------SEHEMU YA SITA - - - - - -
Nilipoangalia mazingira ya yule jamaa mlevi nikaona amekojoa maeneo yale na yale maboksi ya kulalia yamekojolewa, kwa kuwa nilikuwa na usingizi sana nasiwezi kulala kwenye michanga ilinibidi nichague Kati ya haya "kulala kwenye mikojo au kutokulala kabisa".. Nikasema mm nalala maana hakuna namna Ile navua begi mgongoni niliweke ndani nakuta limefunguliwa zipu na baadhi ya documents zilizokuwa kwenye bahasha ikiwemo vyeti vya shule na cha kuzaliwa hamna pamoja na nguo zilizokuwa juu hakuna pia. Hali hii iliniokoa kulala kwenye mikojo maana nilikosa usingizi moja kwa moja huku nikijisemea moyoni mpwayungu village umekwisha. Nilisogea pembeni kidogo tu nikaka chini kama gunia puuuh! Nilitulia kama dakika kadhaa huku sijui hatima yangu maana mambo yalishaharibika. Ikawa kumepambazuka ni saa kumi na moja sasa wengine wanaenda kuswali wengine wanaletwa stend kwenda Dar na maeneo mengineyo. Sasa lile jamaa Levi lililokuwa linatoa mizigo likiwa nyuma ya bus kule nikasikia linatukana, oyaaa mpumbav gani huyu ametupatupa manguo yake huku niliposkia tu nilizunguka chapu kufika pale dah [emoji22] sikuweza kuamini kuo zangu zipo pale japo zimekanyagwa hazitamaniki pamoja na bahasha ya vyeti vyangu, kumbe kipindi tunapigana na wale vibaka zile kurupushani zilifanya zipu ya begi ijifungue nguo na vitu vingine vikadondoka nakwakuwa tulikuwa kwenye body defense hakuna aliyejali wala kuona nguo na vyeti vikidondoka mpaka wale wahuni wanakimbia kwenda kujificha Mungu aliepusha hawakuviona pia.
Ikawa asubuhi saa kumi na mbili watu wa Kawa wengi kiasi mazingira hayo, wauza supu na Chai, shoe shine, bodaboda, abiria, waenda kazini, wasio na kazi, wafanyabiashara na wachuuzi, kila Aina ya kundi mji ulionekana. Kuji kujitazana uso ni mchafu suruwali chafu Shati ndousisema tena ilikuwa nyeupe Ikawa haina rangi, maeneo ya shingo nilichubuliwa na yule kibaka mwingine na kucha zake nikawa nina michirizi tu usoni, nguo zangu za kubadilisha zimekanyagwa ni chafu, sina simu, Sina hata Mia, Sina ninaemjua, tumbo halina kitu kabisa. Ajabu ni kuwa kila aliepita karibu yangu hakuacha kunitazama huku wengine nilisikia wanasema "" WANAJIFANYAGA MATAHILA KUMBE USALAMA WA TAIFA "" nikijisemea kumbe mpaka sasa muonekano wangu nishakuwa kama chizi? Sikuweza kulaumu maana kwa muonekano kiukweli hakili yangu haikuwa Sawa tena nilikuwa nimechafuka kupita maelezo halafu nina njaa nikawa kama natetemeka na wakiona ule mtetemo mpaka mdomo unavibrate halafu nipo rafu kwanzia unyayo mpaka nywele automatically wanajua ni Chizi.
Sasa vikwazo vyote vya kuitwa punguwani nikageuza kuwa fursa. Nilienda kwa mama mmoja hivi anauza chai na tangawizi mm nikaenda kukaa bila kusalimia njaa imeniponda kwelikweli. Sasa wateja waliokuwa pale mmoja wao akamaliza kunywa akampa mama 2000 akarudishiwa 1200 nadhani alikunywa Chai ya 800 lakini yule jamaa hakupokea chenji akasema mpe huyo kijana Chai kwenye hiyo chenji iliyobaki. Yule mama akatabasamu akasema Sawa lakini huku mm nikijifanya sijui chochote vinginevyo watajua naekti. Shukurani za pekee mungu ampe utajiri yule jamaa lakini Uhuni alionifanyia yule mama muuza Chai sitasahau maana katika 1200 ilobaki alinipa maandazi mawili tu na Chai ambapo jumla ni kama 600 tu. Nikijisemea moyoni huyu alieninunulia Chai sio mzawa, wazawa ni huyu mama wanaroho ya nyoka tena wanaweza kukuua. Kwakuwa nilikuwa mgeni na hali ya kimwili mda huo sikuweza kuleta ligi maana ingekuwa vituko.
Nikanywa Chai inaisha yote ila niliona mabadiliko nikawa najihisi niko Sawa. Akili ya kupotelewa na fedha ikarudi tena nikaona ni bora hili swala mda huu nilipoti office za bus. Kwakuwa nipo hapohapo nikaingia ndani nilipo fika pale nikamkuta yule mlinzi, mkaka mmoja anakatisha tiketi na wateja. Mwonekano wangu uliwafanya hata wasinifatilie kwani walijua huyu sio mteja ni tahila, nikasikia yule mkatishatiketi anamwambia mlinzi ebu mtoeni huyo nje nilistaajabu kwakweli kwahiyo yule mlinzi Kwakuwa nimemsumbua tangu usiku hakunitoa kwa upole tena ila ilikuwa ni shuruti naukizingatia amri ni ya boss hataki kibarua kiote nyasi. Kulikuwa Kuna rungu pembeni akashika nakunikong'ota begani na mgongoni akanipiga tanganyika jeck uelekeo ni nje tena mbali na mazingira yale huku nikisikia sauti za watu jamani mwacheni tu, mwacheni jamani hata sisi hatujui kesho yetu, hata wewe unaweza kuwa chizi mda wowote huku mlinzi akisema hili limenisumbua tangu usiku.
Akaenda kunisukuma kandokando ya dampo moja hivi lipo sokoni, pale stend na soko LA kilwa vimepakana tu. Nikakaa kidogo nikasema ivi ni kweli au illusion??. Haya matukio niyakweli? Nikasema hapana let me be serious. Sasa nikaamka kwenye lile dampo nikaenda tena kwenye zile office kufika pale kumbe yule mlinzi akawa ametoka kidogo nikaingia yule jamaa alienifukuza akataka kuleta za kuleta nikamwambia nina yanayonisibu nahitaji kuzungumza na office nikaona mwarabu mmoja hivi yeye alikuwa dreva kipindi nakuja kilwa akasema ebu mwacheni aongee. Nikajisemea moyoni "this is the golden chance Iam going to talk each and every thing". Nilitiririka nikaeleza Sakata la wallet nikaja la vibaka na chanzo cha Kuja kilwa kimsingi ilinibidi niwe muwazi. Yule mwarabu na wengine pale walinipa pole nyingi sana, kwa Mara ya kwanza namuona mwarabu mwenye utu.
Wote nikasikia kumbe ni mkaka na hakili zake tu jamani. Yule mwarabu akasema kijana swala la kupoteza wallet yako ndani ya bus letu pole sana ila sisi hatuwajibiki kwa hilo kwasababu hatuwezi kulinda kitu ambacho hatujakabiziwa. Wallet ipo kwenye mfuko sisi ofisi tunaionaje? Kwahiyo sisi hatuhusiki ila chakukusaidia wewe nenda kituo cha polisi utapata msaada. Nilichoka sana uso ukawa mzito saizi mama aliefiwa na mtoto wake wa pekee. Sina hili wala lile nikaona yule mwarabu kaingiza mkono mfukoni kachomoa 20000 akanipa akasema niondoke au wanisaidie kunipeleka polisi kama sipajui mm nikawaambia nitaenda mwenyewe, Ile nataka kuondoka pia Kuna mama mmoja hivi nadhani alikuwa abiria akasema kaka chukua hii elfu kumi itakusaidia nilimpa asante nyingi sana ila siku piga goti. Ikabidi hivyo hivyo nilivyo nikapotea mazingira yale Ile pesa ikiwa imewekewa ulinzi wa kiwango cha pentagon.
Nilikuwa mchafu sana utofauti wa mimi na nguruwe ni majina tu ila mwonekano ulikuwa similar, nikaona sio ustarabu kukaa hivi ngoja nitafute chaka la kusafisha ngozi yangu money can't make me disrespected nikazunguka nyuma kidogo Kuna kigest flani hivi kufika pale nikanawa kwa maji tiririka huku wahudumu wakinishangaa mwingine akasema mwacheni tu anawe mikono yake jamani akimaliza tutabadilisha maji. Yani natia kinyaa kiasi cha wao maji yatakayobaki kwenye ndoo watamwaga [emoji22]. Nikaenda walipo nikawaambia uhalisia mm sio chizi Ikabidi ni waambie mkasa wa usiku wakacheka wakasema pole mkaka tusamehe tukajua mengine. Nikawaambia kama naweza Pata msaada wakuoga wakasema Sawa nikaonyeshewa Bafu nikapewa kipande cha sabuni ya Eva nikaoga. Nguo zangu nikabadilisha nikachukua ambazo chache hazikudondoka usiku ule wa purukushani ila zimejikunja sana wale wadada wakacheka afu wakaniambia nizivue wa nipigie pasi. Niliflahi kwa kweli niliwapa wakazinyoosha nikavaa nikiwa nimeng'aa.
------inaendelea usichoke - - - - -