Binadamu hua tuna akili za ajabu sana hatuna tofauti na wanyama.
Simba dume anapovamia kambi ya simba mwingine na kumshinda, hua anaua watoto wote wa yule simba na kuanzisha uzao wake.
Cha ajabu binadamu na sisi eti mfano ukikuta mwanamke/mwanaume ana mtoto aliezaa kabla hajakutana na wewe, na wewe eti unaanza kumchukia mtoto!! Hizo ni akili za wapi?
Binadamu yupo tayari kulea watoto wa ndugu, majirani, hata ku adopt watoto wa mtaani lakini hayuko tayari kulea mtoto wa mume/mke wake!
Sijui kama nipo ndani ya mada.