Inaendelea............
.....ili nitoe pullover nivae kwa ajili ya kujikinga na kibaridi kilichokuwa kinachoma mwilini mpaka tumboni. Nilikaa pale kwa muda wa saa hivi kisha nikabeba mabegi yangu kuelekea kuitafuta breakfast maana tokea nilipokuwa nimekula jana saa moja usiku nyumbani kabla ya safari sikuwa nimekula tena hivyo nilikuwa nina njaa sana na hivyo nilichukua mabegi yangu nikaanza kupiga hatua za harakaharaka kuitafuta cafeteria moja ambayo haikuwa mara yangu ya kwanza kwenda kupata chochote pale, ilikuwa inaitwa Kishusi sijui Kama bado ipo maana kipindi kile ilikuwa inajitahidi sn kupika na kuuza vyakula vizuri sana vya kishua mjini Bk.
Nilikuwa na wasiwasi maana nilihofia kuwa huwenda wangekuwa hawajafungua lakini nilipofika nilikuta tofauti, nilisukuma mlango wa kioo kisha nikaingia. Niliagiza chai ya maziwa na kababu tano, nikazifuta zote mpk vile visalia vya vipande vidogovidogo vya nyama vilivyokuwa vinabaki kwa sahani nilifuta kabisa. Muhudumu alipokuja kunitajia bill nilijivuta nikasukuma kiti nyuma, ili nipate nafasi ya kumpatia pesa yake. Nikiwa nimekaa niliinama nikaelekeza mikono yangu mguu wa kulia kwenye raba yangu ya Nike nikafungua kamba zake kisha nikashusha soksi chini nikapenyeza mkono kwenye unyayo Kisha nikachomoa pesa noti za rangi ya bluu, miaka hiyo 10k note ndo ilikuwa mekuwa introduced na BOT, nilichomoa moja nikamkabidhi yule dada, muda wote huo alikuwa amepigwaa na butwaa alivyokuwa anashuhudia kile kitendo cha kuchomoa pesa kwenye viatu. Sikumbuki kwakweli nilitumia kiasi gani na chenji ilibaki kiasi gani Ila baada ya kunirejeshea chenji ilibidi nitumie dakika chache sn kutenga nauli na pesa ya kutumia ninapokuwa njiani ili nikishafunga buti (kiatu)nisianze kufungufungua kila mara.Niliwaza kujiondolea usumbufu. Ikumbukwe kuweka hela chini ya nyayo ndani ya soksi nilikuwa na sababu na nilishazoea kufanya hivyo siku zote za safari yangu ya kuelekea shule. Mguu wa kushoto niliweka ada ya shule na sikuwa nimegusa eneo hilo tokea nilipoiweka nikiwa home baada ya kupewa na mzee, na kulia nilihifadhi pesa ya matumizi.
Wakati huo ilishafika saa mbili kasoro, nikapiga hatua chapchap kurudi standi,kipindi kile magari ya abiria yalikuwa ya kuokotaokota Sana kuelekea huko wilayani hivyo Mimi nilishazoea kupanda kwa kuunga unga na siku hiyo nilipofika eneo hilo nilikuta usafiri unaoelekea Mutukula mpakani kabisa mwa Tanzania na Uganda. Nilipanda lile gari na tulipofika Kyaka kabla ya daraja walinishuka pale ili nisubirie usafiri wa kuunga angalau unifikishe Karagwe wilayani, kisha nikifika pale nilale ili nianze tena safari ya kuunga unga mpaka nifike mwisho wa safari yangu.
Nilikaa Kyaka takribani masaa matatu sikuwa nimepata usafiri, yakipita magari matatu ya abilia lakini yalikuwa yamejaa. Nakumbuka gari za abiria mara nyingi zilikuwa ni Land lover. Pia magari binafsi pamoja na ya Mashirika ya Umoja wa mataifa kama UNHCR, Calitas, UNICEF, Help Age niliyashuhudia yakipita nilikuwa nayasimamisha but hayakuwa yakisimama. Sikukata tamaa niliendelea kusubiri, lakini nikiwa pale niliona nijisogeze kwa mmoja wa vijana wengi waliokuwa wanauza ndizi za kuchomo kule zinaitwa gonja tamu sana i see, nilikula kadhaa huku nikisukumia na soda yangu bariiidi kabisa ndizi mbili tu nikatosheka zingine nikahifadhi kula huko mbele ya safari. Nilikaa Kyaka mpaka saa tisa hivi ndipo gari binafsi iliposimama kisha tukapanda na abilia wachache waliokuwepo pale nakumbuka ilikuwa double cabin, wote tulipanda nyuma
Tulianza safari bila ya kuchelewa,
kipindi hicho barabara zilikuwa mbaya, mbaya mbaya kabisa mashimo kwa kwenda mbele na ukichanganya na kipindi hicho mvua zilikuwa zinanyesha mkoani Kagera barabara zilikuwa hovyo kabisa. Kadiri tulivyokuwa tunaiacha misenyi ndivyo jua lilizidi kuelekea usoni kwetu kwa maana ilikuwa linaelekea magharibi.
Baada ya kuwa tumevuka vilima na mabonde na Safari yetu ikingali inaendelea magari yaliyokuwa yanatokea upande tunakwenda sisi yalikuwa hayaji tena, hatukuwa tukiyaona kupishana nayo kama ambavyo ilikuwa hawali ama kipindi kile bado niko Kyaka nasubiri usafiri.Kwa ujumla nilifikiria kuwa ni kwasababu ya muda kuwa umekwenda. Kitu kilichonishangaza ni yale magari ya abiria yaliyokuwa yamenipita pale Kyaka stand na yalishatembea muda mrefu lakini tuliyapia, Ila nilijiambia moyoni kuwa sababu ni mabovumabovu ndio maana tumeyacover na kuyapita.
Tuliendelea na Safari yetu lakini kilomita chache za mwendo tulikuta gari moja limekwama kwenye dimbwi la tope katikakati ya barabara na hivyo likasababisha tushindwe kuendelea na safari kwa kuwa liliziba njia. Tulikaa hapo kwa muda kama wa nusu saa na muda huo yalishafika magari mengi yaliyokuwa yanasubiri njia iwe wazi. Watu tuliokuwa eneo hilo tuliokuwa tumeshuka kabisa kwenye magari yetu tunalandalanda tu huko na huko wakati huo ni saa kumi na mbili jioni. Nikielekea kwenye bag langu nikafungua mfuko wa pembeni nikachukua kidevice changu Cha kuchezea cassette nikatia cassette moja ya 2pac Omary Shakur kisha nikachukua headfone zangu nikaziseti juu ya masikio barabara (Kama DJ vile) nikaanza kula hip hop kali za moto sana kipindi hicho nikikoshwa zaidi na kibao cha 'Dear Mama'
Ile naanza kuenjoy biti nilishtushwa na milio ya risasi .....papapu..papapaa..... zilipigwa mfurulizo Kama dk 5 hivi tena zilipigwa kutokea both sides yaani kule tulikotokea na huko tunakoelekea, sikujua zile headfone ziliacha kichwa muda gani zaidi nilipokuwa nazungusha macho huku na huko niliyaona mabandidu yanameshika siraha yanahamrisha watu tulale kifudifudi muda wa sekunde kadhaa eneo kulikuwa kimyaa.
Mabandidu yakajichukulia utawala wa gafla Katika kale kaeneo tukiwa tumelazwa pale nilishtushwa na mtu akiniinua Kama sisimizi maana alishika ile kofia ya 'pullover' ilivyokuwa imelalia nyuma ya kisogo akanivuta kisha nikamtizama usoni jamaa lilikuwa limevalia siraha Ina mkanda kama wale waasi wa M23, I see jamaa lilinistua na banzi (kibao)moja heavy la usoni, nikaziona nyota na rangi za bluubluu ilochanganyika na rangi ya damu wakati huo akili yangu ikanituma kuwa sikutaka nimtizame usoni though alikuwa amejifunika uso. Kabla sijatafakari nisali Sala gani nikashangaa mtu ameleta gunia akanivika, nilistuka gunia linanivaa, nikajua nimekwenda na maji.
Ubongo wangu ukiwa umefeli kutafakkari niliishangaa wanaletwa watu wengine sikujua ni wangapi Ila nilikuwa nasikia vishindo kuja kwangu Kisha tukaambiwa kwa kiswahili kibovu 'Mutu hakuna kutembeya' Mimi kila kiungo kimoja kilikuwa hakina mawasiliano na kingine maana kwanza nilikuwa mdogo na ndiyo mara ya kwanza nasikia milio ya risasi. Nilikuwa natetemeka Kama generata bovu kuzidi yale majenerata ya mgao wa Umeme ya tanesco.
Kipindi chote hicho nilikuwa nimefunikwa gunia, Kuna Yale magunia ya enzi hizo yalikuwa yanatengenezwa na katani. so hewa ilikuwa inapita na muda wote ule tokea nimepigwa like Kofi nilikuwa nimefumba macho kwa uoga.Lakini nilikaza moyo baada ya kuhisi majamaa yamesogea hatua chache kutoa pale nilipo nikafumbua macho, kupitia kwenye gunia nikaona mabandidu kama wanasearch magari kwa haraka haraka kisha ndio nikaona pembeni yangu tuko kama watano hivi tuliosimama.Hapo hapo bandidu moja likasogea pàle tuliokuwa huku limetulenga na bunduki sikuwa na mawasiliano ya mwili Ila nilihisi mkojo unateremka kutokana na kuhisi maji ya Moto yakiteremka kutoka saizi ya kiuno Hadi chini kwenye viatu. Jamaa alipokaribia na sisi akapiga risasi (nahisi juu) Kisha Mimi miguu ikaishiwa nguvu nikahisi nimepigwa mimi, nikadondoka chini. Chakushangaza jamaa akaja akaniinua tena akanitoa lile gunia kisha akanambia "we mwana we ntakupiga 'rishashi' cha ajabu nikahisi nguvu zimenirejea maana nilidhani ile risasi amenifyatulia mimi na tayari nimeshakufa kumbe nilikuwa hai sina hata jeraha. Basi wale wenzangu nao walikuwa wanapita wameshika magunia yao nyuma yao kuna mabandidu yanasimamia zoezi kama ilivyokuwa kwangu. Mimi nilikuwa mdogo lakini nashangaa hata leo kwanini Yale majamaa yalining'ang'ania kunipa gunia?? Waga najiuliza Sana, kisha wakawa wanatupitisha kwa abiria pâle walipolazwa, ukifikiwa unaamrishwa utoe ulichonacho kila kitu uwe na pesa saa nzuri unatia kwenye gunia hakuna kupoteza muda.Zoezi hilo likiwa linaendelea wakati huo mateka unatekeleza zoezi kichwa ukiwa umeinamisha chini , mijamaa ikawa inasema ukiinua kichwa unakula 'rishashi' Nakumbuka hili jina rishashi mpaka Leo jinsi walivyokuwa wanatamka neno 'risasi'
Ikumbukwe kitendo kile kilichukua dk zisizozidi ishirini hv, na sehemu walipotutekea ilikuwa ni sehemu ya Kona maana waliokuwa wanatokea tunakokwenda walikuwa hawawezi kuona kuna nini kinaendelea na hata waliokuwa wanakuja wasingejua kutokana na ile kona ambayo pale Kati ndio hiyo ambushi ilipofanyika.
Basi, baada ya like tukio kukamilika waliamrisha watu kulala kimya tena uso chini Kisha wakatwambia sisi wenye yale magunia kwa ukali kilammoja abebe furushi alilonalo tuanze kukimbia kufuata njia kuelekea kwenye msitu. Kiukweli hapo ndipo nilianza kuwaza sitawaona tena Baba, Mom, na ndg zangu, tena nilianza kuwaza ninapotea kwenye uso wa dunia bila kutambliwa nimefia wapi. Uso wote ulijaa machozi, tumaini likapotea tukabebeshwa yale maroba ya vitu na wao walikuwa wamebeba mamizigo kibao waliopora kwenye magari, safari ya maisha nisiyoyafahamu ikaanza, nikakata tamaa, nikakosa tumaini, mwili ukazidi kuvibrate, miguu ikawa inagongana gongana kama mtoto aliyeugua utapiamlo,akili yangu itaitengeneza taswira ya mama angu machozi yakajaa machoni hata kushindwa kuona vema, moyoni mwangu nikahisi kutamka jina langu Mara tatu....Derick....Derick......Derick (Code) why was I born??!!
Itaendea...
Muendelezo soma
Sitasahau nilivyonusurika kuchukuliwa mateka na majambazi mkoani Kagera