Kimsingi hawakua ndugu ila walikua wanafahamiana na huyo ndugu yangu aliyetakiwa kunipatia pesa. Ilikua tukutane nae Arusha tuende nae Moshi.
Hapo Kijenge nilikutana na jamaa wakanielekeza Kwa hao walionisaidia, wanaishi Njiro. Kumbuka nimetembea bila kujua naelekea wapi nikatokea Kijenge, nikaona kibao Cha kanisa la Lutheran, kwenda pale nikaulizia Kwa hao walionisaidia nikaambiwa wapo Dar ( walikua na shughuli pamoja na huyo ndugu yangu Sasa). Lakini mie sikupewa taarifa, vinginevyo ningeenda Dar Kisha Moshi.
Hata wao walishangaa nimepajuaje huko Njiro ila walifurahi.
Ndugu yangu sio kwamba hakua mwaminifu, alijisahsu kunipa taarifa za mabadiliko ya mipango yetu. Kumbuka hata simu sikuwa nayo. Nilikua natembea na vocha za TTCL, ukiona kibox unaiingiza namba unapiga.
Walivyomaliza, akawakabidhi wale jamaa pesa, wakaniletea nikanunue vitu huyoo Moshi.
Hapo katikati sijaelezea nilienda Arusha Technical College Kuna jamaa tumetoka nae Kijiji kimoja, nikaambiwa hajafika Bado. Niliona Giza. Nashukuru Mungu nilishindwa kukaa Kule Njiro, ukiamka asubuhi unaletewa chai, unakula, haufanyi kazi yeyote ni kwenye TV tu. Nikarudi College Bahati nzuri jamaa akawa ameripot nilikaa huko hadi siku naenda kuchukua pesa Njiro, kununua vitu na kuelekea shule.
Huyo jamaa wa College Mungu aendelee kumbariki, alikuja pitia mitihani namshukuru Mungu alinipa nafasi ya kufanya chochote ( nikiwa nimeshaanza kazi). Bahati nzuri na yeye Yuko Dar siku hizi tumekua kama familia Moja.
Maisha Yana mambo mengi sana