Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Katika hal aliyokuwepo sio rahisi akili yake kufanya kazi sawasawa.Kwanini kipindi una minguo michafu na una muonekano wa chizi hukubadilisha nguo ili uitengeneze muonekano mzuri ili hata ukitaka kuongea na watu wakuone sio chizi ila ukaamua uje kubadilisha baadae ulipoenda kuoga? Huoni kwamba unaondoa hisia za waodhani hii ni stori ya kweli kwa huko kupanga kwako matukio?
Kwa kweli uandishi wake unafurahisha😂Et bodaboda akauliza unaenda nikasema siendi [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Sasa hii si riwayaAisee Kuna wanaume wanapitia magumu
Watu tu wazinguzji mara chai mata nini sijuikwa kutaja majina ya shule nimeanza amini hii stori
Pole kwa mikasaTarehe 4 mwezi wa pili 2020 nikiwa katika msongo wa mzito wa mawazo yaliyotokana na ugumu wa maisha nilijikuta nafanya maamuzi magumu bila kutarajia. Nilikuwa nakaa gheto maeneo ya buguruni sheli japo gheto lilikuwa na mshikaji wangu ambae tulisoma nae primary mawenzi shule ya msingi iliyopo moshi mjini mwaka 2006 ndotulimaliza darasa la saba hapo.
Nikiwa nimelala saa sita usiku naona napigwa mgongoni kwa nguvu kuamka namuona rafiki angu tunaelala chumba kimoja pia ndommiliki wa gheto mm kaniweka tu kishkaji, nikasema kulikoni jamaa akajibu kiunyenyekevu akisema "oya demu wangu kafukuzwa na Dada ake alipokuwa anakaa kwahiyo hana pakwenda nasaizi ni saa saba usiku amekuja yupo hapo kibarazani anataka tulale humu kwahiyo please wewe ni mwanaume ebu tafuta ustaraabu wa kuondoka saizi ukija asubuhi tutaweka mambo Sawa ".
Nikamwambia sasa mda huu mm niende wapi ndugu na Sina hata sehemu yakujiegesha!? Akajibu nitajua mwenyewe, ikabidi nivae niende kimboka night club kupoteza mda nikawa naangalia movie kwenye mabanda ya pale kimboka maana majamaa huwa hawalali. Ilipofika asubuhi nikatia timu bahati nzuri nikakuta wote wameamka ila wapo kitandani nikamsalimia shemeji pamoja na jamaa angu japo hawakuonesha uso wa tabasamu walikuwa serious kiasi ambacho nilishindwa kuwaongelesha.
Nilipotazama juu kwenye enga zakuwekea nguo zangu ghafla sikuona nguo yoyote, nilipouliza jamaa akasema nimekuwekea kwenye begi ili ukija usisumbuke kuzipanga maana shemeji ako kasema yeye hatoki atakaa hapahapa sasa hatuwezi kulala watatu. Ilikuwa ni kipindi kigumu sana Kwangu zaidi ya Alpha konde alipotolewa madarakani. Nikatazama juu chini nikawaza nikasema haina shida.
Nikabeba begi langu nikawaaga wakasema kila raheli. Nilikuwa na simu Aina ya tecno F1 na mfukoni nikawa na 20000 nikasema Poteleapote nitaenda popote pale kutafuta rudhiki.
Kwa pesa niliyokuwa nayo kukaa Dar Es Salaam hapakunifaa tena, hiki ndokipindi ambacho mikoani unapaona nafuu kuliko jiji la Dar Es Salaam. Nikiwa na begi langu Zito la nguo mpaka mida ya saa kumi jioni nilikuwa sijajua niende wapi na nitalala wapi. Nilipoona mda unakwenda ilibidi nimfate jamaa mmoja ivi yeye anauza nguo za jinsi buguruni sokoni kama unaenda shell nilipofika alinichangamkia akijua ni mteja kumbe ni mtu mwenye dhiki aliehitaji msaada. Sikupoteza mda ilibidi nimwambie ukweli yote yaliyotokea ila msaada wangu mkubwa ilikuwa anitafutie mteja wa kununua simu yangu.
Akasema nauzaje nikamwambia simu nauza 90000 tu jamaa akasema ngumu kupata mteja leoleo Sema ngoja nimpigie simu Dada mmoja anauza chakula Ana shida sana na simu kubwa. Yule dada akaja alivyoiona na alivyokuwa na pupa ya kumiliki smart phone nikajua tu huyu ni mteja. Jamaa akasema niongee nae ilibidi nimwambie nauza laki moja maana ngozi nyeusi ukitaja bei harisi ushahalibu. Yule Dada akasema ana 80000 nikajifanya nakataa akaongeza 5000 nikamwambia toa pesa akanipa nikampa simu akaagana na jamaa akaondoka. Sasa kimbembe kikaanza Kati ya mm na huyu Dalali.
Jamaa nikampa 5000 akasema niache utani inabidi nimpe 20000 nikacheka kidogo huku mdomo ukiwa umekauka maana mpaka jua lilizama sijapata chochote cha kuchezesha kinywa changu.
Nikamwambia 20000 hapana kutokana na shida niliyonayo jamaa akasema vinginevyo anamwambia yule dada hii simu ya uwizi arudishe. Nikaona isiwe tabu nikampa 10000 nikasema hutaki naondoka na pesa sirudishi maana ilibidi nikunje sura vinginevyo nitakwama. Jamaa akapokea.
Alipopokea Ile pesa nikapotea mda huohuo. Sasa kimbembe nipakulala maana ikawa ni usiku huku nikiwa nimechoka sana. Nikaingia bar moja ivi inaitwa sewa. Nikaongea na muhudumu akasema Vyumba kwanzia saa saba usiku mdaa huu ni short time. Kwa kuwa nilikuwa na shida nikavumilia Ilipofika saa saba nikawa hoi kweli kweli nikiwa nimekaa kwenye kiti huku bar ikiwa imefungwa yule muhudumu akaja akasema kaka pole nenda kalale chumba hicho apo. Akasema nimpe 4000 tu maana naonekana sipo sawa. Nikampa pesa yake Nikaingia kulala japo madadapoa walikuwa wanagonga sana mlango niwafungulie lakini sikujali.
Asubuhi kukapambazuka nikasema leo inyeshe mvua liwake jua sikai Dar. Mm nimemaliza kidato cha sita ila sikubahatika kuingia chuo kikuu lakini najua sana kufundisha. Nikasema hapa ngoja nikatafute kibarua cha kufundisha mikoani ila tu isiwe dodoma. Nikawaza sana nikasema hapa safari ni kwenda lindi. Nikachukua daladala mpaka mbagala, ilikuwa saa sita mchana, kufika pale wakasema mda huu Gari za lindi mpaka temeke hapa mbagala ipo gari ya kwenda kilwa mda huu inaitwa MASHALAH.
Kwasababu kichwa changu mda huo hakikuwa sawa nikasema nikate tiketi tu hata ya kwenda kilwa nitajua mbele ya safari. Wakasema nauli Dar mpaka kivinje ni 11000 halafu Dar mpaka kilwa ni 13000.
Saa sita na nusu tukawa tumeondoka Dar Es Salaam kuelekea kilwa nikiwa Sina ndugu wala yoyote anaenijua lakini nikiwa na Amani ya moyo kwakuwa kilwa sio sudani wala Uganda ni Tanzania pia.
Inaendelea...
Safari ya kuelekea Kilwa ikaanza. Nililipa nauli ya Dar Es Salaam to Kilwa shilling 13000 mfukoni mpaka na panda bus nikawa nimebakiwa na 70000 tu kutokana na pesa nyingine Jana usiku Nililipa gest 4000 asubuhi kabla ya kwenda kukata ticket nilienda saloon kunyoa kwa 2000 baadhi ya pesa nilikula mihogo na maji ya kunywa njiani. Ubovu nikuwa kwenye siti nilikuwa nimekaa na mtoto mdogo wa kike ambae alipakiwa na mzazi wake ila yeye huyo mzazi hakuwa anasafiri sasa akaniambia kuwa nimsaidie kumwangalia lakini pia konda alikuwa amepewa taarifa kimsingi ni mtoto ambae huenda ni miaka 11 au 12 huyu dogo yeye alikuwa anashukia somanga. Kwahiyo nikakosa hata msaada wa kuanzia nikifika kilwa itakuwaje maana nilikuwa nategemea labda mtu nitakae kaa nae atanipa mawazo namna ya mji ulivyo na jinsi ya kuhendo swala langu. Tukiwa safarini ilibidi nimuulize huyu dogo endapo anaijua kilwa ili tu nipate pakuanzia dogo akasema yeye hajawahi fika anaishiaga tu somanga maana ndo kwao. Nikapiga moyo konde nikajisemea moyoni kuwa liwalo na liwe itajulikana.
Tukiwa safarini niliona kibao kimeandikwa IKWIRIRI gari likasimama kwa dakika chache nikajiuliza kulikoni tena kumbe Kuna wa mama walisimamisha wakapanda lakini cha ajabu walikuwa wananuka shombo ya samaki na mabeseni yao. Kuna mmoja alikuja kusimama karibu yangu nikamuuliza kama Ana samaki akasema Sina mwanangu samaki zimeisha. Nikakausha huku mawazo ya kwenda nisipopajua yanakuja nakunikosesha raha kabisa. Mungu yumwema baada ya dakika chache nilipata usingizi mzito sana hii nikutokana na siku ya jana kutokupata usingizi wa kutosha namm kulala Kwangu nikupumzisha mawazo. Nilikuja kushtuka kutokana na makerere mengi yawafanyabiashara wadogo wadogo hususani wanaouza biskuti, korosho, mahindi ya kuchoma na kadharika, kuangalia pembeni dogo simuoni niliyeambiwa nimwangalie nikasema kulikoni tena nikaamka chapu kwenye siti nikaenda kumuuliza konda dogo niliekaa nae yuko wapi??. Konda akasema nina mambo mengi kaka huyo dogo ni yupi? Nikamwambia nilikuwa nimekaa nae siti moja mm nikalala lakini cha ajabu simuoni konda akasema keshashuka. Nikamuuliza kwani somanga tumepita maana mm ni mgeni konda akasema nipande kwenye bus hapo tulipo ndosomanga yenyewe na dogo kashapokelewa na wazazi wake tayari.
Nikapanda kwenye gari. Bus likaiacha somanga na safari ya kwenda kilwa ikawa imewaka moto, niliona bus limejaza wa mama ambao walikuwa wanauza samaki kwenye bus. Kwa kuwa nilikuwa na njaa sana nikasema hapa samaki ni bei sana nilifanya mistake kutokununua muhindi wa jero somanga anyway nitauliza kama ana samaki hata wa buku mbili hata kambale nitatafuna usabato nauweka pembeni.
Nikiwa nasubiri afike Kwangu yule mama muuza samaki nikawaza wale wa mama wa mwanzo waliopandia IKWIRIRI kwani ni tofauti na hawa? Mbona siwaoni? Pembeni Kuna mzee mmoja alipandia somanga kwahiyo tukawa siti moja nikamuuliza akasema wale kwao ni somanga IKWIRIRI huwa wanaenda kuuza samaki wakiisha wanarudi somanga, nikasema hapo Sawa
Mama muuza samaki akawa amefika Kwangu nikamwambia sogeza beseni nichague mwenyewe mama akasogeza beseni la samaki nijichagulie.
Kucheki kwenye beseni niliona samaki wakubwa tupu Aina ya kibua na Changu. Nikajisemea moyoni hapa nimetoka patupu hawa samaki bei yake siiwezi lakini acha tu nimuulize ni bei gani akitaja nimlushe aendelee kuwauzia wengine. Yule Dada akasema samaki ni buku buku. Nikasema ebu rudia tena? Akasema kaka bei haipungui samaki mmoja ni elfu moja. Jamani sikuweza kuamini samaki mkubwa ambae Dar Es Salaam ni 7000 somanga anauzwa buku. Nikasema hapa ndopenyewe nikamwambia anifungie samaki wa buku mbili. Nikachagua samaki wangu huku nikiwa na tabasamu la kusahau shida kwa dakika chache nitakazotumia kumnyanvua samaki na minofu yake. Mama akachukua samaki akawafunga kwenye gazeti na kumimina chumvi kiasi. Kwa kua biashara ni cash to cash basi ikabidi nitoe wallet nimpe pesa yake. Ningaingiza mkono mfuko wa nyuma sikuona wallet nikasema ivi kumbe nimeweka mfuko wa mbele kuangalia mfuko wa mbele wallet hakuna, nikasema nini tena nikaangalia mifuko yote Hola jasho jembamba likianzaga tu kunitoka ujue kweli. Yule mama akasema napitia nikamwambia Sawa aendelee tu kuwauzia abiria wa nyuma akianza kurudi atapitia...
Ikabidi niangalie chini ya seat huenda imedondoka yani Sasa mpaka mwili ukawa unatetema kichwa hakipo sawa na wale samaki nikawadondosha chini kwenye abiria huwa wanapita tukiwa tumekaa.
Nikasema hapana sio kweli wallet imeenda wapi?? Ilibidi nipaniki nikamnyanyua yule mzee tukiokuwa tumepanda nae mzee alivyoniona tu kuwa sipo Sawa nikaona akasimama nikawa naangalia kila Engle ya seat lakini sikupata wallet yangu yenye pesa zangu. Abiria wa pembeni yangu wakaniuliza kulikoni nikawaambia kilichotokea wakaishia tu kunipa pole. Nikajisemea labda nikiweka kwenye begi? Lakini sio kweli maana mpaka begi linawekwa kwenye boot la bus nilichomoa pesa yangu nikiwa ndani ya bus nikanunua maji tukiwa mbagala rangi tatu. Nikiwa nimechanganyikiwa nikasikia konda anatangaza kijiji flani jina nimesahau Kuna jamaa yupo nyuma akasema kwa sauti "shusha" konda akamwambia asogee mbele maana washafika ikumbukwe kuwa Ile misamaki kipindi nasechi wallet yangu nilidondosha chini ya tule tunjia twakupita abiria, jamaa aliekuwa anashuka akapiga akazikandamiza na American buti zake samaki zote zikawa chapati tena zikagandamana na kapeti la bus. Ile nasema we jamaa umekanyaga samaki zangu akajibu kwa hasira hapo ndobakuli ilipo samaki unazibwaga njiani, ikabidi ninyamaze Sasa nikawa sipo Sawa kabisa maana wallet siioni samaki sijalipia na mama ndohuyo anakuja kutoka nyuma kudai pesa ya samaki shilling 2000 na samaki zimekanyagwa hazitamaniki kiasi ambacho hata paka hawezi kula.
HII NI SEHEMU YA TISA (9)Nilipoingia kwenye vichaka sikupata usingizi zaidi ya kuwa na mawazo yasiokwisha, ukiwa mpweke tena porini usiku masaa hayaendi kabisa kwahiyo ikabidi nikaze roho na kumwomba mungu maana hiki ndokipindi ambacho mungu anatamkwa mara nyingi zaidi yaalivyoandikwa kwenye vitabu vitakatifu. Sikupata majanga yoyote nilipokuwa ndani ya vile vichaka mpaka palipopambazuka, saa kumi na mbili kasoro ilinibidi nijongee taratibu kuelekea barabarani huku nikijifanya kama nimetoka tu kuchimba dawa. Hapakuwa na watu wanaopita maana ni asubuhi sana ni wachache tu niliowaona hata watatu hawafiki ila nikaona baada ya mda flani hiace, pikipiki na kila Aina ya magari yapita huku na kule nikasema kumbe kumekucha. Mda si mwingi ikapita hiace inaenda mjini konda akasema panda haraka nikamwambia nitajie nauli nitapanda akasema nauli ni jero, nikapanda kwenda mjini baada ya mda mchache tukawa tumefika ikawa ni saa moja na nusu hivi asubuhi. Ikumbukwe kuwa sikuwa na simu ila nina namba za huyo mkuu wa shule ya kineng'ene ninakoenda kwahiyo ikabidi kwanza nijiweke Sawa kimwili na kiakili nisije tena kutia aibu. Kama ilivyo ada ikabidi nizunguke kutafuta kigest uchwara nipate msaada wa kujimwagia mwili wangu maana nilikuwa nimeanza kupauka niliipata gest moja hivi nyuma kidogo ya stend ya mkoa inaitwa SOUTH HONOUR imetazamana na ukumbi flani hivi wanaonyeshaga mpira. Nikaingia mle ndani nikamkuta muhudumu ni mdada nikasema hapo Sawa hawa wanawake sio wachoyo, nikamwambia hali halisi akasema kuoga 500. Nilitaka kusita kidogo lakini nikasema Sawa nielekeze nioge nikaelekezwa nikaenda kuoga.
Nikamaliza kuoga nikavaa nguo zile zile maana hakuna zenye uafadhali zaidi ya hizi zilizopigwa pasi japo nazo zilianza kuonekana zimepitia misukosuko kiasi. Nikaingia mfukoni nikampa 500 yake huyo mdada anaitwa Zena kutokana na watu walipokuwa wanamwita maeneo hayo ni mmwera pia kutokana na tabia aliyoionesha nisingekuwa na pesa basi nisingeoga. Baada ya hapo nikabakiwa na 15000 tu mfukoni nikasema ngoja nitoe jero nipate tangawizi na kalimati ndonisepe, kutoka tu nje Kuna mdada alikuwa amebeba beseni akasema kaka karibu MING'OKO, hili jina ni geni Kwangu nikaona sio mbaya ashushe beseni nione aliponionesha nikaona ni mizizi tu kama hii inayotambaa kwenye miarobaini ila kutokana na njaa nikasema haya madude inaonesha yanashibisha mihogo cha mtoto kwahiyo nikamwambia anichotee ya 500 nikasisitiza ya kushiba. Alinijazia bakuli nikaanza kula japo hayakuwa na radha lakini sikujali maana lengo ni kushiba na sivinginevyo baada ya hapo nikampa 500 yake mm nikabeba begi langu nikapotea.
Ilinibidi nirudi tena stend nikachukue sasa dalalada za kwenda huko kineng'ene secondary ila kabla sijapanda nikauliza wenyeji wakasema nitashukia kituo kinaitwa MTANGE halafu baada ya hapo Kuna barabarani ya vumbi inaenda mpaka huko. Nikasema Sawa nikapanda hiace nakumuuliza konda bei akasema 500 nikamwambia hapo powa, hiace akaondoka mida ya saa nne hivi tukafika MTANGE mda si mwingi ila kumbe MTANGE ni mbele kidogo tu yapale nilipolala kwenye lile pori lenye mabwawa ya chumvi nilijiraumu kupoteza nauli Bure ila ikawa hamna namna. Nilipo shuka MTANGE bodaboda hawakosi kila penye kituo hawa watu, wakaja kunivamba kama sita hivi kwa mkupuo nikasema siendi popote, ilibidi nitumie hii akili maana bodaboda ukimuuliza njia atasema ni mbali ili apige mkwanja Sasa mimi sikutaka stori yoyote na wao japo wanasaidia pia. Nikaenda kumuuliza dogo mmoja hivi hana kazi yoyote akasema huko ni mbali sana tena shuleni ni mbali zaidi nikamwambia kutembea kwa mguu kwani watu hawaendagi? Akasema wanaenda baadhi ila ni mbali. Nikaondoka kuuliza bodaboda wakasema nauli 2000 nikasema Sina nina buku wakakataa wote japo Kuna jamaa akasema nisubiri apate kichwa kinachoenda kineng'ene ili tupande mshikaki nilipe buku, nikaona huu utoto nikasema njia iko wapi akasema nyoosha hii ya vumbi mpaka mwisho.
Safari ya mguu kwenda kineng'ene sekondari ikawaka moto nikasema saizi sitoi pesa hata itokee shida gani labda nivunjike mguu hata hivyo Nitatambaa tu, nilipiga mguu mpaka nikawa nahisi kizunguzungu viatu nilivyovaa vilikuwa vyeusi vikawa vyekundu huku natimuliwa na mavumbi ya gari na pikipiki. Safari nilipoona haifiki mwisho ikabidi nisite kidogo niulize wenyeji kama nimekaribia kufika huko niendako, nilisimama sehemu nikamuona mama mmoja kakaa chini ya mkorosho nikamfata kuomba maji ya kunywa, nilipokunywa maji nikauliza kama sijapotea njia ya kwenda kineng'ene akasema nifate hiyo hiyo barabara ila bado mbali sana. Nikampa Asante za kutosha nikasepa nilitembea sana jamani yani ilifika kipindi nikaona umasikini unatufanya binadamu tuonekane kama manyani hivi maana binadamu halisi ni ngumu kupitia hizi fedheha. Kama baada ya masaa mawili kwakuhisi nikasema niulize tena wenyeji Majamaa flani yakasema ni hapo tu mbele kidogo kunja kona kwenye hiyo mikorosho Fata barabara utakutana na shule. Baada ya mda nilifanikiwa kufika na kupokelewa na stuff members nilipowaambia wakasema mkuu wa shule yupo darasani ila nenda kwenye lile jengo ndoofisi yake ilipo kamsubiri.
Kweli baada ya nusu saa akaja ofisini akanikuta nje nikamwambia mm ndoyule tuliyeongea Kuja kufundisha, akasema Sawa ingia Tuongee. Tulitambuzana kwa mda na kucheka japo mm nilikuwa na cheka kumridhisha tu maana nimepondeka na matatizo sana. Baada ya maongezi akasema je nina ndugu huku nikasema hapana akasema Sasa kijana Shida ya hapa ni pakulala maana Kuna kijana hapa huwa nakaa pekee ake nikajua mtakaa wote ila bahati mbaya ndugu zake wamefika Jana usiku Kuja kumsalimia nahaijulikani wataondoka lini.
Baada ya hapo akasema nirudi ataniita. Namm nikamjibu kwa ghadhabu kwann hukunipa taarifa mapema akasema alimtaarifu yule mkuu wa shule ya kivinje sekondari ila akamwambia Sina mawasiliano na alijaribu kumpigia yule kijana bodaboda niliekuwa nae pale stend ya kilwa kivinje yule kijana akamjibu Ana abiria anampeleka sehemu kwa hiyo ameniacha stend. Hivyo taarifa ilitolewa mapema ila kutokuwa na mawasiliano ya simu ndotatizo. Yule mkuu wa shule akaniambia nirudi Hao wageni wakiondoka ataniita, kwahiyo safari ya kutoka kineng'ene kwenda sehemu nyingine ikaanza kuleta dalili.
........ Inaendelea usichoke.....