SEHEMU YA KUMI NA MBILI
Basi baada ya kina Kidagaa na bosi zake kuondoka, nikaona isiwe tabu kwa vile njia naijua nikaanza kutembea kufuata uelekeo wa lile basi lilipopita huku nikiangalia alama za matariri ya basi la MACHINGA ili nisije kupotea. Niliendelea na safari kwa muda wa masaa matano bila kupumzika na begi langu la nguo likiwa kichwani. NIkapita sehemu nikakuta wanacheza prutable. Kiukweli walinishangaa sana wale wacheza prutable lakini mimi sikuwajali nikaendelea na safari yangu huku begi lipo kichwani.
Kufika mbele kidogo giza lilishaanza kuingia nikaona hapa sina jinsi itabidi tu nitafute mti nilale juu. Na wakati huo njaa inauma kweri kweri. Sasa wakati najadili jinsi gani nitapata chakula na mti wa kulala, nikaona kwa mbali taa za gari. Ikumbukwe giza lilikuwa tayari lishaingia na mimi lengo langu lilikua nifike Lindi Mjini ili kesho niende Mlandizi kwa rafiki ake baba. Nikaona ngoja nilipungie ili gari linaweza kunisaidia kufika Lindi Mjini. Gari ile ikakairbia na kweli ikasimama. Ilikua ni Nissan Hardbody. Aliekua kwenye gari akashusha vioo vya gari nikaweza kumuona vizuri, dah huwezi amini alikua ni Yule mwarabu wa basi la MACHINGA alienirudishia nauli na kunikataza nisipande ile costa yao. Pembeni ya mwarabu alikua Kidagaa. Yule mwarabu akanitukana na kuniambia nitafia porini kwa sabu ya ujuaji wangu kisha akapandisha vioo na nikamsikia Kidagaa anasema IMEISHA HIYO, gari likatimua vumbi.
Kiukweli nilichoka sana na kuanza kujilaumu huu ujuaji unaniponza kwa kweli sasa nitafia kweli kwenye miji ya watu.
Itaendelea ………………………….