Kuna kipindi fulani cha nyuma nilitoka out na watoto wangu watatu wenye umri wa kujitambua kabisa kwan binti mkubwa alikuwa form 1,boys std lV na ll. Huko tulikutakana na trafic ambao tayari walikuwa wamesimamisha magari mengine,mie nikipita zangu,mara kama KM 1 Naona gari markll inanizonga kwa nyuma na mahorn mengi,mie nikasimama,kuchek ni wale traffic wako wawili,wakaja wananifokea eti kwanini nimesimamishwa na sikusimama,nikawajibu mimi hamkunisimamisha,mara ghafla nina kibao cha uso,mara cha pili,nikasikia watoto wanaanza kupiga kelele za kulia baba,babaaa!!!
Aisee ndo siku ya kwanza kukanyaga katiba ya JMT kwn hicho kipondo walichopokea hawatakaa wasahau maishani,nilidhalilishwa mbele ya watoto.Japo ilicost sana but potelea mbali nilijitunzia heshima mbele ya wanangu. Hii kesi ilimalizwa na viongozi wenye busara japo hapo nshaaumia kipesa, kazini na kifamilia pia.Wanangu niwaambia kila siku sitaki mwanangu awe polisi,nitamlaani maishani