Sitosahau nilivyokoswa na risasi nikiwa baa

Sitosahau nilivyokoswa na risasi nikiwa baa

Habari wanajamii,

Salam kwenu na natumai nyote ni buheri wa afya, Naona nielekee kwenye hoja husika.

Ilikua ni siku ya mapumziko(weekend) siku ya jumapili tarehe 22 ya mwezi wa 9 mwaka 2007 maeneo ya mbezi beach eneo linafahamika sana kwa jina alimaarufu (Africana) njia ya kuelekea whiteSands au kwa zena, maeneo hayo kuna bar maarufu sana inafahamika kwa jina la highbury hapo ndipo lilikua eneo langu la kupumzisha akili baada ya mihangaiko ya kutwa nzima.

Siku hiyo ilikua ni mapumziko na ilikua ni jumapili nilitoka jioni na kuelekea kwenye hilo chimbo kumwagilia moyo na kampani ya wadau kadhaa kama ilivyokuwa kawaida yetu kujumika pamoja na kupata viburudisho kadhaa na kujiopolea warembo katika bar hiyo na walikua wazuri kweli kweli, Sasa wakati tukiendelea kumwagilia moyo hapo mdaa uliendelea kusonga hadi ilipofika majira ya saa nne(4) usiku ziliingia gari mbili aina ya land cruiser nyeusi na walishuka mababiloni nane(8) wakiwa wamevalia makoti marefu meusi na kofia aina ya Pama huku wakiwa wamefunika nyuso zao na walishikilia silaha aina ya mtutu(A.K.A 47) ghafla ulisikika mlio mkali wa risasi mbili zilizopigwa hewani na kuamuru watu wote tulale chini na tutoe kila tulichonacho tuweke pembeni, Sasa mimi wakati wa hamaki zikiendelea na purukushani za watu kujihami na vurumai zile nikaona nikimbilie counter kwakuwa nilijua kuna mlango wa nyuma nilifanikiwa ila huu ndio ungelikua mwisho wangu wa maisha kwani kati ya wale majambazi alifyatua risasi iliyonikosakosa usawa wa kichwa na kwenda kupiga nguzo za counter na kuacha tundu(shimo) kubwa sana.

Nashukuru nilifanikiwa kuokoa maisha yangu siku hiyo maana ilikua ni hatari sana hata kupelekea wahudumu wawili kufariki palepale baada ya kupigwa na risasi siku hiyo na baadhi ya wateja waling’olewa meno kwa kupigwa na vitako vya mtutu wakati wa uporwaji wa mali walizokua nazo siku hiyo.

Hili tukio sitakuja kulisahau maishani mwangu kabisa na huwa namshukuru mungu kwa ujasiri alionipa siku hiyo.

SEMA ulikoswa koswa sio kuokoa
 
Kuna mwana hapa kijiji anaitwa Deo Lyimo amukula chuma Ile siku ya May mosi
Walikuwa wametoka msibani wakasema ngoja waingie bar wale safar mbil 2 then ndio watembee mm mkawaimbia naumwa siwez kula pombe

Mkawasha bike yangu huyo nkatembea,nimefika home tu napigiwa simu washikaji zako huk wamekufa

Kumbe bwana ,baada ya kulewa wakawa wamepakizan Kwa bike wakati wapo njiani jamaa na gar yake akawa akawa kama anatak kuwagonga
Jamaa akaapita na gar wakamuwah Kwa mbele na pikipk wakamblock wanatka kumletea vurugu
Jamaa kazama ndan ya gar katoa chuma akataka kupiga juu but sabab ya ulevi ikamshinda nguv akamfikia jamaa yangu Deo Kwa kifua chuma ikamfumua mapafu yote,yule mwingn baada ya kuskia mlio akazimia


Majuz ndio tumemzika
Wachana na mtu wenye silaha ya aina yeyote hasa akiwa na hasira
Hiyo ni issue ya himo,walitaka kumletea za kuleta mjanja wa himo
 
Back
Top Bottom