Sitosahau safari yangu ya Lindi iliyojaa maumivu na tabu nzito

Sitosahau safari yangu ya Lindi iliyojaa maumivu na tabu nzito

yu wapi kijana wa mihangaiko ya kilwa?

mpwayungu village i call upon you...
mpwayungu village i call upon you...
mpwayungu village kuya mara moyaaa...

kuyaaa.. kuyaaa... kuyaaa hapa mara moyaa
[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Nimemkumbuka The bold😂😂😂😂anyways ngoja tusubiri amalize kucheza prutable kwanza!!
 
TATEPA
Screenshot_20220518-233156~2.jpg
 
SEHEMU YA KUMI NA MBILI​

Basi baada ya kina Kidagaa na bosi zake kuondoka, nikaona isiwe tabu kwa vile njia naijua nikaanza kutembea kufuata uelekeo wa lile basi lilipopita huku nikiangalia alama za matariri ya basi la MACHINGA ili nisije kupotea. Niliendelea na safari kwa muda wa masaa matano bila kupumzika na begi langu la nguo likiwa kichwani. NIkapita sehemu nikakuta wanacheza prutable. Kiukweli walinishangaa sana wale wacheza prutable lakini mimi sikuwajali nikaendelea na safari yangu huku begi lipo kichwani.

Kufika mbele kidogo giza lilishaanza kuingia nikaona hapa sina jinsi itabidi tu nitafute mti nilale juu. Na wakati huo njaa inauma kweri kweri. Sasa wakati najadili jinsi gani nitapata chakula na mti wa kulala, nikaona kwa mbali taa za gari. Ikumbukwe giza lilikuwa tayari lishaingia na mimi lengo langu lilikua nifike Lindi Mjini ili kesho niende Mlandizi kwa rafiki ake baba. Nikaona ngoja nilipungie ili gari linaweza kunisaidia kufika Lindi Mjini. Gari ile ikakairbia na kweli ikasimama. Ilikua ni Nissan Hardbody. Aliekua kwenye gari akashusha vioo vya gari nikaweza kumuona vizuri, dah huwezi amini alikua ni Yule mwarabu wa basi la MACHINGA alienirudishia nauli na kunikataza nisipande ile costa yao. Pembeni ya mwarabu alikua Kidagaa. Yule mwarabu akanitukana na kuniambia nitafia porini kwa sabu ya ujuaji wangu kisha akapandisha vioo na nikamsikia Kidagaa anasema IMEISHA HIYO, gari likatimua vumbi.

Kiukweli nilichoka sana na kuanza kujilaumu huu ujuaji unaniponza kwa kweli sasa nitafia kweli kwenye miji ya watu.

Itaendelea ………………………….
😂😂😂
 
Amini usiamini sehemu nyingi alizotaja kwa majina hadi vijijini huko Chinongwe hajabuni ni sahihi.

Kama amebuni basi kweli amepita huko kote na anakujua vizuri.
Nakubaliana na wewe, ila hijaitaje Nangurukurulu, njia panda ya kwenda Kilwa.
 
Mkuu ipo.
Marehemu Mengi alikuwa na kampuni ya madini inamiliki Property (vitalu) vya kutosha huko.
Kuna watu toka kanda ya ziwa kibao wamelowea huko, wachimbaji wadogo wadogo.
Vijiji gani kuna hayo machimbo ya dhahabu.?

#MaendeleoHayanaChama
 
Hii hadith umeanza jichanganya sehemu nyingi ukiwa na lengo la kuionogesha. Unataka matukio mengi sana mpaka unakosea. Hilo la huyo binti kumtaka inaonesha kabisa hukujipanga vizuri kulielezea. Na hilo la Majangiri kuwasha moto mkubwa kiasi cha wewe kutembea dk 45 kuufikia ni uongo mwingine ambao hukujipanga.

Mwendo wa kuuona moto umbali wa dk 45 ni moto mkubwa sana ambao majangiri hawawezi hatarisha maisha yao hivyo. Na hapo ukataja bunduki SMG eti uliifahamu sababu ulipitia JKT acha kufanya watu wote humu watoto. Wewe andika hadithi kama hadithi si lazim udanganye kuwa yalikukuta.
 
Back
Top Bottom