Sitosahau UKIMWI ulichofanya mtaani kwetu. Nyie watu wa mapenzi kuweni makini

Kama Waafrika wengi tunakufa kutokana na magaonjwa yanaonezwa na nzi na MTU ,why Serikali zetu kukazania kuongeza madaktari,vifaa na mahospitali kwa ajili ya hayo magonjwa yatokanayo na Mbu na nzi huku tungeweza kuja mazalia yote ya Mbu na nzi Nchi nzima?
 
Kunawatu wanautetea sana ukimwi [emoji1787][emoji1787][emoji1787] kwamba ni ugonjwa mdogo, kunakitu sio bure [emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Na wenyewe ndio unapend kutetewa
 
Dar njoo Kinondoni.... Huku tunaambukizana Ngoma kama kuambukizana mafua tu.
 
Yani mkuu hawa ndugu unaweza kukuta hawaishi pamoja kila mtu ana maisha yake sehemu nyingine ila sasa mmoja akipata mara na dada yake mkoa mwingine kule anao na mwingine tena hvyo yani jaribu kuchunguza

Nilishawahi kusikia hiyo kitu ila naona kama coincidence hakuna uhalisia wa katika familia mmoja akipata basi na wengine watapata ,kama unafanya mapenzi(dry au na mwenza ambaye si mwaminifu) basi kuna possibility ya kupata ukimwi.
 
Nakubaliana na wewe kuwa afya ya binadamu ni biashara za watu. Kama mm ninavyoaamini kuwa upungufu wa nguvu za kiume ni illusion na watu wanaigwa sana pesa.

Ila kwenye hili la ukimwi nakupinga kwa 101%. Sote tunajua kuwa ukimwi si ugonjwa ula ni UPUNGUFU WA KINGA MWILINI. VVU ndio hushusha kinga ya mwili na hapo ndiowaliko wa magonjwa mengine unapokuja. Kinga ikishuka utapigwa na kila gonjwa.

Mkuu kama mtoa mada alivyosema, ni ngumu kumuelewa kama hujawahi kushudia haya. Tulioona watu wa karibu yetu wakiteseka acha tuendelee na imani yetu potofu
 
hii dunia bana,unaweza pia ukabaki njia kuu ila wife akamtamani handsomeboy wa mtaani kwenu unakuja kuambukizwa hujui.

ila jamani kuna midada imeumbika aiseee
Moni Ana Ngoma Yake Anakwambia " Mjini Kuna Toto, Kuna Toto ", kuna watoto wazuri bhana aisee
 
Kwani dalili za ngwengwelism toka umeipata inachukua Mda gani? Maana mimi na kondom ni kama Bush na Osama tu.
Anyway kwa hiyo wote humu hamjawahi kuuza mechi et?
kijana km umri unaruusu kamata mwenza mpime vyovyote itavyokuwa muoane muwe huru. kurukaruka hakusaidii mwisho wa siku utaleta tafrani kwako na kwa wategemezi wako. kumbuka majuto na ninge uja bdae. chukua chuma icho.
 
Ludewa duuuuh....Ludewa secondary.....
 
Ukimwi km hujawahi mshuhudia mgonjwa anakuaje especially zile hatua za mwishoni utauchukulia POA Ila km umeshuhudia utaelewa Jambo

Ipo hivi

Watu hawasemi Ila Mimi wacha nivunje yai Mimi sio muathrika ya ukimwi Mimi nimemhudumia mgonjwa wa ukimwi mpaka anakufa alikua jirani yangu

Samahani kwa kusema hivi Ila ukimwi ni km Curse fulani yaan hii familia walikua jirani yetu kipindi Baba yao yupo hai kulitokea kutokuelewana kati ya Baba na watoto huyu Baba alikua na watoto wawili tu mmoja wa kike mmoja wa kiume, kabla hajafa akawalaani

Jamàa kaka mtu alikua ni fundi umeme akawa anapenda sana Pombe, siku ya siku hio siku aliyoenda kuukwaa Mimi nilisikia asubuhi maana mtaa hauna Siri ukifanya Jambo mtaani ukadhani watu hawatojua sahau, basi baada ya kuukwaa unaambiwa aliambikiza familia yake yote unajua ile miaka ya 90 kuja 2000 basi akaanza mke akaenda na maji (aliemuambukiza) punde si punde akaja mtoto wake wa kike akaenda (alikua anamhudumia Baba yake na Mama yake nae akapata), chanzo Cha yote siku hio ya kunywa Pombe na story zake kuzagaa mtaani ni kwamba alikula barmaid ambae anaejulikana kwamba ana VVU jamaa sababu ya tungi akapita kavu kuja kucheck ndio hivyo, mkewe akapuuzia zile habari hakuchukua round nae akawa kwenye grid ya taifa

Dada yake jamàa alipozidiwa dada alikua mzima kabisa km Mimi na wewe alipoona kaka anazidiwa huruma ikamuingia basi amsaidie kaka yake sijui alikosea nini masikini na yeye akapigwa shoti kwenda kupima anao, wakawa wote wagonjwa hanawa wa kumsaidia jamàa hali mbaya akawa na kijana wake wa kiume wa mwisho huyu kijana nae alikua ndio amemaliza mafunzo ya ufundi amerudi nyumban kumkuta Baba yake hali mbaya akaanza kumsaidia kumhudumia

Kijana hakuchukua mwezi nae sijui alikosea nini, akapigwa shoti akaanza kuumwa kwenda kupima anao tayari kashaambukizwa, Basi kukawa na ugomvi yule dada akawa analalamika kila siku kua kaka yake ndie aliemuambukiza yeye alikua mzima tu

Jamàa akazidiwa tena akawa hana tena mtu wa kumsaidia zaidi ya kujisaidia mwenyewe au baadhi ya majirani wenye huruma na wengi walikua wanatoka mbali waliokua wanakuja sana sana ni walokole fulani hivi maana watu wakawa wanaogopa kwamba yeyote atakae msaidia yule lazima na yeye umpate ni km Curse fulani alafu Mzee alikuja niambia na kunisisitizia kua niwe nae makini ninapoenda kumnyoa maana Baba yao aliwalaani, Basi mpaka jamàa anakufa alikua anaomba msaada wa dawa na dawa ya mwisho aliyoomba kwa kutuma meseji kwa njia ya simu kwa watu aliomba dawa ya kuunyoosha uti wa mgongo maana kwa maelezo yake anakwambia mishipa ya misuli ya uti wa mgongo ilivutika kiasi Cha yeye kushindwa kunyanyuka kitandani hata kuweza kupumua vizuri na hivyo haikuchukua siku 2 alivuta pumzi ya mwisho

Mimi nilikua namsaidia km kinyozi wake yaan nywele zikikua alikua haendi saloon hivyo basi ananiita nyumbani kwake niende nikamnyoe nywele nimpunguze zimekua nyingi, Mara nyingi tulikua tunapiga story za mpira Yanga na Simba na kutaniana sana na Mara nyingi jamàa alikua ananipigia sana marufuku kuhusu wanawake ananiambia 'wanawake we waangalie sana sio watu wazuri kabisa hawa sio watu wazuri watakumaliza' hapo akilenga na dada yake ambae aliamua kususa kumhudumia na ukizingatia Mimi sio muongeaji sana nilikua naitikia tu 'sawa' Basi tunapiga story huku namnyoa fresh kabisa tukimaliza Nampa kioo anajiangalia anasema 'hapa safi' nimemaliza ananipa maji nanawa mikono na sabuni maana kichwani ni km alikua na ukoko, ndio ukoko ukipika ugali ule wa chini kwenye ugali unaitwa ukoko ukiupekecha km ungaunga, Basi nikimaliza kunawa namuaga naendelea na Mishe zangu nyingine

Wakati namnyoa na kumsaidia huduma ndogo ndogo za hapa na pale kwa tahadhari maana
nilijua huyu jamaa kawaambukiza dada yake na mtoto wake wa kiume na mtoto wake wa kike (alikufia Mwanza) nilichokibainii ni kwamba

Kwanza jamàa alikua anajipenda Ila kutokana na umasikini ndio hivyo kifo kimempeleka mapema, wakati namnyoa nilikua namkagua maana yeye anakua mbele Mimi nipo nyuma namnyoa hivyo namwangalia mgonjwa wa ukimwi anakua kuaje nikaona ni hali ya kukonda sana ngozi inavutika na inawambana na skeleton la mwili (mwili wake wa asili hakua mnene) kisha kifuani hapa sijui kwanini kifuani sio mwanamke sio mwanaume wakifika stage za mwisho pananenepa kuanzia kifuani kuja maeneo ya tumbo, mwanaume anaonekana km ana maziwa na yule jamaa alikua km ana maziwa na alipofika stage ile kutembea kwenda job ikawa ni mtiti yaan sio Siri UKIMWI kuna stage unatesa utakula hizo mbaazi (ARV) Ila kuna stage utafika utaanza kukutafuna jamàa alikufa kifo Cha mateso sana kaacha mtoto wake aliemuambukiza na dada yake aliemuambukiza wote wapo Ila wanakula dawa hadi sasa ni story ya kusikitisha sana
 
Hii Tanzania nyumba ziachwe mpka watu wakae bure? Acheni story za kitoto basi!
shangaa na wewe mkuu, itoshe kusema taarifa nyingi za UKIMWI kwa miaka ya hivi karibuni ni za kupika na hazina uhalisia wowote.
 
Yani mkuu hawa ndugu unaweza kukuta hawaishi pamoja kila mtu ana maisha yake sehemu nyingine ila sasa mmoja akipata mara na dada yake mkoa mwingine kule anao na mwingine tena hvyo yani jaribu kuchunguza
Charrote upo sahihi kabisa. Mara nyingi wanakuwa hawaishi pamoja, tena unakuta mikoa tofauti na Kila. Mtu ana mke au mume wake. Lakini mwisho wa siku ndo hivyo
 
Halafu kuna mtu anaongea kirahisi rahisi tu
 
Itoshe tu kusema kwamba Iringa, makambako huko sijui njombe, ludewa kuna baridi sana[emoji23][emoji119] Yan kujaamiiana ni inevitable[emoji19]

Nimesoma Mafinga(Advance) na nilifanya school project Njombe dooh kwenda darasani tuu balaa yan inaweza pita siku nzima ni baridii sana hata jua haliwaki

ko kwa utafiti huo mdog nikagundua kuwa ngono kwa maeneo ya kule haiwezi kukwepeka kabisa ko HIV haikwepeki kabisa afu nyumba za kulala wageni bei chee sana[emoji23] na hawa madereva wa malori hawa wengi wanapaki sana magari maeneo hayo ko ni balaa tupu[emoji119][emoji119]
 
Charrote upo sahihi kabisa. Mara nyingi wanakuwa hawaishi pamoja, tena unakuta mikoa tofauti na Kila. Mtu ana mke au mume wake. Lakini mwisho wa siku ndo hivyo

There is something behind this Sh..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…