Sitooa abadan asilan

Sitooa abadan asilan

Kwanza kuilinganisha Runzewe Shinyanga na mambo yasiyokuwa na akili haikubaliki. Runzewe ni sehemu nzuri sana, tengua kauli.

Pili, kama wewe hujawahi kuona tajiri asiye na mke basi hujatembea, au labda macho yako yana makengeza.
Sasa mpaka utembee sana ndio umuone?
 
Tuanzie mwisho turudi Mwanzo
1662144081333.jpg
 
Ndoa ina heshima kwa sababu tu ya mila za kiafrika ambazo zinabadilika kwa kasi sana, siku zijazo tutakuwa tu kama ulaya, mtu bachela ataruhusiwa kuwa raisi kama vile nchi za ulimwengu wa kwanza.

Ukizungumzia kazi au vyeo, mbona kuna watu hawana ndoa na wana kazi nzuri sana na vyeo vikubwa, na wanafanya vizuri makazini, nikupe mifano?
Japo huwa hawaaminiki haminiki hivi kwenye madaraka makubwa sana...
Hebu nipe mfano
 
Sasa mpaka utembee sana ndio umuone?
Sasa wewe Rasterman hujui kwamba mtu wa kwanza kuagiza gari aina ya Hammer kwenye nchi hii ni Zitto Kabwe, au hujui kwamba hana ndoa?

Huamini kwamba Sugu a.k.a Jongwe ni bilionea? Ana ndoa gani yule zaidi ya kula bata tu kwenye hotel yake kule Soko Matola?

Hata kama ni kweli hujawahi ona, hata masikio hayasikii?
 
Japo huwa hawaaminiki haminiki hivi kwenye madaraka makubwa sana...
Hebu nipe mfano
Kwa nini wasiaminike?

Anna Makinda aliliongoza bunge letu vizuri tu. Hana ndoa huyo mama.

Kuna mtangazaji bora kuwahi kutokea BBC kama Zuhura Yunus?
Hajaolewa na ameaminiwa na Ikulu ya nchi yetu hadi kupewa usemaji wa nchi, niongeze mifano?
 
Una uhakika hao wanawake wanafurahia kukosa watoto na waume? Au ni kwa vile tu hawakujaaliwa
 
Una uhakika hao wanawake wanafurahia kukosa watoto na waume? Au ni kwa vile tu hawakujaaliwa
Hilo la kufurahia ama kutofurahia ni jambo jingine, Hata wenye waume ni wengi tu hawafurahii kuwa kwenye hizo ndoa, ni kwa vile tu wameshindwa namna ya kujiondoa.

Nilikuwa najibu hoja kwamba bila ndoa unaweza ukakosa kazi au cheo na ukikipata hauaminiki, hoja ililetwa mezani na mkuu Kalpana .
 
Usiogope kuoa kwa kusikiliza matatizo ya ndoa za rafiki zako, huenda ukayapata kwa hao unaoruka nao,
 
Ila sikuhizi ukipata shida ndoani mwenza badala ya kukupa kampani apite nawe shidani na Faraja tele yeye ndo hukukimbia mazima.Sijui ndo shetani kashatawala walimwengu? Daaa
Imenitokea hii japo tulikuwa hatujafunga ndoa
 
Endeleeni kuzalisha nje badae mje muwaponde humu single mothers wa watu...kuoa au kuolewa utabaki kuwa na heshima yake hata mje maelfu kusema ndoa sio jambo jema..kuna kazi zingine mtazikosa au vyeo mtavikosa kisa tuu huna ndoa ya kisheria.
Mfano cheo gani au kazi gani ulishasikia au mtu anaweza kosa kisa ana ndoa nineuliza naomba unij
 
Mfano cheo gani au kazi gani ulishasikia au mtu anaweza kosa kisa ana ndoa nineuliza naomba unij
Uraisi wa nchi..
Kuna vyeo nyeti vya usalama wa nchi huwezi kuwekwa bachelor...
Any way hizi sio sababu nguli za kufanya uoe au uolewe mwisho wa siku kila mtu afanye na aonavyo inampendeza...
 
Zamani ilikuwa mtu akiwa kwenye ndoa unaona enhee kweli jamaa anafaidi. Kuna vitu ulikuwa ili uvipate aidha kwa mwanamke au mwanaume lazima uingie kwenye ndoa.

Sikuhizi mambo yamekuwa vice versa.

Binafsi sijaona sababu ya kunifanya nioe. Rafiki zangu waliooa kila siku wananiambia matatizo wanayokumbana nayo. Leo hili kesho lile.

Haya basi usiseme sitaki kuoa kisa hizo shida lakini pia raha zao, raha wanazopata kwenye ndoa hata mimi nisiyeoa naweza kuzipata.

Sijui wanawake wamejirahisisha au ndo usasa? Naona vitu vimekuwa tofauti na zamani

Cha msingi ni kuwa na ela tu.

Ela ndo kila kitu ukiwa nazo utapata kila kitu anachopata mwanandoa tena bila karaha zake. Binafsi sijioni nikioa labda miaka inavyozidi kwenda nitabadili mtazamo wangu.

Ila kwa sasa BADO SANA.
Me mwemyewe kwasasa sina mpango wa kuoa kabisa labda mtazamo utakuja kubadilika lkn sidhani
 
Endeleeni kuzalisha nje badae mje muwaponde humu single mothers wa watu...kuoa au kuolewa utabaki kuwa na heshima yake hata mje maelfu kusema ndoa sio jambo jema..kuna kazi zingine mtazikosa au vyeo mtavikosa kisa tuu huna ndoa ya kisheria.
Nani kakwambia anataka kazi ?
 
Back
Top Bottom