Sitosahau UKIMWI ulichofanya mtaani kwetu. Nyie watu wa mapenzi kuweni makini

Wewe neenda kwenye wadi ya saratani ndo utajua ukimwi ni cha mtoto na inaua watu wazima na consciousness yao kwa % kubwa, kule cancer inaua watoto wadogo wazee vijana, masikini wenye pesa kila aina ya mtu. Ukimwi ni hatari ila is over rated kwasbb ni ajira kwa mashirika mengi na misaada kwa serikali zetu........je wa jua kwamba Malaria inaua watu hapa Africa Tanzania ikiwemo kuliko HIV? kila baada ya dakika 3 kuna mtu anakufa kwa Malaria hususani watoto walioko chini ya 5yrs infants......mtu anauwezo wakuishi na ukimwi kwa zaidi ya miaka 30, kinacho ua wa Tanzania ni umasikini ulio kithiri kupata chakula sahihi na dawa kwa wakati ila sio HIV
 
Utanipata kwenye redio mi bado nimoo nimoooo!!

Utanipata kwenye video mi bado nimoo nimoooo!!

Madawa mengi yamenishindwa mimii bado nimoo nimoooo

Na imani nitawamaliza tu bado nimoo nimoooo

Yeah!!!

Kuna watu wananisema sana Mimi kama huyu mama terry sijui nimfanye Nini!?

Kila anasema kwenye tv magezeti na redio mi Wala......

Damn Ngwair noma
 
Halafu kuna watu wanaambiana waende kavu eti haya ni maisha tu sote tutakufa. Mungu atuepushe na huu ugonjwa umekaa pabaya
Nyie mnao penda uterezi sehemu hatari kupata ukimwi kwa juju ni hizi.
1. Kwaya za walokole na walokole wanao kesha.
2. Singo maza wasio nyoosha maelezo yao kuhusi mzazi mwenzie iko wapi.
3. Makahaba wa Buguruni na sinza wengi wameathirika siku nyingi.
4. Wanachuo walio tokea mikoani angalieni wengi wanaambukuza bila kujua kwasbb ya axcitement ya mjini.
5.sexnetwork ndani workmates kazini hususani hizi kazi za field zenye trips hao watu wana laliana sana chungeni usikubali mkeo apangiwe hizo trips atakuletea ukimwi, komaa na kipato chako hicho kdgo.
 
Polee ndo mapito hayo
 
Dah mkuu mi naona kila ugonjwa ni mbaya hasa AIDS achana na HIV tunasemea ile stage ya progression to AIDS from HIV

Mtu anaumwa kila aina ya ugonjwa TB yake, homa yake, vidonda vyake, mkanda wa jeshi wake yaani kila ugonjwa maskini ni wake

Lets say kila ugonjwa ni hatari tu na tuombe MUNGU mno atuepushe na majanga
 
Sasa hivi asilimia kubwa ya watu wameathirika sema vidonge vinawaficha.
Its true,na inasemekana kuwa hawa wanaotumia dawa ukienda kupima na rapid test wadudu hawaonekani,yaani nikiwaza hapo nasema wacha tu nibaki njia kuu maana nimeshapoteza marafiki na ndungu wengi sana,nakumbuka katika jamaa waliotangulia kuna aliyefikia mpaka kutoka funza kwenye mwili ni kama alikuwa anaoza,aisee hii kitu ni hatari sana,HIV is real...
 
Thank you for a positive reminder.....it feels so safe to know that there are people who still care
...and it's disturbing reading a lot about HIV, yet you don't know your status.

Mnatuchanganya jamani, kuna wakati unatamani umpigie aliyekupa utam mara ya mwisho umuulize hivi we dada upo salama kweliπŸ˜…πŸ˜…
 
Ngoma ina mistari kuntu, inaitwaje hio mkuu??
 
Inaitwaje hii mkuu??
 
Iringa ni home na umezungumza ukwel japo Mafinga hapo mbona pa kirembo sana..
2010 February baada ya kumaliza kidato cha sita nilipata kazi kwenye volunteering program flan ilikua inajulikana kama student partnership worldwide (SPW) now days wanajiita RESTLESS DEVELOPMENT hii organization ilikua inajihusisha na mambo hizo za UKIMWI na Peer education.

Nilifanya kazi sana Njombe, Ludewa na Makete..zaid zaid Ludewa na Vijiji vyake..Lugarawa..Masimbwe...Itundu... n.k.

Aisee kule ukimwi ulikua UNAOUNA KWA MACHO HIVIIIII yan huhitaji kipimo wala nini.Watoto wadogoo vijana watu wazima kwa wazee jinsia zote ukimwi ulikua unafagia sanaaaaa..

Nashkuru Mungu those days nilikua sijaanza kuchakata bado.
E bwana ukimwi ni noma sana.
Those days elimu rika ilikua adimu sana na kwakwel moja ya vitu najivunia nilifanya kwenye maisha yangu ya u teeneger basi ni mojawapo.

Tulikua tunapiga sana semina.
Mnaandaa matamasha ya muziki kutoa elimu nakumbuka sana pande za ULAYAS secondary pale Mlangali Ludewa...Anzisha sana maktaba za kujisomea kutengeneza HIV Awareness kwa vijana ... ligi la soka ambazo zilikua zinaambatana na Semina na upimaji wa HIV ..

Ukimwi umetafuta sana nyanda za juu kusini magharib.Sanaaa yani.
Kilimo cha chai na miti kama kichocheo cha maambukizi..
IKUMBUKWE maeneo hayo yalikua maarufu sana kutoa ma house girl.Wakija Dar wanaukwaa ukimwi wakianza kuumwa wanarudishwa Huku vijijin wazaz wasio na elimu ya kuwahudumia wanaambukizwa..plus pisi imetoka mjini vijana wa village nao wanapambana japo waonje ...Imooooo..
Dah ukimwi ni nyokoo sanaaaa.

But now days angalau hali ime stablize..

Nakumbuka pale Mlangali nilishakutana na li shangazi Nurse limoja hakyanan lile lilikua linataka nili gonge kila mitego aliniwekea haikunasa maana akili yangu kipinzi hiko badoo hata mbususu sizijui so nikawa hata sielewi yule mama anataka nini πŸ˜„πŸ˜„πŸ˜„πŸ˜„..

All in all AIDS Kills.
Tatizo mojawapo kwasasa watu tumesusa Kampeni za kuijengea jamii HIV AWARENES sawa kuna mitandao siku hiz ndio ila hili la kila mtu kujifunza kibinafs ni hatar sana maa internet is full of wrong information.

TUJILINDE..TUJIKINGE
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…