Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mama anaupiga mwingiHabari,
Niende kwenye mada, kama kichwa cha habari hapo juu, Ninaweza kusema kwamba waliotunga sheria mbalimbali za utumishi wa umma watakuwa wajinga na walikuwa na njia njema kabisa.
Miongoni mwa Vitu muhimu kabisa ni nyongeza ya mishahara, increments na kupanda madaraja kila baada ya miaka kadhaa ili kuendana na kupenda kwa gharama za maisha kila mwaka.HIVYO mtumishi aliweza kuyamudu maisha yake japo kwa kudanadana.
Utawala wa JPM yeye hakuona umuhimu wa jambo hili na kuwasugua watumishi kwa miaka sita bila kuwapatia hiyo haki yao ya msingi, aliwafanya watumishi wengi kushindwa kuendana na gharama za maisha na kuwa na hali mbaya sana kiuchumi.
Hivyo kitendo hichi kilififisha ufikiwaji na upelekaji wa maendeleo kiurahisi kwa wananchi japo wananchi wajinga walikuwa wa kwanza kupiga makofi wakifurahia hayo Mateso ya watumishi wa serikali yao.
Watumishi walifanya kazi quantity na si quality kama maroboti, ufanisi ulishuka sana na nidhamu ya uoga kuwa asilimia 100, nia na hamu ya kufanya kazi za serikali ilipungua kabisa na hata maendeleo yaliyoyowafikia wananchi yalikuwa hafifu japo yalikuwa jina kubwa sana na wale waimba mapambio kama mtakumbuka.
Watumishi wa serikali ni DARAJA la kupitisha maendeleo kutoka kwa serikali kwenda kwa wananchi wakiwa na hali mbaya kiuchumi, kiafya na kijamii basi hata maendeleo tarajiwa yatawafikia wananchi kwa namna hali yao ilivyo na wakiheshimiwa, kupewa stahiki zao kwa wakati basi hata utoaji wa huduma na maendeleo kwa jamii huongezeka maradufu.
Binafsi ninamuona MAMA samia kufanikisha zaidi katika mambo yake hata kwa kulijali hili kundi muhimu katika jamii, na 23% imewaongezea watumishi nguvu sana kabla hata ya kuipata, tunakuomba MAMA samia watumishi utushike mkono na sisi hatutakuangusha kuyatafsiri mawazo yako ya kimaendeleo kuwa uhalisia kwa wananchi wetu tunaowahudumia.
Mungu ibaraki Tanzania, Mungu ibaraki ccm na raisi wetu MAMA SAMIA
Ungesema tu ule uwanja ulikuuma haya mengine yote ni ngojera.
ww unalalamika kutokupandishwa mshahara, kuna watu private sector walipunguziwa mishahara 25-40% for 1yr during covid na wengine walipoteza kazi kabisa ww unalia lia kutoongezewa salary while uliendelea kupata mshahara na you kept your job during covid.
Kweli shukrani ya punda ni mateke.
Wewe uliyekuwa na ajira unasema usikumbushwe machungu na je ambao hawakuwa na ajira je?ukikaa kutegemea mshaara utakuwa na ulemavu wa akili siku zote mshaara haujawahi kutosha...Sio kweli. Wewe sio mfanyakazi ndio maana huoni tofauti, kaa kimya usiwakumbushe watu machungu.
Acha uzwazwa dogo!We pimbi, kwani pamoja na Magufuli kutoongeza mishahara inflation haikutokea? kwani wakati anaingia madarakani alikuta sukari inauzwa sh.ngapi na akiwa madarakani ikawa inauzwa sh.ngapi? aliyependekeza kodi ya nyumba kupitia luku hakuwa Jiwe? Shenzy type.
Unamtetea Magufuli mpaka yeye mwenyewe anashngaa huko aliko. Eti Magufuli na Samia hawana tofàuti!! Kweli?Japo Magufuli hakuongeza mishahara lakini pia hapakuwepo na huu mfumuko wa bei uliopo sasa, kwa kifupi Magufuli na Samia hawana tofauti kwenye hili la kuinua hali ya wafanyakazi.
Magufuli alianzisha mega projects 3 kwa wakati mmoja; SGR, Stiglers Gorge na Dodoma City. Mbali ya projects zingine kama Busisi, hospitals na barabara. Na mpaka anakufa yeye mwenyewe alishindwa kumaliza sababu ya kukosa uwezo wa ku PLANKaongezewa laki mbili anaporwa laki nne bado anachekelea tu, hakuna mradi wowote wa kimkakati kama taifa unaoendelezwa, Mradi mkuu umekua mradi wa Kusafiri
Jiendeleze. Utakuja kunishukuru Sikh moja😂😂😂😂we si tayari ulishatumbuliwa
Mshahara umepanda ila tatizo ni mfumuko wa bei.Enzi za Magufuli nilikuwa napokea mshahara 300,000 ilitosha kununua 240Kg za mchele ,mshahara umeongezeka napokea 369,900 inatosha kununua 185Kg za mchele,nisaidieni hesabu hesabu hapo mshahara umepanda au umeshuka?
Kuwa kiongozi wa malaika Lucifer ofisi yake ipo palepale kuzimu mjiniHivi ni kazi gani aliomba kwenda kufanya kule kuzimu😂😂😂
Magufuli angekuwa Raisi miaka 20 watumishi wa serikali akili zingewakaa sawa na wananchi pia tungeanza kuwa na akili za kujitengemea bila kuwaza Ajira za serikali ambazo zinafanya tuendelee kuwa masikini uku wageni wakijiajiri sisi watanzania akili zetu zikiitaji kazi za ualimu na Upolisi na kwenda jkt kupoteza muda basi.Tulitaka kuwa na raisi Magufuli kwa miaka kama 20 hivi inchi iendelee
USSR
sawa mke wa shetani😁😁😁Maweee!! nani ampe?? yule ni kuruta kule anaponda kokoto kila uchao!! na kutumwa barabarani ili kusababisha ajali!!...anatamani arudi atubu lkn wapi!!!....... ..imekwisha pitishwa........
Anatamani angekuwa anaongoza km Rais wetu mpya Mama Samia...lkn ndo basi tena!!.......amemnunia shetani kule kuzimu eti alimdanganya!! na shetani kwa kumkomoa huyo Jiwe, ameamua kumpa kazi ngumu!
Wewe ni mzalendo wa kweli, mawazo yako yanawakilisha Watanzania wengi! Hao wanaoshinda hapa kumkashifu Magufuli wengi wao hata kazini kwao ni wavivu na Mizigo kwa mwajiri.Mkuu bado upo kwenye ajira? Labda tuanzie hapo kwanza, and Jee increment ulopewa imeleta impact kiasi gani kwenue maisha yako.
Mkuu wewe ni mbinafsi sana voz unasngalia upandishiwe mshahara wako ila kumbuka asilomia kibwa ya watanzania ni maskini wasio na kazi hao nao maisha yao wanasaidiwa na nani.
Utawala wa mwendazake ulijikita katika kuweka mazingira mazuri kwanza kwa kila mtanzania aweze kujiingizia kipato chake kirahisi lakibi atimize pia wajibu wake kulipa kodi.
Mtazamo wa mwenda zake ulikuwa ndo mtazamo walioanza nao china, angalia china walipo sasa. China walifsnya kazi kwa nguvu na hadi kufikia masaa zaidi ya 10 na wengi walifia kwenye mashine sababu ya kuchoka
Leo dunia nzima inafurahia kila aina ya bidhaa kutoka china sababu walijengewa utamaduni wa kufanya kazi bila kuchoka.
Ndugu yangu mm nimeanza kazi enzi ya kikwete nlikuwa kijana mdogo tu 20+ na sasa nimekuwa mbaba . Hakuna kipindi nlifanya kazi kwa bidii na kwa umahiri wangu wote na kwa uzalendo kama kipindi cha JPM sababu alikuja na mtazamo niliokuwa naota kabla hajawa rais. Kwangu mimi magufuli atakuwa rais wa maisha yangu yote sababu bado naishi kwenye ndoto zake hadi sasa. Na nitaendelea kuwa hivo mpaka nife.