Uchaguzi 2020 Sitampa kura yangu Dkt. Magufuli kwa sababu hii 'kubwa'

Uchaguzi 2020 Sitampa kura yangu Dkt. Magufuli kwa sababu hii 'kubwa'

Hata mimi sitasubiri kampeni kushawishika na chochote.

SITAMPA MAGUFULI KURA YANGU NA YA FAMILIA YANGU NA NDUGU ZANGU NI HIVYO HIVYO.

Magufuli ametufunga mdomo wote anataka yeye tu ndie asikike na kuwa kama mungu wa nchi hii.

Ona alivyominya uhuru wa vyombo vya habari, hadi hata kusikiliza BBC, VOA, DW n.k mpaka tupate kibali kutoka kwake!! Siwezi kukubali Tanzania yangu ifikishwe shimoni na gizani namna hii kwa maslahi binafsi na mtu mmoja...NEVER...NEVER..!
 
Riziki anatoa Mungu, lakini anayegawa ni mwanadamu.. Magufuli ni mgawaji mkuu wa riziki iliyotolewa na Mungu katika ardhi hii ya Tanzania.
Yanaweza yakatokea maafa sehemu fulani mathalani; Singida, Mo akatoa magunia 100 ya mchele.. Lakini siye yeye atakayeenda kugawa.. Kuna watu kule kwenye maafa ndio watagawa hivyo kuamua huyu apate kilo moja na yule apate kilo mbili japo sio wao waliotoa.. Kwa hiyo mgawaji naye ana nafasi kubwa kuamua upate riziki kiasi gani!
Pesa zinaweza zisiwe za Magufuli lakini yeye ndiye anayehusika kuzigawa.
 
Eeee Mola wa Mbingu na Ardhi
Mlinde Mja wako(Rais wetu huyu) na muongoze njia ya sawa
Mpe Mafanikio katika kazi zake na maisha yake
Mpe mwisho mwema na furaha ya Kudumu
 
Magufuli yuko sawa kwenye matumizi ya fedha.. hasa miradi ya maendeleo. Namsapoti kwa hilo, ilo bunge unalotaka lisimamie mapato na matumizi ndio bunge hili hili la Ndugai? Hapana... Big NO! hata hivyo kwa mimi kura hatopata kwa sababu ya Ufalme, umimi, kuminya demokrasia na uhuru wa habari! Nimesikia mgombea mmoja akisema jambo la kwanza akichaguliwa ni kuvunja Habari maelezo, Bunge live na kurejesha Uhuru wa Kujieleza.. Huyo atapata kura yangu... Na hii ni kwa sababu maendeleo bila uhuru, haki na demokrasia hayana maana! Huwezi kuvuruga upinzani kwa sababu tu una dola ukadhani unaitendea nchi haki.. hapana, unaturudisha utumwani na unaumiza hisia za wengi, siku hizi ufuasi wa vyama ni kama imani tu!
 
Wapiga dili mmevumilia mpaka mmeona mtoe povu. Mlizoea kuzichota, sasa hamna mwanya mnatapatapa.

Kura yako hiyo moja haiwezi kumnyima ushindi. Kwanza inaweza kuwa ni kati ya zile zinazoharibika.
Wewe kula na kulala kwako kunategemea posts ulizo jibu JF. Haya kachukue Bk 7 zako
 
Utampigia Nani mkuu. Mana Kura ya mtu Ni Siri Sasa umeamua kumwaga mboga, Malizia na Ugali
 
Duh Mzee Tupatupa, hii ni hatari sana kwa mgombea wetu kwasababu kura yako ndio the determinant vote ya kumfanya JPM arejee Ikulu kwa kushinda urais!.

Kama ingekuwa bila wewe kumpigia kura yako rais Magufuli, then hawezi kushinda urais, hapo tungekubembeleza na lukupigia magoti tuipate kura yako!, JPM ashinde, lakini kwa vile Watanzania wana macho yanaona na masikio wanasikia, wameona na wanasikia, wanajua wanataka nini na ni nani atawapatia wanachotala, hivyo hiyo October, wanajua wachague nini na wanamchagua nani.

Hivyo Mzee Mwenzangu Tupa Tupa, you can as well, just go to ... with your single, tiny, insignificant piece of sand kwenye ufukwe wetu wa mafuriko ya ushindi.
Wish you all the best!.
P
P, najua moyoni humpendi JPM.
Ila imebidi uulaghai moyo ili uendelee kupata riziki, vikao vya chama vijavyo.
 
Mfalme Suleiman aijaliwa utajiri mkubwa, madaraka makubwa, alikuwa na wanawake wa ndoa na Masuria wa kutosha.
Mungu alimuuliza mfalme Suleiman baada ya hayo yote ni kupe nini?

Mfalme Suleiman alimjibu Mungu, haya yote uliyonijalia niona ni upuuzi mtupu ila sasa naomba unijalie Hekima na Busara.

Kamwe katika Historia Kiongozi hatakumbukwa kwa Utajiri au wa Inchi yake bali kwa Hekima na Busara katika kuwaongoza watu wake.
Hekima na Busara hulenga kwanza maendeleo ya watu na si vitu.

Maendeleo ya vitu ni matokeo ya maendeleo ya mtu na si msingi wa maendeleo ya mtu.
 
Inawezekana ulituletea kura yako kipindi tunaihitaji..asante kwa hilo..kwa sasa wape wengine tu ili nao wajione watu.
 
Tangu lini ukamuunga mkono JPM? Mpelekee kura Membe wako utaenjoy mno..
 
Naunga mkono hoja, mimi na familia yangu tulisha amua siku Lissu anachukua fomu ya uteuzi kuwa kura zetu ni kwake.
 
Duh Mzee Tupatupa, hii ni hatari sana kwa mgombea wetu kwasababu kura yako ndio the determinant vote ya kumfanya JPM arejee Ikulu kwa kushinda urais!.

Kama ingekuwa bila wewe kumpigia kura yako rais Magufuli, then hawezi kushinda urais, hapo tungekubembeleza na lukupigia magoti tuipate kura yako!, JPM ashinde, lakini kwa vile Watanzania wana macho yanaona na masikio wanasikia, wameona na wanasikia, wanajua wanataka nini na ni nani atawapatia wanachotala, hivyo hiyo October, wanajua wachague nini na wanamchagua nani.

Hivyo Mzee Mwenzangu Tupa Tupa, you can as well, just go to ... with your single, tiny, insignificant piece of sand kwenye ufukwe wetu wa mafuriko ya ushindi.
Wish you all the best!.
P
Kura 1 inaweza kukufanya uwe rais au uukose urais.ukilijua hilo basi utamwelewa tupatupa
 
Back
Top Bottom