Sitosahau siku niliyotishiwa bunduki na baba!

Sitosahau siku niliyotishiwa bunduki na baba!

Ed Kawiche

JF-Expert Member
Joined
May 28, 2020
Posts
2,987
Reaction score
5,566
Ilikuwa hivi.
Muda mrefu sana yapata miaka 10 na ushee. Hiyo siku nilikuwa nacheza pool table mtaani, huo mchezo unaitwa "shamkware." Ni kamari na una majina mengi sana huo mchezo, pia mnaweza cheza watu wawili na zaidi.

Katika kucheza na kupiga mahesabu makali mwisho wa game mshindi nlikuwa mimi. kwenda kuchukua pesa nlizoshinda ghafla muona baba ananitazama kwa ukali kinoma!
Ikanibidi niiache ile pesa niondoke kinyonge tena kwa haraka nikijua tayari umeshakuwa msala!

Kurudi nyumbani dakika tano nyingi baba naye huyo! nilipigwa kila aina ya kipigo, ngumi, makofi, mateke na mkanda mwisho wa siku akachukua bunduki aina ya gobole na kulikoki kuelekeza kwangu lahaula!
Akanipiga mkwara mzito sana na kusema "nitakuua nikikuona unacheza michezo ya kipuuzi na sioni faida ya kuwa na kijana mjinga ndani ya nyumba yangu."
Niliogopa sana! Tangu hiyo siku mpaka leo hii pool table sina mzuka nalo kabisa.

Baba amenipa vitu bora maishani, muda wake, kujali kwake na upendo wake. Nafurahi sana kuwa nae katika maisha yangu.

He is my superman.
 
Ilikuwa hivi...
Muda mrefu sana yapata miaka 10 hiyo siku nilikuwa nacheza pool table mtaani, huo mchezo unaitwa "shamkware." Ni kamari na una majina mengi sana huu mchezo pia mnaweza cheza watu wawili au zaidi.

Katika kucheza na kupiga mahesabu makali mwisho wa game mshindi nlikuwa mimi. kwenda kuchukua pesa nlizoshinda ghafla muona baba ananitazama kwa ukali kinoma!
ikanibidi niiache ile pesa niondoke kinyonge nikijua tayari umeshakuwa msala!

Kurudi nyumbani dakika tano nyingi baba naye huyo! nilipigwa kila aina ya kipigo, ngumi, makofi, mateke na mkanda mwisho wa siku akachukua bunduki aina ya gobole na kulikoki kuelekeza kwangu...! akanipiga mkwara mzito sana na kusema "nitakuua nikikuona unacheza michezo ya kipuuzi na sioni faida ya kuwa na kijana mjinga ndani ya nyumba yangu."
niliogopa sana na tangu hiyo siku mpaka kesho pool table sina mzuka nao kabisa.

Baba amenipa vitu bora maishani, muda wake, kujali kwake na upendo wake. Nafurahi sana kuwa nae katika maisha yangu.

He is my superman.
Angekutia ulemavu ungekua unamlaumu hadi Leo, na ange kuua walimwengu wangekua wanamlaani,
 
Ndo najiuliza mshana alishikiwa nini wakati anakula kipondo! Kama sio hirizi pumuzi basi ilikuwa kibuyu..!

Appreciate ziwaendee wazee wetu wametulea vyema sana kwa vipondo na makaripio ni kitu ambacho kinaumuhimu na huja kuonekana mtu akishakuwa.
 
Back
Top Bottom