----SEHEMU YA TANO - - -
Wale majamaa walipotoka kwenye uvungu wa bus ghafla wakanizingira wengine nyuma wengine mbele, nilipandwa na hasira nikajisemea moyoni "atakaegusa hili begi ama zangu ama zake". Kile kijamaa kigonvi kuliko wote kikataka kuchomoa kisu nikamuhawi kumkamata mikono nikampiga kichwa akadondoka wale wengine waliokuwa mbele yangu nikaona wamehamaki kabla ya kuchukua reaction yoyote nikampiga mmojawapo mtama wa kufa mtu nae chali, yule watatu sikumuona sijui alipoteaje ila kile kingine nilichokipiga kichwa nikaona kanaamka nikakandamiza kifuani na buti yangu, kule walinzi hawajui kitu maana ilikuwa ni silent league. Kutazama haraka nyuma naona yule mwingine hayupo akawa anakaita kajamaa ili wakimbie na mimi nikaona nikaachie mwanya kijanja ili kisepe. Kaliondoka chapu wakaenda kupanda pikipiki yao ilikuwa nyuma ya jengo la stend.
Nikiwa nahema sana tena kwa nguvu nilijiona sipo Sawa kabisa maana kama ndomaisha ni kutafuta sio hivi tena ilifika wakati hata ningeona banda la nguruwe Walah ningejiegesha kwenye matope maana ni banda linanistiri. Sikujua tena ule mda ni saa ngapi ila kwakuhisi ilikuwa ni majira ya saa kumi kasoro. Nikiwa nimeduwaa Sina hili wala lile nikasikia kishindo kizito puuuuuuuuh!!! Nikashtuka kuangalia chini ni bonge la jiwe sikujua limetoka wapi nikasema mpwayungu village hapa utakufa hawa watu hawana Nia njema inabidi uondoke. Shida ni kuwa hata nikiondoka naenda wapi?? Ile najiuliza nikaona jiwe limeshuka karibu na miguu yangu huku nikiskia sauti kwa mbali tuliaaaa huyu Leo Tupo nae anamaliza sisi tunaanza. Niliposkia hivo ikabidi niondoke hapo nikaenda tena kwa yule mlinzi awamu hii nikasema acha aniuwe tu saa nitaenda wapi mm jamani.
Kusema kweli sikujua wale jamaa kwa nini walikuwa hawasogei kwenye office za mashalah alipo huyu mlinzi lakini huenda wanajulikana kwa tabia zao ovu. Ile nimefika tu kwa mlinzi ikabidi nigonge mlango mlinzi akafungua nikasema kwa haraka samahani nimekuja kukata ticket. Mlinzi aliniangaliaaa mwishowe akasema weka begi hapo subiri wenyewe waje, namm nikamwambia haina shida ila naomba nijiegeshe hapa mpaka patakapopambazuka yule mlinzi sijui nini kilimkuta au kubadili fikra zake mpaka awe mwelewa kiasi kile. Nikaona katoa shuka lake akasema lala hapo. Sikuweza kuamini kwa mara nyingine naenda kupumzisha mwili wangu mida ya saa kumi usiku. Nikamwambia yule mlinzi Asante sana mungu akubariki mm nitakata tiketi ya saa moja, nimewahi tu mapema siti zinaweza kujaa, mlinzi akanielewa.
Mda huo nikiwa nimesimana kabla ya kulala nikaona kimya kizito sijui wake vibaka walienda wapi tena, kumbuka pale nje Kuna yule jamaa ambae alikuwa amelewa, nikaona kaamka nikasema hapa kazi ipo sijui nitaanza kutukanwa tena. Ahse nilidondosha chozi maana shida zote nilizopitia zilikuwa na maumivu makali sana, yani Sina pesa then wale vibaka wakawa wanataka chochote kitu, ila kama baada ya dakika 3 hivi hali yangu ikakaa sawa. Yule mlevi akaamka akaja akasukuma mlango kwa nguvu nikajiuliza nini tena?. Yule mlinzi akasikika akimwambia atoe mizigo na magunia yaliyopo mle ndani maana kumepambazuka. Sasa ajabu ni kuwa Ile booking office ni ndogo ili atoe Ile mizigo inabidi nisilale nitoke nje maana hakuna nafasi. Nikasema rahaulah!!!, kwa hiyo silali. Yule mlinzi akasema mwambie huyo mteja atoke hapo ndani.
Kwahiyo swala la kulala ikawa basi tena nasikutaka kujionesha nina dhiki na usingizi maana wangeshtuka kumbe mimi sio abiria and for sure sikuwa mteja Bali nilienda tu kukwepa ngumi za vibaka. Lakin wazo likaja ghafla kwanini nisilale alipokuwa amelala huyu mlevi. Mm nikaona haina shida ngoja nilale, Ile kwenda kuangalia mazingira ya yule mlevi alipokuwa amelala kumbe alijikojorea tena kojo jingi limechimba mpaka mfereji halafu pananuka. Miguu ilikufa gazi kwakweli ilibidi kujitoa ufahamu nilale hivyo hivyo japo nilijiuliza nikiamka asubuhi siwatasema mm ndonimejikojorea. Nikasema Poteleapote mimi navua begi langu naweka hapo ndani nilale Sasa.
Ile navua begi ili nilale nakuta limeyepuka zipu imefunguka bahasha yangu yenye vyeti siioni na baadhi ya nguo zilizokuwa juujuu,..... Ni simanzi nzito..zaidi ya maiti iliyofufuka ndani ya kaburi.
........ Inaendelea usichoke.......