Sitasahau tanuru la moto nililopitishwa na Hayati Magufuli mimi kama mtumishi wa Serikali

Kumbe sukuma gang ni wengi kiasi hiki?

Maana huku mtaani ni balaa! Muulize hata mumeo atakwambia Magu ni chuma,

Basi nae kumbe ni sukuma gang
Umeanza upuuzi sasa
 
Ma
Mama anaupiga mwingi
 
An old ways of thinking by Mwenzake Chawa
 
Sio kweli. Wewe sio mfanyakazi ndio maana huoni tofauti, kaa kimya usiwakumbushe watu machungu.
Wewe uliyekuwa na ajira unasema usikumbushwe machungu na je ambao hawakuwa na ajira je?ukikaa kutegemea mshaara utakuwa na ulemavu wa akili siku zote mshaara haujawahi kutosha...
Walimu mnatuchosha sana
 
Acha uzwazwa dogo!

Sukari alikuta inauzwa 1800 ikapanda hadi 2800..


Haya twambie nini kingine kilipanda maradufu?

Bajeti ya kodi ya nyumba imeanza kipindi cha Mwigulu mteule wa Samia huyo hakuwa Magu acha utahira.
 
Japo Magufuli hakuongeza mishahara lakini pia hapakuwepo na huu mfumuko wa bei uliopo sasa, kwa kifupi Magufuli na Samia hawana tofauti kwenye hili la kuinua hali ya wafanyakazi.
Unamtetea Magufuli mpaka yeye mwenyewe anashngaa huko aliko. Eti Magufuli na Samia hawana tofàuti!! Kweli?

Unamdanganya nani kuwa bidhaa hazikupanda bei kipindi chake? Sukari ilikuwa Tsh 1,800 wakati anaingia mwaka 2015 akaivuruga hadi Tsh 3,000- 5,000 na mpaka anakufa haijawahi kurudi pale pa awali.
 
Mleta mada anawaza tumbo tu.

Hujali kabisa namna tunavyopigwa mnada kwa kasi ya umeme.

Yaani wewe ukipata uhakika wa kula hata ukiuzwa hutajali.
 
Kaongezewa laki mbili anaporwa laki nne bado anachekelea tu, hakuna mradi wowote wa kimkakati kama taifa unaoendelezwa, Mradi mkuu umekua mradi wa Kusafiri
Magufuli alianzisha mega projects 3 kwa wakati mmoja; SGR, Stiglers Gorge na Dodoma City. Mbali ya projects zingine kama Busisi, hospitals na barabara. Na mpaka anakufa yeye mwenyewe alishindwa kumaliza sababu ya kukosa uwezo wa ku PLAN

Hizo projects zinahitaji fedha za kujengea na zingine tumeanza kulipa riba wakati hatujaanza kuzalisha. Mama Samia amefanya restructuring tu ili maisha mengine yaendelee Wakati miradi inajengwa
 
Ukiwakuta maofisi wanavyozurura, wasivyofanya kazi kwa uadilifu na wanavyokusubirisha; ila wanavyolalamikia nyongeza sasa.
 
Enzi za Magufuli nilikuwa napokea mshahara 300,000 ilitosha kununua 240Kg za mchele ,mshahara umeongezeka napokea 369,900 inatosha kununua 185Kg za mchele,nisaidieni hesabu hesabu hapo mshahara umepanda au umeshuka?
Mshahara umepanda ila tatizo ni mfumuko wa bei.
 
Mwacheni Magu aitwe Magufuli na Mama Samia aitwe Samia kila Zama na kitabu chakeMagufuli alitenda kwa kiwango chake na alitufumbua macho watanzania wengi anastahili sifa zake na mama anaandika chake tumpe muda
 
Tulitaka kuwa na raisi Magufuli kwa miaka kama 20 hivi inchi iendelee

USSR
Magufuli angekuwa Raisi miaka 20 watumishi wa serikali akili zingewakaa sawa na wananchi pia tungeanza kuwa na akili za kujitengemea bila kuwaza Ajira za serikali ambazo zinafanya tuendelee kuwa masikini uku wageni wakijiajiri sisi watanzania akili zetu zikiitaji kazi za ualimu na Upolisi na kwenda jkt kupoteza muda basi.
 
watu aina ya mletamada ni hasara kubwa kwa taifa.
 
sawa mke wa shetani😁😁😁

hizi ndio info anakupa akiwa faragha nawewe.
 
Wewe ni mzalendo wa kweli, mawazo yako yanawakilisha Watanzania wengi! Hao wanaoshinda hapa kumkashifu Magufuli wengi wao hata kazini kwao ni wavivu na Mizigo kwa mwajiri.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…