yaani story za jf huwa zinaanza hivi,
sehemu ya kwamza ni (utumishi) huwa zinashuka haraka haraka sana,zinaweza tengwa na michango miwili miwili ya wasomaji.
sehemu ya pili ni(utegeaji)mleta story anapunguza speed ya kushusha story lakini mi msikivu,akiombwa aendelee anaendelea kwa kutoa sehemu kadhaa kisha anaomba udhuru,wakati huu itaendelea .......huwa ni nyingi.
sehemu ya tatu (udenguaji)mara nyingi hapa story huwa imenoga, hapa sasa story inakatwa ,katwa mnashindwa kujua hatima yenu[emoji16][emoji16],mletamada hajibu michango,akionekana anarusha moja anapotea,au anaweka ahadi ya siku,siku ikifika anaweka episode moja tu analala mbele.
sehemu ya nne(uvunaji )hapa ndipo sasa watu huanza kuitwa telegram kimya kimya,kwenda kuilipia huko sehemu zilizobaki kwa kujinoma.
sehemu ya tano(armagedon)hii huwa ni vita rasmi kati ya waliokuwa wanafatilia kwa umakini na mleta mada,hapa nisitie neno sana,lakini kimsingi mtu asipokuwa makini hakuna silaha itaacha kutumika,maana wananzengo wanakuwa wamemind kweli kweli,si ajabu mleta mada akaunganishiwa ID nyingine ambayo hataki tuijue,na mara nyingi story huwa inaishia hapa maana strong room zote huvunjwa,tutajua hata kama story umeiba sehemu.
NOTE,mods tunaomba mtu akianzisha story na kuishia hewani apigwe ban ya maisha,maana anautumia mtandao huu kutapeli watu.