Kijana Kuoa Ni Muhimu kuliko unavyofikiria.
Kama ww umetoka kwenye familia yenye Baba na Mama, na ukalelewa.
Kwann unataka watoto wako walelewe kiholela?..
Na Kama umetoka kwenye familia ya upande mmoja, najua umepitia changamoto nyingi. Unataka pia watoto wako wapitie Kama ww?..
Ukioa unakuwa na Maono ya kujenga na kutunza Familia.
Utaoa, utawajibika Kama baba, utapanga nyumba(utaacha kukaa gheto), utanunua kiwanja, utajenga, utaanzisha biashara nk nk.
Usipooa Sasa, maisha yako kila mwaka Inakuwa Ni kuhangaika na wanawake, Leo huyu, kesho huyu, miaka na miaka Ni kusuluhisha tu mpenzi.
Utakuwa Mwanaume hopeless kabisa.
Mimi nimeoa Nina miaka 6. Nina maendeleo ambayo naona kabisa ningekuwa mwenyewe Nisingekuwa hapa.