Sitosahau UKIMWI ulichofanya mtaani kwetu. Nyie watu wa mapenzi kuweni makini

Sitosahau UKIMWI ulichofanya mtaani kwetu. Nyie watu wa mapenzi kuweni makini

Ndugu acha kujitoa ufahamu...Shida ya Ukimwi ni HATIA ambayo mgonjwa anajiskia. Jamii inavyokuchukulia, kila mtu anakuona unahatia, malaya, mchafu.Hata kama umeletewa na mwenza..utaonekana ulioa au kuolewa na malaya tu...Hiyo ndo tatizo ya Ukimwi..Yaani familia, ndugu..wote wanakulaumu.Wewe mwenyewe unajilaumu...tamaa...n.k.

Na ndo maana watu huwa wanaficha....hawasemi kama wameungua..

UKIMWI ni shida ndugu..Mzee wangu UKIMWI ulimbeba 2011, lkn hata yeye hakuwahi kutamka anaumwa nini, anajua tunajua lkn..hawezi sema chochote....
Kwa sasa kuna magonjwa konki kuliko UKIMWI

Mfano tu, kisukari kikikubeba vizuri hakuna namba utaacha kuisoma

Kisukari kinaambatana na

1. Shida ya macho hatimaye upofu
2. Ganzi mwili mzima
3. Matatizo ya miguu hatimaye kukatwa mguu
4. Vidonda visivyopona
5. Upungufu wa kinga mwilini na kuumwa mara kwa mara (UTI, miwasho nk)
6. Presha ya kupanda
7. Stroke
8. Kufeli figo
9. Uume kulegea na kushindwa kufanya tendo la ndoa

NB: Kwa sasa UKIMWI ni rahisi kuucontrol kuliko baadhj ya magonjwa yasiyoambukiza, mfano kisukari

naongea kuhusu ugonjwa wa kisukari kwa experience kabisa maana ninadeal na wagonjwa wa kisukari.


kibaya zaidi ukiwa na magonjwa haya kunakuwa na masharti magumu ya ulaji, ila UKIMWI unajiachia tu

UKIMWI ni swala la psychology tu, mtu akiwa na njia nzuri za kumanage stress na depression anatoboa kirahisi
 
Kwa sasa kuna magonjwa konki kuliko UKIMWI

Mfano tu, kisukari kikikubeba vizuri hakuna namba utaacha kuisoma

Kisukari kinaambatana na

1. Shida ya macho hatimaye upofu
2. Ganzi mwili mzima
3. Matatizo ya miguu hatimaye kukatwa mguu
4. Vidonda visivyopona
5. Upungufu wa kinga mwilini na kuumwa mara kwa mara (UTI, miwasho nk)
6. Presha ya kupanda
7. Stroke
8. Kufeli figo
9. Uume kulegea na kushindwa kufanya tendo la ndoa

NB: Kwa sasa UKIMWI ni rahisi kuucontrol kuliko baadhj ya magonjwa yasiyoambukiza, mfano kisukari

naongea kuhusu ugonjwa wa kisukari kwa experience kabisa maana ninadeal na wagonjwa wa kisukari.
 
Kuna mwalimu mmoja wa kike (RIP) tukiwa tunakaa kota, siku za mwisho mwisho wa uhai wake alitoka nje ya nyumba yake mida ya saa 2:30 usiku hana nguo mwilini, akawa anazungumza kwa sauti kubwa,"vijana njooni muone jinsi ninavyoteseka. Msiache tamaa ziwaponze, mtakufa. Mimi nitakufa sio muda mrefu, njooni mjionee ninavyoteseka". Alikaa kama miezi 2 hivi akaaga dunia akiwa kwao Mbeya. Hiyo ilikuwa mwaka 2009 hivi
Mwenyezi Mungu amsamehee dhambi zake! She did her duty!

Apumzike kwa amani! [emoji120][emoji120]
 
Umekaa mitaa choka sana sisi tulifikia mtaa unaitwa pipeline ndo kulikuwa uzunguni nyumba zina angalizika kwa mbali mwaka 96 nyumba nzuri kidogo na vihela kiukweli vilikuwepo tulitoka navyo dar vya uamisho wa maza tukapanga pipeline

baadae ndo tukamia huo mtaa wa mikosi wenye jina la herufi tu 2003...... mtaa wa kishua sana miaka hiyo ndo majanga yalipo anzia ... na kwanini nilijua majirani zetu wanakufa kwa ukimwi mama angu alikuwa nurse so alikuwa anapiga story tunasikiliza pia alikuwa anawauguza wakiwa hoi pale mafinga hospital...

pamoja na u unurse wake ukimwi ulikuja kum bamiza RIP my mumy...sitosahau ulivyoniangalia those dying eyes my god niliumia mara mwisho na kuniambia napenda harufu(perfume nilipaka) yako mwanangu nikasema bye ukajibu bye ndo maongezi yetu ya mwisho i will always love you ...leo naandika haya tribute yako pia kuwaasa wengine.... nikapanda basi la abc kurudi dar nikijua sito kuona tena ..kweli baada week tatu kaka angu alinipigia simu kusema mama is no more....

Tulificha kifo cha kusema kafa tu kwa presha ila ilikuwa AIDS .... hata wanangu nitakuja kuwasilimua hii story ya ule mtaa na hakuna hata sehemu.nimedanganya wala kusingizia maana maza alikuwa nurse so alijua hali za watu wengi wakilazwa

Mbaya zaidi mwaka 99 waliweka hodi maalumu la watu wa HIV so ukiwa huna hela afu una ukimwi unasekwa huko nadhani ile hodi walikuja kuivunja kuondoa unyanyapaaa ilikuwa chini kabisa kule

Nimesimulia story asilimia 5% tano tu ya majanga nilishuhudia mafinga why niliyajua mengi nilikuwa mtoto wa nurse tena mtoto pendwa.....

Asanteni wadau uzi wangu umesomwa na watu wengi naamini umetoa elimu kubwa kuhusu hili gonjwa ..

Wengine wanasema bora ukimwi kuliko kansa...ni hivi ukiwa na ukimwi hata kansa unapata kiu rahisi mno yaani ukimwi ni kama boss la magonjwa yote linapiga simu moja kansa njoo mara moja inakuja....likiamua kumwite chawa wake TB fasta tu.... bado kijana wake mkanda jeshi

Ukimwi ni boss wa magonjwa ukiamua inaweza sema basi tumvuruge awe kichaa unakuwa kichaa madaktar wanajua hili yaani ninaposema UKIMWI ni boss la magonjwa yote namaanisha linaweza sema tuletee vidonda tu utapata hadi ufe

Hizo kansa kwa watu wenye ukimwi ndo nyumbani maana boss wao ukimwi si anakuwepo ndani utashangaa unapata kidonda hakiponi then kansa

AIDS SIO MCHEZO
The last moment with your mother, umeniliza mkuu!

Pole sana, ndugu zetu waliotutangulia wapumzike kwa amani!
 
Itakuwa Kitobo kuelekea Buyango, Kanyogo na kigarama huko na baadhi ya vijini vingine!
Hayo maeneo nilipolipita miaka ya 2011 kuna sehemu nilijionea magofu ya nyumba hadi miti imeota ndani niliumia sana. Maana yake Ukimwi uliua familia zote mpaka watu wa kurithi hata nyumba wakakosekana [emoji24][emoji24]
Labda kanyigo ila hiyo kitobo kuelekea buyango nimeishi hilo eneo miaka hiyo hii unayosema haipo acheni uongo,

Kagera eneo lililoathirika kiwango hiki inasemekana ni kanyigo,
 
Jamani acheni kukamia game,piga ka bao kale ka kwanza tu ambapo kila MTU anautelezi mwanamke uke unakuwa umelowa,kisha tambaa sasa wewe ukitaka ukomae na cha pili na tatu lazima upate
Magonjwa ya zinaa je?
 
Huu uzi umenifanya nijipime [emoji23]
PXL_20230521_065147219.jpg
 
Wewe neenda kwenye wadi ya saratani ndo utajua ukimwi ni cha mtoto na inaua watu wazima na consciousness yao kwa % kubwa, kule cancer inaua watoto wadogo wazee vijana, masikini wenye pesa kila aina ya mtu. Ukimwi ni hatari ila is over rated kwasbb ni ajira kwa mashirika mengi na misaada kwa serikali zetu........je wa jua kwamba Malaria inaua watu hapa Africa Tanzania ikiwemo kuliko HIV? kila baada ya dakika 3 kuna mtu anakufa kwa Malaria hususani watoto walioko chini ya 5yrs infants......mtu anauwezo wakuishi na ukimwi kwa zaidi ya miaka 30, kinacho ua wa Tanzania ni umasikini ulio kithiri kupata chakula sahihi na dawa kwa wakati ila sio HIV
Well said,it's no longer a top killer disease
 
Iringa ni home na umezungumza ukwel japo Mafinga hapo mbona pa kirembo sana..
2010 February baada ya kumaliza kidato cha sita nilipata kazi kwenye volunteering program flan ilikua inajulikana kama student partnership worldwide (SPW) now days wanajiita RESTLESS DEVELOPMENT hii organization ilikua inajihusisha na mambo hizo za UKIMWI na Peer education.

Nilifanya kazi sana Njombe, Ludewa na Makete..zaid zaid Ludewa na Vijiji vyake..Lugarawa..Masimbwe...Itundu... n.k.

Aisee kule ukimwi ulikua UNAOUNA KWA MACHO HIVIIIII yan huhitaji kipimo wala nini.Watoto wadogoo vijana watu wazima kwa wazee jinsia zote ukimwi ulikua unafagia sanaaaaa..

Nashkuru Mungu those days nilikua sijaanza kuchakata bado.
E bwana ukimwi ni noma sana.
Those days elimu rika ilikua adimu sana na kwakwel moja ya vitu najivunia nilifanya kwenye maisha yangu ya u teeneger basi ni mojawapo.

Tulikua tunapiga sana semina.
Mnaandaa matamasha ya muziki kutoa elimu nakumbuka sana pande za ULAYAS secondary pale Mlangali Ludewa...Anzisha sana maktaba za kujisomea kutengeneza HIV Awareness kwa vijana ... ligi la soka ambazo zilikua zinaambatana na Semina na upimaji wa HIV ..

Ukimwi umetafuta sana nyanda za juu kusini magharib.Sanaaa yani.
Kilimo cha chai na miti kama kichocheo cha maambukizi..
IKUMBUKWE maeneo hayo yalikua maarufu sana kutoa ma house girl.Wakija Dar wanaukwaa ukimwi wakianza kuumwa wanarudishwa Huku vijijin wazaz wasio na elimu ya kuwahudumia wanaambukizwa..plus pisi imetoka mjini vijana wa village nao wanapambana japo waonje ...Imooooo..
Dah ukimwi ni nyokoo sanaaaa.

But now days angalau hali ime stablize..

Nakumbuka pale Mlangali nilishakutana na li shangazi Nurse limoja hakyanan lile lilikua linataka nili gonge kila mitego aliniwekea haikunasa maana akili yangu kipinzi hiko badoo hata mbususu sizijui so nikawa hata sielewi yule mama anataka nini [emoji1][emoji1][emoji1][emoji1]..

All in all AIDS Kills.
Tatizo mojawapo kwasasa watu tumesusa Kampeni za kuijengea jamii HIV AWARENES sawa kuna mitandao siku hiz ndio ila hili la kila mtu kujifunza kibinafs ni hatar sana maa internet is full of wrong information.

TUJILINDE..TUJIKINGE
Restless,mwalimu wangu wa high school aliachaga kazi akajiunga huko.alikuwa anaitwa Nicas Ngumba.Huko huko akakutana na demu wa kizungu
 
Hujawahi muona mgonjwa wa aggressive cancer
Si bora ukimwi unaweza ishi hata miaka 20 aggressive cancer ndani ya miezi kinakua ni kipindi cha mateso makali sana mgonjwa ni analia mda wote au anaugumia maumivu mda wote
Recently nimeondokewa na ndugu yangu ,aliteseka sana worse enough hakuwahi hata shiriki sex.Kifo ni kifo,cha kumuomba mungu tuwe na mwisho mwema.
 
Hukua na mahusiano mazuri na baba yako,alafu unaona ni sawa? this time na wewe ni baba...vipi watoto wako waseme hivi
 
Back
Top Bottom