Ilipoishia....
.......nikakaa kwa kutulia ili nisikilize vizuri, jinsi dk. zinavyoenda ndivyo kengele inaongezeka nikakimbia kupanda juu ya mti.....
Inaendelea.......
Baada ya kuwa niko juu ya mti nilirusha jicho la upelelezi kutazama nini hicho kinakuja huku kengele ikigongwa? katikati ya nyasi ndefu kwa mbali nikaanza kuona mipembe mirefu mirefu mingi sana ikiwa inakuja eneo nilokuwepo, kumbe yalikuwa makundi makubwa ya ng'ombe wakiwa machungoni. Ile kengele ilikuwa inavishwa kwa dume kiongozi ndiye aliyekuwa anawaongoza ng'ombe wenziye.
Nilijiskia furaha sana baada ya kuwaona wale ng'ombe nilijua fika kwamba sasa angalu siko mbali na vijiji au makazi ya watu. Kwakuwa wale ng'ombe walikuwa ni wengi na walikuwa wanakuja uelekeo wangu nikaona si busara kushuka kwenye mti nisubiri kwanza wapite kwa huo mti kisha nishuke, maana niliogopa wangeweza kunichoma na zile pembe zao. Ndugu msomaji, ng'ombe wale walikuwa na pembe ndefu sana. Nilikuja kujua baadae kuwa ng'ombe wa namna hiyo ni aina ya ankole wanafugwa zaidi maeneo ya Uganda, Rwanda pamoja na Burundi.
Baada ya kuwa wameupita ule mti niliokuwa juu yake nilishuka nikiwa na tumaini la kuwa sasa niko salama na hapo nikawa natazama huku na huko ili niwapate wachungaji lakini sikuona mtu. Ngo'mbe walikuwa wanajilisha wenyewe. Sikukata tamaa nilivuta subira nikiwa na tumaini la kuwaona muda wowote maana nilikuwa najipa moyo kuwa ng'ombe wale wote wasingekuwa porini bila wa kuwachunga. Nikijipa moyo kuwa uwenda Mchungaji/ wachungaji wamepumzika 'somewhere in the bush' Niliendelea kutizama sikuona mtu. Kwakuwa nyasi ni ndefu green sana nikawa na shaka kuwa nisiendelee kubaki pale chini, nipande tena juu ya mti uwenda wachungaji wako upande mwingine wa eneo tofauti na lile nililokuwa nipo.
Nikapanda tena kwenye mti nikaangaza macho pande zote sikuona mtu, nikaamua kubaki pale juu niliendelea kusoma mnara but sikuambulia kuona mtu yeyote. Ikumbukwe wale ng'ombe wanakula majani huku wanasonga polepole hivyo nikajikuta nazidi kuachwa hatua, harakaharaka mawazo yakanijia kwanini nisishuke niwafuate hao ng'ombe? kweli nikashuka nikafikiria lakini kwanini niwafuate,kwanini nisiendelee na safari yangu tu, nipuyange nitakapoishia ndio hukohuko. Wazo jingine likalipinga hilo la mwisho maana niliona nikipuyanga tu bila ya kuelewa naelekea wapi na kwa kutizama muda ulikuwa unazidi kwenda, nikaona nikifanya mzaha nalala porini na mwisho wa siku nakuwa mgeni wa wachawi kama ilivyokuwa usiku wa siku iliyopita.
Wazo lilikuwa ni moja tu kuwafuata ng'ombe hakuna kingine. Nilijiambia kuwa lazima hawa ng'ombe wana wenyewe, haiwezekani kabisa wawe machungoni peke yao. Nikaamua kushikilia msimamo wa kuwafuata. Kiujumla walikuwa wameshasogea kiasi maana kwa kukadiria ingeweza kuwa umbali Sawa na urefu wa mita Mia tatu ama urefu wa viwanja vitatu vya mpira wa miguu.
Nilianza kuwafuata nikiwa kwa mbali kutokana na kuwa wale ng'ombe walikuwa wanaongozana na mbwa wengi wengi hivyo nilikwenda kwa tahadhali sana. Sikuwa nawakaribia kabisa nilimaintain kukaa mbali mita za kutosha. Pamoja na kutembea hatua za kutosha kutokea kule ng'ombe walikonikuta na kuniacha bado sikuwa nimemwona mchungaji, Niliishangaa Sana. Kwa kuwa nilishacover distance na wale ng'ombe nao wametulizana hawatembei kama hawali nikaamua nikae nipumzike njaa nayo ilikuwa kama yote. Niliangalia huku na kule walau nione hata tunda lolote sikuona chochote. Nikajisemea acha nijikaze tu, nikajisogeza karibu kabisa na mti kisha nikaseti mgongo juu yake nikajiegemeza. Nikiwa pale ubongo wangu ulianza ku- rewind matukio yote namna yalivyonitokea nikawa najiuliza wale mateka wenzangu mwisho wao ulikuwaje n.k....n.k, Nilifikiria namna gani nyumbani hawana habari na maswahibu yale ya kutisha yaliyokuwa yananikuta. Nikafikiria mabegi yangu na kila kitu kilichokuwemo nikaishia kusikitika kwa uchungu mwingi. Nikiwa niko kwenye lindi la mawazo usingizi ukanipitia.
Ndoto....
Nikiwa usingizini nilifunikwa na njozi.....Kwamba Mimi, Jasmine (code), Viviana(code) na Shansy (Jina halisi) la toto la Kinyarwanda, Mama ake alikuwa anafanya kazi BENACO katika kambi ya wakimbizi.
(siku moja ntawaletea hapa uzi kuhusu kisa changu na huyu binti Chansy ambaye alinifanya nifike mpaka Rwanda baada ya kuwa nimeoza na kunuka kimapenzi juu yake
hata baada ya kumalizia shule. Nikisa Cha kusisimua )
Tuendelee....
wote hawa walikuwa mademu niliokuwa nasoma nao pale shuleni, wote hao walikuwa mademu zangu Jasmine na Vivy hawa tulikuwa tunasoma kidato kimoja, Jasmine nikiwa naye mkondo 'A' na Vivy alikuwa 'B' Ila Chansy alikuwa nyuma yetu.(Sijawahi kuwasahau hawa na sitakuja kuwasahau)
Nirudi kwenye ndoto...........................
Basi sote wanne tulikuwa mbele ya wanafunzi baada ya kugongwa kengele ya dharula kisha shule nzima wanafunzi wote Wakassemble.
Tukiwa pale mbele na walimu wote kasoro Headmaster, Ilikuwa nafasi ya discipline Master kutoa hutuba juu ya kutufukuza shule wote wanne baada ya kugundulika Mimi na wale mademu wote watatu tulikuwa tunajihusisha na mapenzi shuleni na hii ilitokana na wao kuchapana makonde bwenini baada ya kugundua na kutambuana wote kwa pamoja kuwa niliwapelekea zawadi za pafyum
Mwalimu wa nidhamu alianza kuwatangazia wanafunzi....
Discipline Master: " Students, as you see ..... beside me are your fellow ladies and this one cow here, .......he has been trying to transform what is in the novel that you use to have for your learning...which is called Three suitors one husba...., "Kabla hajahitimisha wanafunzi wote wakachekaaaaa
Kisha mwalimu anaendelea.....
He wants to show us that his penis sting bittersweet than that of the bee is.
"Now.. as far as our school disciplinary rules and procedures are concerned, This Derick, concomitantly with his tri-wives are all finally dismissed from schoo....kabla hajamaliza nikashtuka kutoka usingizini, nikakurupuka haraka, nikawa naona mawenge wenge nikaanza kutamka kwa sauti ya ndani yenye mashaka mengi ng'ombe....ng'ombe....ng'ombe....jamani, nikaangalia huku na huko sioni kitu nikakimbia kimbia huku nikiwa nimepagawa nikiangalia mazingira yalionekana kama jioni jioni maana hata hali ya hewa ilikuwa ya mawingu jua halionekani kabisa. Nikawa siamini amini kilichokuwa kinaendelea.
Baada ya sekunde chache ikabidi nijiweke kwenye utulivu, nikasoma mazingira nikawaza hawa ng'ombe si wakati najiegemeza kwenye mti walikuwa mbele yangu, kwa hiyo acha nichukue uelekeo huo huo. Kutokana na kisa cha wachawi cha jana yake sikuhitaji kabisa kuona nalala sehemu isiyo na watu, sikutamani kabisa hata kulikumbuka lile tukio la kuogofyaa, sikuhitaji kumezwa na misitu.
Nilianza kupiga hatua ndefu ndefu pale porini, Kisha nikaanza kukimbia nilikuwa nahisi kuwa dhaifu kutokana na njaa,kumbuka sikuwa nimetia chochote tumboni tokea siku iliyokuwa imepita mchana wa saa nane nikiwa kule Kyaka niliponunua ndizi (gonja) nikala mbili pamoja na soda. Ila nilipokuwa nakumbuka niliyoyashuhudia usiku nguvu zilinijia na nilikuwa naongeza mwendo ili nipambane walau nifikie Kijiji chochote niwe salama. Mbele kidogo nikaanza kuziona nyayo za ngombe, nilifurahi sana, sana... nikaanza kutembelea alama za kwato za ng'ombe nikajiambia sasa hapa ni mimi na kwato mpaka nifike huko ng'ombe walipoelekea.
Ndugu msomaji nilitembea sana hadi nikaanza kuhisi kiu ya maji, nikawa nimechoka kabisa ikabidi nivumilie niendelee. Nilifika sehemu nikakuta dimbwi la maji machafu, nikasimama nikavua pull-over kisha nikaitoa na t-shirt nikapiga magoti pale mbele ya dimbwi nikainama nikatandika ile t-shirt juu ya maji nikaweka kinywa juu ya t-shirt nikajaribu kunyonya maji nikaona imekuwa usumbufu pia napoteza muda. Moja kwa moja niliamua kuuloweka mdomo juu ya maji nikapiga mafundo kadhaa Kisha nikainuka nikavaa t-shirt yangu kisha pullover nikaifunga kiunoni nikaendelea na mwendo.
Hatua chache kutoka pale nikaanza kuhisi njaa zaidi baada ya kunywa yale maji nikasikia tumbo linawaka moto hapo ndiyo nikawa nimeichokoza njaa kabisa. Muda ulikuwa umeenda kwa expérience niliyokuwa nimeipata kwa muda mfupi pale porini nilikisia kuwa ilikuwa kwenye saa 12 :30 za jioni. Nikitizama mbele nyuma, kushoto kulia naona nyasi,miti na vichaka. Nikitizama juu angani nikawa nashuhudia makundi ya ndege na eneo lile zilisikika sauti kutoka vinywani mwa ndege hao......
"Wawawa.....wawawa...........wawawa....."!!
Hali ile ikanifanya niamini kuwa kweli sijakosea muda ilikuwa ni jioni na wakati huo giza lingepiga hodi muda wowote.
Nikijitahidi sana kukata mbuga nyayo za ng'ombe zilinisaidia, wakati huo sikuwa nikijisikia vizuri tumboni yale maji yalikuwa yameniletea njaa kali sikuwa na nguvu zaidi nilikuwa nakata mbuga na vichaka kwa mwendo wa kujilazimisha. Niliendelea kusonga mbele nikawa nahisi kuchoka miguu inawaka moto viatu vikawa ninanichoma visiginoni na vidoleni Kati Kati ya nyayo ile hela nimeficha huko ikawa naya inanikwaruza inaniumiza nyayo nikatamani nivue viatu nivitupe maana hata vilianza kunielemea.
Ilibidi nisimame,nivitoe viatu, nikavua soksi harakaharaka nikaitoa ile Ada ya shule pamoja na hela ya matumizi nikaviweka chini kisha nikafungua ile pullover niliyokuwa nimeifunga kiunoni nikafungua mkanda wa suruali kisha zip,nikaishusha suruali usawa wa mapaja nikanyanyua t-shirt juu kisha nikachukua ile pesa kibunda chote nikakipenyeza kwenye kimfuko cha mbele cha chupi niliokuwa nimeivaa, nikaona mbele kumetuna sana, sikujali nikavuta suruali juu nikafuga mkanda, nikavaa soksi zangu, viatu nikaviunganisha kamba kisha nikavitupa begani nikaendelea na safari nikiwa nimevaa soksi tupu.
Giza lilishaingia sikuona tumaini wala dalili zozote za kukifikia Kijiji machozi ya uchungu yalianza kunitoka, nilihisi kufakufa nguvu zikaniishia, mashavu yakawa yanalowa machozi nikafuta nikachoka mpaka nikaachana nayo, nikayaacha yaendelee kumwagika tu. Hasira zikanijaa nikaanza kuilaani elimu, nikafikiria ndiyo imenifikisha hapo. Muda huo nilishaachana na nyayo kwakuwa sikuwa nikiziona tena sababu giza lilishatanda.
Niliendelea kupuyanga kwasababu nilishapaniki, roho ya utu ilianza kunitoka nikaanza kuchanganikiwa, nikawa kama komandoo yosso, leo hii ndio( panyaroad)unyama ukanijaa wakati huo, nikajiambia moyoni "I will never die easy.....I 'll die standing" Niliendelea kusogea giza likaanza kunizidi nguvu ya lenzi ya macho yangu nikajisemea...." Derick tafuta mti panda ulale. Nilitafuta mti mmoja mrefu eneo lile maana sikutaka kuwa chini ili wale wachawi wakija nisiwaone kabisa wakicheza kunizunguka kama ilivyokuwa siku iliyopita.
Tokea giza lilipoanza nakumbuka nilikaa sana juu ya mti sikufumba jicho kabisa, sikuwa nikisikia njaa tena wala usingizi bali uoga ndio ulikuwa umenizidi. Nilishalia saana mpaka machozi yakakauka kabisa,giza totoro, nilichoshangaa hapakuwa na mbu kabisa. nikiwa nimekaa akili imesiz nilianza kuona vimulimuli vya moto vinawaka na kuzima angani. Nywele na mwili wote vikaanza kusisimka nikajua leo lazima wanile hawa. Sikuwa na jinsi wala namna yeyote zaidi ya kuwasubiri.
Ndugu zangu wasomaji wachawi wapo, asikwambie mtu kufumba na kufumbua nilishuhudia upepo wa gafla ukatikisa mti nikasikia na tawi kutoka kwenye mti uliopo linakatika kkhaa... nikawa natetema tu. Sikuwa nikiona chochote sababu ya giza mle msituni nikiwa niko kwenye bumbuazi kubwa nilishtushwa nimemwagiwa maji usoni kisha gafla nikageuka pembeni nikaona kitu kama kifurushi juu ya mti kimekunjwa kwenye tambala nililoliona ni jeupe, nikahisi sasa ndio naliwa, wamekuja kunichukua.....
Itaendelea.
Muendelezo soma
Sitasahau nilivyonusurika kuchukuliwa mateka na majambazi mkoani Kagera