Sitosahau: Siku niliyosingiziwa natembea na mtoto wa darasa la sita, yaani mbakaji

maandamano

JF-Expert Member
Joined
Nov 12, 2025
Posts
726
Reaction score
1,548
Nakumbuka ilikuwa mwaka 1995 nikiwa naishi mbeya Sokomatola,. Nilikuwa nafanya biashara za maduka ya rejareja, sasa unajua mambo ya uswahilini kuzoeana na vitoto ambavyo vinakusaidia kuvituma vikakununulie bidhaa

Basi siku hiyo nilikuwa nimetoka kuzindua duka langu jipya, mida kama ya saa moja usiku nimerudi kwenye duka jingine ambapo ndipo nilikuwa naishi, nikastuliwa mdogo wangu kuna watu nje wanakuita.

Nikamwambia mdogo wangu asubirie nimalize kula akaniambia kuna nyomi kubwa sana.

Ile natoka nakutana na kakijana ambako hupenda kukatuma, kakasema ni yule pale

Basi nikaanza kushambuliwa kwa maneno, kubwa zima linatembea na vitoto vidogo. Kipindi hicho nina miaka 19 na sijawahi kulala na mwanamke

Basi katika kubishana tukakubaliana tukamuone huyo binti wanayesema mimi natembeya naye

Ikabidi ianze safari ya kwenda kwa binti hapakuwa mbali sana. Kufika wakasema binti mwenyewe hayupo kesi watahukumu wenyewe.

Stori inaanza kuna katoto kama ka miaka 4 kalitumwa kakamuite huyo binti wa darasa la sita na kakijana ka miaka kama 14 ambako hukatuma kakaninunulie bidhaa, sasa yule dogo alipoingia ndani na ilikuwa kama saa moja usiku akadakwa.

Yule kijana wa mika 14 alipoona dogo kadakwa akatimua mbiyo kukimbilia kwao, ikabidi wazazi wa binti wamfuate wakiwa na kale katoto ili kakawaonyeshe nyumbani kwa yule kijana

Kufika nyumbani kwa dogo mkubwa wa miaka 14 akabananishwa si akanitaja mimi kwamba niliyemtuma

Ndiyo ikabidi waje dukani kwangu ndiyo pale naambiwa unaitwa kuna watu wanakutafuta

Basi dogo akaakomaa kabisa kwamba mimi ndiye nilimtuma na siyo mara moja, kumbuka huyo binti simjui na hayupo na sijawahi kumuona na hanijui,

Mwisho wa siku nikaambiwa niombe msamaha, kwa kweli niliwaambia kwa kabila langu siruhusiwi kuomba msamaha kwa kitu ambacho sijakifanya

Nikaambiwa nina kiburi,nilipigwa kama mwizi na familia nzima niko peke yangu

Yaani unataka kutoka mlangoni unarudishwa

Sitokuja sahau ili tukio, nashukhuru Mungu yalishapita
 
Nakumbuka ilikuwa mwaka 1995 nikiwa naishi mbeya Sokomatola,nilikuwa nafanya biashara za maduka ya rejareja,sasa unajua mambo ya uswahilini kuzoeana na vitoto ambavyo vinakusaidia kuvituma vikakununulie bidhaa
Basi siku hiyo nilikuwa nimetoka kuzindua duka langu jipya,mida kama ya saa moja usiku nimeludi kwenye duka jingine ambapo ndipo nilikuwa naishi,nikastuliwa mdogo wangu kuna watu inje wanakuita,nikamwambia mdogo wangu asubirie nimalize kura,akaniambia kuna nyomi kubwa sana,ile natoka nakutana na kakijana ambako hupenda kukatuma, kakasema ni yule pale,basi nikaanza kushambuliwa kwa maneno, kubwa zima linatembea na vitoto vidogo,kipindi hicho nina miaka 19 na sijawahi kulala na mwanamke

Basi katika kubishana tukakubaliana tukamuone huyo binti wanayesema mimi natembeya naye,ikabidi ianze safari ya kwenda kwa binti,hapakuwa mbali sana,kufika wakasema binti mwenyewe hayupo kesi watahukumu wenyewe,

Stori inaanza kuna katoto kama ka miaka 4 kalitumwa kakamuite huyo binti wa darasa la sita na kakijana ka miaka kama 14 ambako hukatuma kakaninunulie bidhaa,sasa yule dogo alipoingia ndani na ilikuwa kama saa moja usiku akadakwa,yule kijana wa mika 14 alipoona dogo kadakwa akatimua mbiyo kukimbilia kwao,ikabidi wazazi wa binti wamfuate wakiwa na kele katoto ili kakawaonyeshe nyumbani kwa yule kijana,kufika nyumbani kwa dogo mkubwa wa miaka 14 akabananishwa si akanitaja mimi kwamba niliyemtuma,ndiyo ikabidi waje dukani kwangu ndiyo pale naambiwa unaitwa kuna watu wanakutafuta

Basi dogo akaakomaa kabisa kwamba mimi ndiye nilimtuma na siyo mara moja,kumbuka huyo binti simjui na hayupo na sijawahi kumuona na hanijui,mwisho wa siku nikaambiwa niombe msamaha,kwa kweli niliwaambia kwa kabila langu siruhusiwi kuomba msamaha kwa kitu ambacho sijakifanya,nikaambiwa nina kiburi,nilipigwa kama mwizi na famiria nzima niko peke yangu,yaani unataka kutoka mlangoni unarudishwa,sitokuja sahau ili tukio,nashukhuru Mungu yalishapita
Duuuh pole sana mkuu ila sio mbaya

Maneno haya ukayawekea l badala ya r

Kura❎
Kula✅

Famiria❎
Familia ✅
 
Wewe unaonekana hata hio 1995 ulikua haujazaliwa bado
 
Ungekubali tu kwamba ulikuwa ukimkula na siyo kubaka, maana katika makubaliano hakuna ubakaji.
 
Since 1995 bado haujakomaa akili mpaka sasa bado unacheza the same game in different seasons

Sasa hivi unasapoti Maandamano ya kijinga ambayo utajikuta upo on trouble Kama ulivyokuwa 1995.

Sign of immaturity.
 
Kama baba yako hasapoti maandamano au anaikubali serikali ya CCM basi jua mimi nimemzidi akili
 
Back
Top Bottom