Ilikuwa hivi...
Muda mrefu sana yapata miaka 10 hiyo siku nilikuwa nacheza pool table mtaani, huo mchezo unaitwa "shamkware." Ni kamari na una majina mengi sana huu mchezo pia mnaweza cheza watu wawili au zaidi.
Katika kucheza na kupiga mahesabu makali mwisho wa game mshindi nlikuwa mimi. kwenda kuchukua pesa nlizoshinda ghafla muona baba ananitazama kwa ukali kinoma!
ikanibidi niiache ile pesa niondoke kinyonge nikijua tayari umeshakuwa msala!
Kurudi nyumbani dakika tano nyingi baba naye huyo! nilipigwa kila aina ya kipigo, ngumi, makofi, mateke na mkanda mwisho wa siku akachukua bunduki aina ya gobole na kulikoki kuelekeza kwangu...! akanipiga mkwara mzito sana na kusema "nitakuua nikikuona unacheza michezo ya kipuuzi na sioni faida ya kuwa na kijana mjinga ndani ya nyumba yangu."
niliogopa sana na tangu hiyo siku mpaka kesho pool table sina mzuka nao kabisa.
Baba amenipa vitu bora maishani, muda wake, kujali kwake na upendo wake. Nafurahi sana kuwa nae katika maisha yangu.
He is my superman.