuli mwaka huu , tusidanganywe na sauti za wale 'wapayukaji'
 
Back
Top Bottom