Sitooa abadan asilan

Sitooa abadan asilan

Endeleeni kuzalisha nje badae mje muwaponde humu single mothers wa watu...kuoa au kuolewa utabaki kuwa na heshima yake hata mje maelfu kusema ndoa sio jambo jema..kuna kazi zingine mtazikosa au vyeo mtavikosa kisa tuu huna ndoa ya kisheria.
Watu wengi ikiwemo wewe apo sista hamsomi mada na kuitafakari mada kama hizi kwa undani. Vijana karibia wote unaowaona wanaanzisha hizi mada jua kwamba alikuwa kwenye mahusiano yawe 1 au zaidi tena kwalengo la kuoa. Ila katika mahusiano hayo purupushani zilitokea na in either circumstances alishuhudia mwanamke kutokuwajibika katika makosa au udhaifu autendao. Jua alijaribu kusulihisha ila mwanamke hakutaka awajibishwe ilihali yeye anawajibishwa. Na kuukoleza moto zaidi akasikia na maswaibu hayohayo kutoka kwa watu wake wakaribu. My sister, jua hapo mwanaume ataifunga project husika na kuiona kama shit maana ndani ya mahusiano hayo yote hakufaidika chochote, pesa zikapunguzwa na alijiaibisha. Just know, maamuzi ya kiume yakipita hivi kichwani kuyaoverride nivigumu sana tena sana.
 
Zamani ilikuwa mtu akiwa kwenye ndoa unaona enhee kweli jamaa anafaidi. Kuna vitu ulikuwa ili uvipate aidha kwa mwanamke au mwanaume lazima uingie kwenye ndoa.

Sikuhizi mambo yamekuwa vice versa.

Binafsi sijaona sababu ya kunifanya nioe. Rafiki zangu waliooa kila siku wananiambia matatizo wanayokumbana nayo. Leo hili kesho lile.

Haya basi usiseme sitaki kuoa kisa hizo shida lakini pia raha zao, raha wanazopata kwenye ndoa hata mimi nisiyeoa naweza kuzipata.

Sijui wanawake wamejirahisisha au ndo usasa? Naona vitu vimekuwa tofauti na zamani

Cha msingi ni kuwa na ela tu.

Ela ndo kila kitu ukiwa nazo utapata kila kitu anachopata mwanandoa tena bila karaha zake. Binafsi sijioni nikioa labda miaka inavyozidi kwenda nitabadili mtazamo wangu.

Ila kwa sasa BADO SANA.
Unafuga ng'ombe wa nini huku hitaji lako ni kikombe kimoja cha maziwa kwa siku
 
Vijana wa Sasa ni waoga wa maishaa hatarii ....!
Kijana kuogopa maisha sio kosa tena ni faida maana ndiko kunamfanya asiperform au kuundergo unnecessary costs na actions ambazo zitamuharibia maisha yake. Ideology ya wanawake ilipoanzishwa ya kuwa hamuhitaji mwanaume walifikiri it's an advantage kwao ila kiundani mwanaume akarevolt kwenye psychological nature ya fear kwa kumbeba au kuwa na mwanamke hata kama huwezi iona. Hiyo psychological fear imekuja ilikumkumbusha mwanamke alishamkataa kifikra kuwa yeye kwake haitajiki vivyo hivyo basi naenende kwa caution ili asijeumiza. It's just a psychological matter.
 
Ukiona mtu ana hamasisha kataeni ndoa basi kuna uwezekano mkubwa ni mwana chama wa upinde mambo ya rangi rangi mambo ya kupindishwa nyoro

Sent using Jamii Forums mobile app
Nahizi comment kwakipindi hiki zimekuwa nyingi sana hasa kutoka kwawanawake ingawa pia wanaume wapo waliozitaja. In every action ambayo mwanaume atakayoifanya ambayo itamtenga au kumuweka mwanamke mbali naye, wanawake na jamii kwa ujumla itamperssive kuwa ni shoga ili tu wamdharaulishe. Nikitu cha ajabu na cha kijinga sana, maana jamii haitataka hata siku moja mwanaume ajijenge mwenyewe na kujiondolee unnecessary expenses ambazo mwanamke humuingizia wanapokuwa kwenye mahusiani ila watampaisha na kumpromote mwanamke kumuundermine mwanaume. Mpaka hivi sasa hivi sijajua hii ideology au mentality inasababishwa nanini.
 
siku ukiwa kitandani huna uwezo hata wa kunyanyua mkono, umejinyea umejikojolea huku huna hata wa kukuangalia achana na ndugu zako ambao lazima utawaonea maaibu tu au watakuchoka mapema Sana ndo utajua umuhimu wa kuwa na mtu manayeweza kusaidiana katika hali kama hiyo. hatuoi Kwa sababu ya starehe bali mambo kama hayo na mengine machache Sana lakini.

halafu kama wewe sio risk takers usioe nakwambia usioe utapigika ufe.

ndoa tuachie sisi wenye roho ngumu na wanaume wa kweli kweli nyie wavulana endeleeni na umalaya ambao mshaona ni dili kumbe mnaangamia tu. Kuna vitu ni vya kufanya ujananai na vya uzeeni Sasa wewe jitie misimamo na woga uchwara uje uwe na madeni huko mambele yaani utafanya vya ujana uzeeni na vya uzeeni uvifanyie huko kaburini au popote pale na ukione cha mtema Kuni. haya maisha ni marufuku kuruka namba eleweni nyie watoto mbona wagumu hivyo?????????????

naongea kwa niaba ya tuliojitoa mhanga na kuoa pamoja na tufaida tuchache kiasi hicho KWENYE ndoa ila Bado tunakomaa TU.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
We jamaa yangu sikia hii kituuu.

OA AKIZINGUA ACHA (FANYA HII KITU MPAKA UTAKAPOZEEKA)

MIMI NILIONA UMUHIMU WAKATI NAFANYIWA OPERATION. AISEE MKE ALINISTIRI SANA.

UKIANZA KUUGUA UTAITAMBUA THAMANI YA NDOA
Ukiwa na hela utapata wakukutunza..nadhani ushauri mzuri ni awe na pesa tu atatunzwa vzr kabisa hadi siku anakufa.

#MaendeleoHayanaChama
 
Mungu alipomletea Adam mwanamke alifanya kosa? Wa kwako atachukuliwa na nani? Omba tu upate mke mwema.
 
Ukiwa na hela utapata wakaukutunza..nadhanj ushauri mzuri ni awe na pesa tu.

#MaendeleoHayanaChama
😂😂😂Huyu msukumu vip? Kuna mambo ya chumbani sio mambo ya kizungu kuchukuliwa ni shida zile kwenda kutunza vizee huku uarabu na ulaya.
 
Kwa upande mwingine ongezeko la vijana wengi ambao hawaoni umuhimu wa ndoa.

Ni tafsiri ya kuwa wengi ambao hawaoni umuhimu wa ndoa isipokuwa ngono na kupata watoto basi wameanza kupukutika, kutokana na uwezekano wa kupatikana hayo hati pasi na ndoa.

Lakini hii haina maana kuwa ndoa haina thamani yoyote, hasha bali waliostaarabika na wanafahamu umuhimu wa ndoa basi wanaendelea kuoa na wanauona umuhimu wa ndoa.

Na migogoro katika ndoa fulani sio kipimo cha ubaya wa taasisi ya ndoa kwa ujumla wake.
Cheti cha ndoa ni mfumo jike uliojificha kwenye jamii,Haki kwa mwanamke zinazozidi mwanamme ni mfumo jike uliorasmishwa Rasmi!!
 
siku ukiwa kitandani huna uwezo hata wa kunyanyua mkono, umejinyea umejikojolea huku huna hata wa kukuangalia achana na ndugu zako ambao lazima utawaonea maaibu tu au watakuchoka mapema Sana ndo utajua umuhimu wa kuwa na mtu manayeweza kusaidiana katika hali kama hiyo. hatuoi Kwa sababu ya starehe bali mambo kama hayo na mengine machache Sana lakini.

halafu kama wewe sio risk takers usioe nakwambia usioe utapigika ufe.

ndoa tuachie sisi wenye roho ngumu na wanaume wa kweli kweli nyie wavulana endeleeni na umalaya ambao mshaona ni dili kumbe mnaangamia tu. Kuna vitu ni vya kufanya ujananai na vya uzeeni Sasa wewe jitie misimamo na woga uchwara uje uwe na madeni huko mambele yaani utafanya vya ujana uzeeni na vya uzeeni uvifanyie huko kaburini au popote pale na ukione cha mtema Kuni. haya maisha ni marufuku kuruka namba eleweni nyie watoto mbona wagumu hivyo?????????????

naongea kwa niaba ya tuliojitoa mhanga na kuoa pamoja na tufaida tuchache kiasi hicho KWENYE ndoa ila Bado tunakomaa TU.

Sent using Jamii Forums mobile app
[emoji383] talks
 
Kuna muda mwandani wako anakusaidia vitu ambavyo hakuna mtu au ndugu yako yeyote wa damu anaweza kukusaidia.

Oeni vijana mpate baraka ambazo Mungu amezitayarisha kwaajili yenu.

Ndoa hufungua hufungua na kurahisisha vile ambavyo umekuwa ukivitafuta na kuvitamani siku zotenin
kweli kabisa.
 
Back
Top Bottom