Sitasahau nilivyonusurika kuchukuliwa mateka na majambazi mkoani Kagera

Sitasahau nilivyonusurika kuchukuliwa mateka na majambazi mkoani Kagera

Ilipoishia.......

.....nikahisi sasa ndiyo naliwa, wamekuja kunichukua........

Inaendelea.........

Wakati huo nikaanza kuhisi kupoteza kumbukumbu, nikawa kama vile niko juu juu tu ninaelea hewani mti na matawi yake sivioni, ufahamu halisia sikuwa nao nilikuwa kwenye lindi la mauzauza.

Ilikuwa ni asubuhi tena, kijua kimechomoza na ndio nililiona jua siku hiyo kwa usahihi, nilijikuta niko nimelala chini ya mti, ule ule niliyokuwa juu yake usiku wa siku iliyopita, nikiwa nimekaa nikawa najiuliza maswali, hivi nimefikaje pale chini, nilishuka mwenyewe kweli? nikijitahidi kuvuta kumbukumbu sikung'amua kitu.

Nilijikusanya pale nikakaa kitako, nikajikagua kama ile fedha ipo nikajigusa nikasikia ipo imetuna. Nikainuka ili nijisikilizie hali yangu ikoje, nitambue viungo viko salama au nilianguka kutoka juu ya mti. Ukweli ni kwamba sikuwa na tatizo lolote la viungo nilikuwa niko sawa.

Muda wa dk chache nilizosimama kujikagua, nilihisi kizunguzungu ikabidi nikae chini tena. Wakati huo nilikuwa napanga mipango ya kuanza safari huku nikiwaza jua nilipige kisogo nielekee upande wa pili maana huko ndiko Karagwe iliko yaani Kaskazini Magharibi.

Nilibaki pale chini takribani saa nzima maana kila nilipokuwa najaribu kuinuka nilikuwa nahisi kuanguka. Sikuwa na namna mbadala ilikuwa lazima niondoke. Ukizingatia nilijua fika kwamba hata nikibaki pale haitasaidia zaidi nitakufa njaa. Nilijikaza nikaanza kuondoka.

Nakumbuka sikuwa nimekwenda mbali sana kutoka sehemu nilikotoka, maana miguu ilinilegea nguvu zikanishia kabisa, sikuwa na ziada ya kusonga mbele tena maana hata kijua kilizidi kunilevya zaidi. Nilijisogeza chini ya kivuli cha mti nikalala pale.

Mawazo yalinitawala sana, nikawa nawaza, nimenusurika kwa risasi za yale mabandidu sasa ona nakufa katikati ya pori kwa njaa. Nikiwa nimelala kisogo chini uso juu machozi yalikuwa yakinitiririka pale. Nikawa nikiwaza lolote litakalonipata sawa!

Nikiwa nimejilaza pale chini, matumaini nimekwisha yazika, Mara nilianza kuhisi kama kuna kitu kinakuja,nikiwa pale nikainua kichwa kutoka chini ili nitege sikio vizuri, kweli kuna kitu kilikuwa kinakuja kwenye nyasi, nikakurupuka gafla.Kile kishindo cha mkurupuko kikamshtua pia yule mnyama, kumbe alikuwa mbwa.

Yule mbwa akaanza nibwekea kwa sauti ya chin, Yani Kama anaunguruma hivi, muda mfupi nakawaona watu wakikatiza mwitu huku wakipiga miruzi kadhaa kumuita yule yule mbwa. Nilinyanyuka taratibu nikawatazama vizuri kwa jicho la udadisi nikaona ni wanaume watatu wawili wameweka madumu ya rangi ya njano begani mmoja hana kitu Ila wote wameshikilia fimbo mikononi mwao.

Sikutaka kupoteza muda nilipiga kelele kuwasimamisha walinisikia kisha wakasimama, nilianza kutoka pale kwa nguvu ya ajabu. Walibaki kupigwa butwaa mmoja asiye na dumu alikuwa ameiweka fimbo yake ikikatiza mabega yote mawili usawa wa mgongo huku mikono yake miwili imeshika kila upande wa ncha ya hiyo fimbo. Aliishusha ile fimbo akaiweka sawa. Wale wawili walishashusha madumu yao chini wakiendelea kunitizama kwa udadisi huku nikiwa nawakaribia. Niligundua walikuwa wafugaji.

"Shikamoo.. " niliwasalimia, hakuna aliyenijibu, mmoja niliona alichakatachakata mdomo akageuza shingo pembeni akatema mate chini....ptuuu. Wakaongea kilugha, kisha wakanicheka kwa dharau hivi. Ndani yangu nikasikia moyo unasema hakuna msaada hapa, gafla nikapigwa swali
"Onakwenda wapi'
kwa unyeyekevu mkubwa nikawambia mkasa wote ulivyokuwa.

Baada ya kuwapa ule mkasa walitizamana, wakaongea kilugha wakaonekana kwa macho like matukio hayo wanayafahamu hayakuwa mageni kwao( kwa jinsi nilivyowasoma mimi)na hapo walionesha kunielewa. Muda huo niliwaomba wanisaidie maziwa niywe maana niligundua madumu yao yalikuwa na maziwa. Jamaa alianza kutikisa dumu Kisha akachukua kikombe cha bati akanimiminia maziwa. Daah! yalikuwa maziwa ya viwango I see. Nilipiga vikombe viwili mfurulizo Kama maji kisha nikawekewa cha tatu iko nkakipiga kawaida.

Tumbo lilikuwa limejaa Sana wakati huo nikashiba barabara, nikawa na nguvu mpya. Ingawa lilianza kuuma Sana Ila sikujali. Wenyeji wangu wakaniambia wanakwenda kwenye Kijiji kimoja sikumbuki jina lake Ila pia wanapitia kwa jamaa yule (hasiye na dumu) kwenye boma yake kisha wao wananyoosha kwenda kwenye Kijiji husika kwenda kuuza maziwa yao.

Niliwaomba msaada wa kujua barabara kuu iendayo Karagwe wakaniambia iko mbali sana na eneo lile. Wakanambia kuliko kwenda kutafuta barabara tena peke yako acha twende pamoja mpk kwa yule jamaa yao kisha nilale pale kwake ili yeye anipeleke hiyo kesho kijiji nitakayopata usafiri ili niende Kayanga makao makuu ya Wilaya wakati huo sijui sasa.

Baada ya kutembeza masaa Kama matatu hivi tulifika, kulikuwa Kuna vijumba vya nyasi kadhaa pia na watu wengiwengi hususani vijana na watoto. Nilikuwa nimechoka sana, kila mmoja ananishangaa. Nikapelekwa kwenye kijumba kimoja wapo nikatambulishwa kwa mke wa yule jamaa na wamama wengine, kisha nikaitiwa kijana mmoja anioneshe wapi pa kupumzika.

Nilishtushwa na mguso wa mikono ya mtu akinipapasa miguu,nikakutana na giza, kumbe ilishakuwa usiku. Niliamshwa kwa ajili ya kupata chakula cha jioni. Tulikula Kisha wakati wa kulala tulilala tumerundikana kama saba kwenye kale kajumba ka nyasi. Wale watu wanalala vibaya i see, mara ukistuka mguu wa mtu uko kichwani kwako , pia vijana wanajamba mno, ukichanganya harufu ya mafuta ya samli wanayojipaka mwilini kuoga hawaogi duh! yaani ni tafrani tupu. Hayo yote kwangu mimi nililiona sio kero hata kidogo na kama mmoja wapo angeamka na kujisaidia kabisa kwenye zile ngozi tulilalia, mi nisingeiona shaka. Kikubwa nilijiona niko salama. Sikuwa nikichungulia kuzimu kama ilivyokuwa siku mbili zilizokuwa zimepita.

Mvua iliyoanza usiku ilikuwa bado inanyesha hata kulipokuwa kumekucha. Ile Kaya haikuwa ikijali hayo mambo ya mvua walishaamka wote. Moyoni nikawa nawaza sasa hii mvua tutaondoka kweli? Lakini jinsi muda ulivyokuwa unakwenda ikawa inapungua na ilifika mida ya saa nne ilikuwa imekata kabisa. Nakumbuka siku hiyo Nilipiga Lita na nusu ya maziwa fresh hata hayakuwa yamechemshwa, Ila yalikuwa ya motomoto,nikajisikia niko vizuri kuianza safari.

Kwa ule ukarimu waliyonionesha nilitamani nichomoe shilingi elfu moja niwapatie lakini nikawa na hofu kuwa naweza leta kiherehere, wakajua kumbe nna pesa wakanicharaza fimbo nikanyang'anywa pesa yangu yote. Huo mpango nikaucancel. Mida ilikuwa inasogea yule jamaa ninayeenda naye alikuwa tayari amefunga kifurushi cha wastani akakifunga mgomgoni akakaza fundo kwa bega akachukua fimbo yake tukaanza safari (Alikuwa amebeba mafuta ya samli).

Baada ya mwendo wa masaa kama matatu tunakatiza porini tulianza kuona nyumba moja moja na jinsi tulivyozidi kusogea tulianza kupita maeneo yenye makazi na ndo hapo nikaambia hapa ni uzuri wa kondoo jina lilinifanya nitabasamu bila kuhoji kwanini paliitwa hivyo.

Mwisho wa siku tulifika kwenye kaji-center, kalionekana kuchangamka kuliko huko tulikopita sikumbuki paliitwaje pale lakini ni viunga hivyohivyo vya maeneo ya uzuri wa kondoo, tuliingia ndanindani kidogo Kisha mwezangu akaniacha hapo akaniambia hapo nitapata gari kiurahisi na wakati huo ilikuwa ni saa kumi na moja za jioni. Kabla hatujaagana nilitoa hela nikampatia Kama shukrani akashangaa sana.

Niliwaza kwa muda ule siwezi Pata gari na nilikuwa nalinga sana nilijua nyumba zote zile nitalala kwa yeyote tu ili kesho yake nianze safari ya kuelekea shule. Wakati nikiwaza niende wapi nilijisogeza kwa watu waliokuwa wamesimama maeneo yale kisha nikawauliza wapi Kuna kanisa eneo hilo. Halikuwa swali gumu kwao maana walinielekeza tu kwamba kamata kibarabara hiki nenda bila kupinda kokote utakuwa utaliona kanisa mbele yako.

Ko..nko..nko... nilikuwa nagonga mlango nyumbani kwa Mchungaji wa lile kanisa la KKKT. Baba mmoja wa umri wa Kati ya miaka 45-50 ndiye aliyenifungulia mlango.

Inaendelea.......
SEHEMU INAYOFUATA NDIYO ITATUFUNGIA KISA HIKI AMBACHO KIMENIACHIA KUMBUKUMBU ISIYOFUTIKA.

Sehemu ya mwisho ya stori soma Sitasahau nilivyonusurika kuchukuliwa mateka na majambazi mkoani Kagera
 
Ni mbele ya uzuri wa kondoo, kiliwekwa mpaka kituo cha askari wa kusindikiza magari kuna kona flani hivi ya mchongo,

Ngoma nzito ni kimisi huko ndo pabaya hata sasa bado panaogopesha kiaina
😅😅 miaka ya 2002 nilikuwa naenda karagwe kama msimuliaji anavyosimulia ndio ilikuwa route yangu ya kwanza mkoa wa kagera nikitokea mwanza nimefika na meli bukoba fasta nikawahi zile hiace kiherehere nikawahi siti ya mbele nikawa nashangaa wenyeji wanaikwepa wanakimbilia huko nyuma😅😅 dereva akapiga gia kufika uzuri wa kondoo askari akaingia siti ya mbele siti ya mbele afu kavaa kiraia na bunduki imefungwa mapira kibao mi nikasogea karibu na gia sasa tumefika maeneo ambayo wanateka dereva anamuuliza afande " hivi jana wametekea hapa au pale juu afande anajibu ni pale juu babu afu eskota akamrushia abiria bunduki aliyekuwa jirani yake kama hivi huyu dogo aliyekaa hapa" ebwana ee kusikia hii kauli nikawa naicheki ile bunduki jasho la kwapa linatoka nikawaza huyu mjinga ikitokea noma saivi anaweza kunirushia hii bunduki daah ndio nikajua kwa nn kule stand abiria hawakutaka siti ya mbele..
Usiombe siku hiyo nilipiga Sara zote maana gari zima tulikuwa kimya kila mtu akiokoka moyoni😅😅
 
Ila naomba Léo niishie hapo maana
Pole mkuu story inasikitisha na kufurahisha kwa wakati mmoja,hilo pori la kitengule ?maana nimeona uzuri wa kondoo hapo

Sent from my HUAWEI MLA-AL10 using JamiiForums mobile app

Kwakweli ni miaka mingi sn tokea nilipokutana n'a kadhia hii. Ujue inafika miaka 28 ama 29 Ni zamani kidogo na ndiyo maana siwezi elewa mpaka Kati ya pori la kitengule na lile eneo ambalo tulitekewa ambalo mbele ndio Uzuri wa kondoo
 
😅😅 miaka ya 2002 nilikuwa naenda karagwe kama msimuliaji anavyosimulia ndio ilikuwa route yangu ya kwanza mkoa wa kagera nikitokea mwanza nimefika na meli bukoba fasta nikawahi zile hiace kiherehere nikawahi siti ya mbele nikawa nashangaa wenyeji wanaikwepa wanakimbilia huko nyuma😅😅 dereva akapiga gia kufika uzuri wa kondoo askari akaingia siti ya mbele siti ya mbele afu kavaa kiraia na bunduki imefungwa mapira kibao mi nikasogea karibu na gia sasa tumefika maeneo ambayo wanateka dereva anamuuliza afande " hivi jana wametekea hapa au pale juu afande anajibu ni pale juu babu afu eskota akamrushia abiria bunduki aliyekuwa jirani yake kama hivi huyu dogo aliyekaa hapa" ebwana ee kusikia hii kauli nikawa naicheki ile bunduki jasho la kwapa linatoka nikawaza huyu mjinga ikitokea noma saivi anaweza kunirushia hii bunduki daah ndio nikajua kwa nn kule stand abiria hawakutaka siti ya mbele..
Usiombe siku hiyo nilipiga Sara zote maana gari zima tulikuwa kimya kila mtu akiokoka moyoni😅😅
Maisha yalikuwa magumu mno acha tu kwa sasa karagwe bk ni kugusa tu 24/7 gari zinatembea,, mziki umebaki kasindaga, kimisi na nyakahura na ulipunguzwa nguvu alivyoingia Magufuli, saiv wameruhusu kupita hata usiku mkubwa ila mie bado sina imani napo matukio yalikuwa mengi mno japokuwa namshukuru Mungu sikuwahi kupitia hayo madhira
 
Karibu unaleta story ambayo huna hata neno moja la lugha ya wajomba zangu hujui kihaya, hujui kinyambo, hujui kiangaza, hujui kinyarwanda, hujui Kirundi, story haiishi inakata atimu
Hapa tatizo linakuja pale ambapo kila mtu anataka uandike anavyotaka yeye. Mimi nimeandika kwa maslahi ya wanajamii wote ili kushare niliwahi kuexperience nini huko nyuma. Ule wakati ambao Visa vya utekaji vilikuwa vimekithiri hapa nchini, ili hata wewe ambaye hukuwa umezaliwa ujue nchi hii tumetoka mbali.
 
Hapa tatizo linakuja pale ambapo kila mtu anataka uandike anavyotaka yeye. Mimi nimeandika kwa maslahi ya wanajamii wote ili kushare niliwahi kuexperience nini huko nyuma. Ule wakati ambao Visa vya utekaji vilikuwa vimekithiri hapa nchini, ili hata wewe ambaye hukuwa umezaliwa ujue nchi hii tumetoka mbali.
Kelele za chura zipuuze usitolewe kwenye reli mkuu
 
Back
Top Bottom