Sitosahau UKIMWI ulichofanya mtaani kwetu. Nyie watu wa mapenzi kuweni makini

Sitosahau UKIMWI ulichofanya mtaani kwetu. Nyie watu wa mapenzi kuweni makini

Naandika uzi huu huku nikiwakumbuka wengi waliokufa na gonjwa la hatari la ukimwi kule kwetu iringa mafinga kwenye misitu mbao mji wa biashara mji wenye viwanda vidogo vidogo vingi vya mbao mji wa majani ya chaibora

Mimi nilizaliwa mwaka 90 dsm ... baadae mwaka 95 tukahamia mafinga mjini kikazi mafinga ikiwa bado changa sana mwaka 97 nikiwa na miaka saba ndo nilipoanza kusikia hii term UKIMWI .

Mama angu alikuwa anafanya kazi hospital ya mafinga kama nurse pale sasa mara nyingi alikuwa anakuja na viperurushi navisoma nashangaa ukimwi nini

Jamani huu ugonjwa kama hujaoana mgonjwa ukimwi anavyokufa huwezi elewa pia utaendelea kupiga kavu ...lazima ushuhudie kama week mgonjwa kabla haja kata roho ndo utajua why HIV is king of all diseases hakuna kama hiv maana linaalika magonjwa yote HIVAIDS NI MFALME WA MAGONJWA sio utani

Nisipoteze muda kifo cha kwanza nilihushudia jirani yetu alikuwa mwalimu alianza mume alikonda mwaka 97 maskini afu walikuwa na watoto mapacha waliachwa bila wazazi asee jamaa alikonda kiasi hata mimi mtoto mdogo enzi hizo niliogopa na watu walikuwa hawatak kumgusa kabisa

Kifo cha pili bamkubwa wangu huyo yeye hakuchukua hata round alikuwa mlevi na ukimwi wa enzi hizo ni miezi mitatu tunazika

Haya sasa baada hapo tukahama mtaa tukamia mtaa mpya mtaa wa mikosi mkosi mkubwa hadi naandika uzi kwa uchungu mkubwa ni tulihamia ule mtaa mwaka 2003 hadi ninavyoongea 80% ya ule mtaa wamekufa na AIDS ule mtaa jamani wafanya wa serikali walijenga sana nyumba maana serikali ilipima na kuwaanzia kwa bei nzuri wafanyakazi wengi wakahamia huko na kujenga majumba kumbe wamehamia mtaa mtoa roho mtaa na majanga yake

Tulianza jiran mwanajeshi huyo tunafika akavuta ila mke wake hadi leo yupo anakula ARV ... kanali yule tulizika tukiwa tumehamia ule mtaa week tu

Upande mwingine alikuwa ni hakimu yule aliishi ishi akaja na kuvuta mama wa watu alikuwa na roho nzuri nahisi sijui nae ukimwi alitoa wapi

Kule idara ya maji dada mmoja akitwa eliza mchaga alikuwa mtaani kwetu nae hiv she was beautiful japo nilikuwa mdogo huyo alikufa hata mtoto hakuacha alicha nyumba tu

Kuna jirani yetu yeye pamoja na mke wameeacha mtoto wao mvuta bangi nao hivi huyu alikuwa fundi wa magari alijenga bonge la jumba mke alikuwa mzuri sana

Pia upande wa juu kwa mbele mwanajeshi mmoja yeye na mke walikuwaga na baa walipishana tu miaka ule mtaa jamani sina hamu Hiv iliwapiga fasta ikaacha watoto wakijilea

Kuna mwamba pia pale kitaa alikuwa usalama wa taifa yeye ndo alikufa yeye na mdogo wake ...huyo ni hivi mdogo wake alikula mke wa kaka yake nae akapata kaka yake anavyokufa akamwambia kama uliniabia mke wangu tutaonana very soon walikuwa wote watatu na mke juu wakaacha nyumba na katoto kachanga sijui kako wapi

Haya dada mmoja alikiitwa rukya mzuri sana alikuwa alijenga kijumba chake kipya kabisa akifanya kazi halmashauri nae kufika tu mafinga uzuri ulimponza tukazika akapenda hela za mpasua mbao mmoja tajiri miaka hiyo sijui yuko wapi alikuwa mweupe handsome alikuwa akiindesha shangingi miaka hiyo


Wadau mtaaa ni mkubwa mno uke 80% ya zile nyumba zimejengwa wajenzi wake HIV iliwabeba

Kila siku tukawa tunazika majirani tukijua kwetu salama 2012 babangu nae sijui alitoa wapi ila nilifuatialia nasikia alipata miaka ya 90 nae tukazika sikuwa na mahusiano mazuri na dingi hivyo hata msiba niliona normal tu nikamuuliza maza akasema si unajua mimi na baba ako tuliachana mmi mzima

Basi miaka ikaenda hadi mwaka 2018 nilikuw nimetoka zangu china nikaenda iringa kumpa hi maza mara kuingia chumbani nakuta ARV kasahau kitandani asee nililia sana nikamuuliza akaniambia samahani niliwaficha wanangu nikambatia kwa uchungu mkubwa sana siku kesho yake nikarudi dar..... nikisema why why mama angu nurse nae anaondoka

2020 akaanza kuumwa kumbe nae aliishia nao kimya kimya toka miaka 2000 mwanzoni .....2021 kuiukweli HIV/AIDS hapa ilionesha uwezo wake ilimua mama angu kikatili mno siwez simulia

Basi wadau nasema kutoka moyo ule mtaa wetu 80% nyumba zimebaki za urithi tu siwezi taja mtaa ila una jina la herufi tu ....kama uko mafinga utakuwa umeshaujua ni kwa kishua sana

Research niliyofanya why ukimwi uliua sana mafinga ni padogo pia na walio kufa sana ni wafanyakazi serikali ilikuwa ikileta wafanyakazi miaka ile 90 wanaambukizana sana bila kujua so wafanyakazi wengi mafinga miaka 90 kuna 2000 mwanzoni walikufa na HIV wengi ni wageni kutoka mikoa mingine including my mom

Kuna makaburi yanaitwa MET 50% half ya marehemu pale watu wa ukimwi wa miaka 90

RIP To those beautiful souls ....... nimesimulia machache sana kuhusu mafinga na HIV .... ni mengi mno nimeacha na niliyoshuhudia toka 96

Nilihama sijawahi kanyaga tena hata nyumba tuliuza kwa hasira maana majirani wote wamekufa now naishi dar kama businessman

Huwa sipigi demu bila kupima pia mtumiaji mzuri wa condom

Uzi wa leo asubuhi asanteni ila mafinga never forget japo napapenda sana familia ilihamia kikazi mji ule kumbe tulienda mazikoni..... kuweni makini na mafinga wafanyakazi mnaoenda hapo bahati yenu kumetulia ila miaka ile asee hapana
Wewe neenda kwenye wadi ya saratani ndo utajua ukimwi ni cha mtoto na inaua watu wazima na consciousness yao kwa % kubwa, kule cancer inaua watoto wadogo wazee vijana, masikini wenye pesa kila aina ya mtu. Ukimwi ni hatari ila is over rated kwasbb ni ajira kwa mashirika mengi na misaada kwa serikali zetu........je wa jua kwamba Malaria inaua watu hapa Africa Tanzania ikiwemo kuliko HIV? kila baada ya dakika 3 kuna mtu anakufa kwa Malaria hususani watoto walioko chini ya 5yrs infants......mtu anauwezo wakuishi na ukimwi kwa zaidi ya miaka 30, kinacho ua wa Tanzania ni umasikini ulio kithiri kupata chakula sahihi na dawa kwa wakati ila sio HIV
 
Verse 1

Nasikia raha jinsi nilivo star

Ni zaidi ya Robert De Niro

Nini top in Dar

Najukikana dunia nzima

Na kila kona hua natajwa langu jina

Sio tu watu wazima hadi watoto

Majina mengi a.k.a moto

A.k.a umeme a.k.a miwaya

A.k.a ngoma nzito isiyo na dawa

Ayaaaaah

Lakini sina ubaya

Na sibagui nchi za Africa nchi za Ulaya

Ni wengi tu nshawaondoa duniani

Na wengi bado nawatesa vitandani

Acha idadi kubwa ambao wapo safarini

Sijali mtoto wa kishua au unapoa uswahilini

Si mshajua nachozungumzia nini?

(UKIMWI UKIMWI UKIMWI)

Yeah a.k.a mimi

Natesa sana napokuingia mwilini

Akina gono kaswende wote baba yao mimi

Amini mi ndo kubwa la maadui

Na leo nakuja kwako usizuge kama hunijui

Halaa
Utanipata kwenye redio mi bado nimoo nimoooo!!

Utanipata kwenye video mi bado nimoo nimoooo!!

Madawa mengi yamenishindwa mimii bado nimoo nimoooo

Na imani nitawamaliza tu bado nimoo nimoooo

Yeah!!!

Kuna watu wananisema sana Mimi kama huyu mama terry sijui nimfanye Nini!?

Kila anasema kwenye tv magezeti na redio mi Wala......

Damn Ngwair noma
 
Halafu kuna watu wanaambiana waende kavu eti haya ni maisha tu sote tutakufa. Mungu atuepushe na huu ugonjwa umekaa pabaya
Nyie mnao penda uterezi sehemu hatari kupata ukimwi kwa juju ni hizi.
1. Kwaya za walokole na walokole wanao kesha.
2. Singo maza wasio nyoosha maelezo yao kuhusi mzazi mwenzie iko wapi.
3. Makahaba wa Buguruni na sinza wengi wameathirika siku nyingi.
4. Wanachuo walio tokea mikoani angalieni wengi wanaambukuza bila kujua kwasbb ya axcitement ya mjini.
5.sexnetwork ndani workmates kazini hususani hizi kazi za field zenye trips hao watu wana laliana sana chungeni usikubali mkeo apangiwe hizo trips atakuletea ukimwi, komaa na kipato chako hicho kdgo.
 
Naandika uzi huu huku nikiwakumbuka wengi waliokufa na gonjwa la hatari la UKIMWI kule kwetu Iringa Mafinga kwenye misitu mbao mji wa biashara mji wenye viwanda vidogo vidogo vingi vya mbao mji wa majani ya Chaibora.

Mimi nilizaliwa mwaka 1990 DSM, baadae mwaka 1995 tukahamia mafinga mjini kikazi Mafinga ikiwa bado changa sana, mwaka 1997 nikiwa na miaka saba ndo nilipoanza kusikia hii term UKIMWI.

Mama yangu alikuwa anafanya kazi hospital ya Mafinga kama nurse pale sasa mara nyingi alikuwa anakuja na viperurushi navisoma nashangaa UKIMWI ni nini.

Jamani huu ugonjwa kama hujaoana mgonjwa UKIMWI anavyokufa huwezi elewa pia utaendelea kupiga kavu, lazima ushuhudie kama week mgonjwa kabla haja kata roho ndo utajua why HIV is king of all diseases hakuna kama HIV maana linaalika magonjwa yote. HIV/AIDS NI MFALME WA MAGONJWA sio utani.

Nisipoteze muda kifo cha kwanza nilihushudia jirani yetu alikuwa mwalimu alianza mume alikonda mwaka 1997, maskini afu walikuwa na watoto mapacha waliachwa bila wazazi asee jamaa alikonda kiasi hata mimi mtoto mdogo enzi hizo niliogopa na watu walikuwa hawataki kumgusa kabisa.

Kifo cha pili ba mkubwa wangu huyo yeye hakuchukua hata round alikuwa mlevi na UKIMIW wa enzi hizo ni miezi mitatu tunazika.

Haya sasa baada hapo tukahama mtaa tukamia mtaa mpya mtaa wa mikosi mkosi mkubwa hadi naandika uzi kwa uchungu mkubwa ni tulihamia ule mtaa mwaka 2003 hadi ninavyoongea 80% ya ule mtaa wamekufa na AIDS ule mtaa jamani wafanya wa Serikali walijenga sana nyumba maana serikali ilipima na kuwaanzia kwa bei nzuri wafanyakazi wengi wakahamia huko na kujenga majumba kumbe wamehamia mtaa mtoa roho mtaa na majanga yake.

Tulianza jirani mwanajeshi huyo tunafika akavuta ila mke wake hadi leo yupo anakula ARV, kanali yule tulizika tukiwa tumehamia ule mtaa week tu.

Upande mwingine alikuwa ni hakimu yule aliishi ishi akaja na kuvuta mama wa watu alikuwa na roho nzuri nahisi sijui nae UKIMWI alitoa wapi.

Kule idara ya maji dada mmoja mchaga alikuwa mtaani kwetu nae hivi she was beautiful japo nilikuwa mdogo huyo alikufa hata mtoto hakuacha alicha nyumba tu.

Kuna jirani yetu yeye pamoja na mke wameeacha mtoto wao mvuta bangi nao hivi huyu alikuwa fundi wa magari alijenga bonge la jumba mke alikuwa mzuri sana.

Pia upande wa juu kwa mbele mwanajeshi mmoja yeye na mke walikuwaga na baa walipishana tu miaka ule mtaa jamani sina hamu HIV iliwapiga fasta ikaacha watoto wakijilea.

Kuna mwamba pia pale kitaa alikuwa usalama wa taifa yeye ndo alikufa yeye na mdogo wake, huyo ni hivi mdogo wake alikula mke wa kaka yake nae akapata kaka yake anavyokufa akamwambia kama uliniabia mke wangu tutaonana very soon walikuwa wote watatu na mke juu wakaacha nyumba na katoto kachanga sijui kako wapi.

Haya dada mmoja mzuri sana alikuwa alijenga kijumba chake kipya kabisa akifanya kazi halmashauri nae kufika tu mafinga uzuri ulimponza tukazika akapenda hela za mpasua mbao mmoja tajiri miaka hiyo sijui yuko wapi alikuwa mweupe handsome alikuwa akiindesha shangingi miaka hiyo.

Wadau mtaaa ni mkubwa mno ule 80% ya zile nyumba zimejengwa wajenzi wake HIV iliwabeba.

Kila siku tukawa tunazika majirani tukijua kwetu salama 2012 babangu nae sijui alitoa wapi ila nilifuatialia nasikia alipata miaka ya 90 nae tukazika, sikuwa na mahusiano mazuri na dingi hivyo hata msiba niliona normal tu nikamuuliza maza akasema si unajua mimi na baba ako tuliachana mmi mzima.

Basi miaka ikaenda hadi mwaka 2018 nilikuwa nimetoka zangu China nikaenda Iringa kumpa hi maza, mara kuingia chumbani nakuta ARV kasahau kitandani asee nililia sana nikamuuliza akaniambia samahani niliwaficha wanangu nikambatia kwa uchungu mkubwa sana siku kesho yake nikarudi Dar nikisema why why mama angu nurse nae anaondoka.

2020 akaanza kuumwa kumbe nae aliishia nao kimya kimya toka miaka 2000 mwanzoni, 2021 kuiukweli HIV/AIDS hapa ilionesha uwezo wake ilimua mama yangu kikatili mno siwezi simulia.

Basi wadau nasema kutoka moyo ule mtaa wetu 80% nyumba zimebaki za urithi tu siwezi taja mtaa ila una jina la herufi tu, kama uko mafinga utakuwa umeshaujua ni kwa kishua sana.

Research niliyofanya why UKIMWI uliua sana mafinga ni padogo pia na walio kufa sana ni wafanyakazi serikali ilikuwa ikileta wafanyakazi miaka ile ya 90 wanaambukizana sana bila kujua so wafanyakazi wengi mafinga miaka 90 kuna 2000 mwanzoni walikufa na HIV wengi ni wageni kutoka mikoa mingine including my mom.

Kuna makaburi yanaitwa MET 50% half ya marehemu pale watu wa UKIMWI wa miaka 90.

RIP To those beautiful souls, nimesimulia machache sana kuhusu mafinga na HIV, ni mengi mno nimeacha na niliyoshuhudia toka 1996.

Nilihama sijawahi kanyaga tena hata nyumba tuliuza kwa hasira maana majirani wote wamekufa now naishi Dar kama business man.

Huwa sipigi demu bila kupima pia mtumiaji mzuri wa condom.

Uzi wa leo asubuhi asanteni ila Mafinga never forget japo napapenda sana. Familia ilihamia kikazi mji ule kumbe tulienda mazikoni, kuweni makini na Mafinga wafanyakazi mnaoenda hapo, bahati yenu kumetulia ila miaka ile asee hapana.
Polee ndo mapito hayo
 
Wewe neenda kwenye wadi ya saratani ndo utajua ukimwi ni cha mtoto na inaua watu wazima na consciousness yao kwa % kubwa, kule cancer inaua watoto wadogo wazee vijana, masikini wenye pesa kila aina ya mtu. Ukimwi ni hatari ila is over rated kwasbb ni ajira kwa mashirika mengi na misaada kwa serikali zetu........je wa jua kwamba Malaria inaua watu hapa Africa Tanzania ikiwemo kuliko HIV? kila baada ya dakika 3 kuna mtu anakufa kwa Malaria hususani watoto walioko chini ya 5yrs infants......mtu anauwezo wakuishi na ukimwi kwa zaidi ya miaka 30, kinacho ua wa Tanzania ni umasikini ulio kithiri kupata chakula sahihi na dawa kwa wakati ila sio HIV
Dah mkuu mi naona kila ugonjwa ni mbaya hasa AIDS achana na HIV tunasemea ile stage ya progression to AIDS from HIV

Mtu anaumwa kila aina ya ugonjwa TB yake, homa yake, vidonda vyake, mkanda wa jeshi wake yaani kila ugonjwa maskini ni wake

Lets say kila ugonjwa ni hatari tu na tuombe MUNGU mno atuepushe na majanga
 
Sasa hivi asilimia kubwa ya watu wameathirika sema vidonge vinawaficha.
Its true,na inasemekana kuwa hawa wanaotumia dawa ukienda kupima na rapid test wadudu hawaonekani,yaani nikiwaza hapo nasema wacha tu nibaki njia kuu maana nimeshapoteza marafiki na ndungu wengi sana,nakumbuka katika jamaa waliotangulia kuna aliyefikia mpaka kutoka funza kwenye mwili ni kama alikuwa anaoza,aisee hii kitu ni hatari sana,HIV is real...
 
Thank you for a positive reminder.....it feels so safe to know that there are people who still care
...and it's disturbing reading a lot about HIV, yet you don't know your status.

Mnatuchanganya jamani, kuna wakati unatamani umpigie aliyekupa utam mara ya mwisho umuulize hivi we dada upo salama kweli😅😅
 
Utanipata kwenye redio mi bado nimoo nimoooo!!

Utanipata kwenye video mi bado nimoo nimoooo!!

Madawa mengi yamenishindwa mimii bado nimoo nimoooo

Na imani nitawamaliza tu bado nimoo nimoooo

Yeah!!!

Kuna watu wananisema sana Mimi kama huyu mama terry sijui nimfanye Nini!?

Kila anasema kwenye tv magezeti na redio mi Wala......

Damn Ngwair noma
Ngoma ina mistari kuntu, inaitwaje hio mkuu??
 
Verse 1

Nasikia raha jinsi nilivo star

Ni zaidi ya Robert De Niro

Nini top in Dar

Najukikana dunia nzima

Na kila kona hua natajwa langu jina

Sio tu watu wazima hadi watoto

Majina mengi a.k.a moto

A.k.a umeme a.k.a miwaya

A.k.a ngoma nzito isiyo na dawa

Ayaaaaah

Lakini sina ubaya

Na sibagui nchi za Africa nchi za Ulaya

Ni wengi tu nshawaondoa duniani

Na wengi bado nawatesa vitandani

Acha idadi kubwa ambao wapo safarini

Sijali mtoto wa kishua au unapoa uswahilini

Si mshajua nachozungumzia nini?

(UKIMWI UKIMWI UKIMWI)

Yeah a.k.a mimi

Natesa sana napokuingia mwilini

Akina gono kaswende wote baba yao mimi

Amini mi ndo kubwa la maadui

Na leo nakuja kwako usizuge kama hunijui

Halaa
Inaitwaje hii mkuu??
 
Iringa ni home na umezungumza ukwel japo Mafinga hapo mbona pa kirembo sana..
2010 February baada ya kumaliza kidato cha sita nilipata kazi kwenye volunteering program flan ilikua inajulikana kama student partnership worldwide (SPW) now days wanajiita RESTLESS DEVELOPMENT hii organization ilikua inajihusisha na mambo hizo za UKIMWI na Peer education.

Nilifanya kazi sana Njombe, Ludewa na Makete..zaid zaid Ludewa na Vijiji vyake..Lugarawa..Masimbwe...Itundu... n.k.

Aisee kule ukimwi ulikua UNAOUNA KWA MACHO HIVIIIII yan huhitaji kipimo wala nini.Watoto wadogoo vijana watu wazima kwa wazee jinsia zote ukimwi ulikua unafagia sanaaaaa..

Nashkuru Mungu those days nilikua sijaanza kuchakata bado.
E bwana ukimwi ni noma sana.
Those days elimu rika ilikua adimu sana na kwakwel moja ya vitu najivunia nilifanya kwenye maisha yangu ya u teeneger basi ni mojawapo.

Tulikua tunapiga sana semina.
Mnaandaa matamasha ya muziki kutoa elimu nakumbuka sana pande za ULAYAS secondary pale Mlangali Ludewa...Anzisha sana maktaba za kujisomea kutengeneza HIV Awareness kwa vijana ... ligi la soka ambazo zilikua zinaambatana na Semina na upimaji wa HIV ..

Ukimwi umetafuta sana nyanda za juu kusini magharib.Sanaaa yani.
Kilimo cha chai na miti kama kichocheo cha maambukizi..
IKUMBUKWE maeneo hayo yalikua maarufu sana kutoa ma house girl.Wakija Dar wanaukwaa ukimwi wakianza kuumwa wanarudishwa Huku vijijin wazaz wasio na elimu ya kuwahudumia wanaambukizwa..plus pisi imetoka mjini vijana wa village nao wanapambana japo waonje ...Imooooo..
Dah ukimwi ni nyokoo sanaaaa.

But now days angalau hali ime stablize..

Nakumbuka pale Mlangali nilishakutana na li shangazi Nurse limoja hakyanan lile lilikua linataka nili gonge kila mitego aliniwekea haikunasa maana akili yangu kipinzi hiko badoo hata mbususu sizijui so nikawa hata sielewi yule mama anataka nini 😄😄😄😄..

All in all AIDS Kills.
Tatizo mojawapo kwasasa watu tumesusa Kampeni za kuijengea jamii HIV AWARENES sawa kuna mitandao siku hiz ndio ila hili la kila mtu kujifunza kibinafs ni hatar sana maa internet is full of wrong information.

TUJILINDE..TUJIKINGE
 
Back
Top Bottom