Sitosahau UKIMWI ulichofanya mtaani kwetu. Nyie watu wa mapenzi kuweni makini

Sitosahau UKIMWI ulichofanya mtaani kwetu. Nyie watu wa mapenzi kuweni makini

Ila kuna kitu kimefichwa kwenye AIDS ikitokea kwenye familia mmoja akaupata trust me lazima na wenzie aidha Wawili Au watatu watapata,ni kitu kama laana hivi but anyway naendelea na tafiti
Kweli hicho kitu nimeshuhudia sana, ni ngumu sana kwenye familia mmoja akapata wengine wakabaki salama.
Huko moshi nimeshuhudia kuna familia kaka na dada karibu wote wanaotumia dawa, hapo tayari wawili walishafariki kwa tatizo hilo miaka ya 90 huko ila waliobaki wanatumia dawa sasa. Najiulizaga nakosa majibu
 
Kwa mujibu wa baiolojia ya kidato cha pili che; virusi (vikiwemo vya UKIMWI) vina sifa zote za viumbe hai na visivyo hai.

Kwahiyo; kinapokuwa nje ya seli hai kinakuwa inactive (dormant) punde tu kinapopata access ya kuwa kwenye seli hai kinaanza kuishi.

Haya mambo magumu sana kuyaelewa! 😁
Unanitisha sasa mkuu
 
Ila kuna kitu kimefichwa kwenye AIDS ikitokea kwenye familia mmoja akaupata trust me lazima na wenzie aidha Wawili Au watatu watapata,ni kitu kama laana hivi but anyway naendelea na tafiti
Kwenye Familia yetu hovyo sana wanaimani potofu, ulipo mbeba baba yangu mdogo wakawa wanasema karogwa saivi Aunt yangu nae anao japo hataki kumeza dawa kakonda balaa.
 
MSAADA wakuu Kuna jamaa Aliandika BONGE LA UZI HAPA KUELEZEA UKIMWI.


KAMA KUNA MTU ANAO NAOMBA ANITUMIE.
ALIKUWA ANADAI UKIMWI SI UGONGWA.
MAELEZO YAKE YALIKUWA MAREFU SANA.

AU ANITUMIE LINK INBOX.
 
Issue siyo Tohara. Mafinga wanatiana sana sababu ya hali ya hewa na pia magari makubwa mengi yanapiga kambi pale. Sisi wengine tumefanya research ni mji unaokua sana. Na una mchanganyiko mkubwa kama mleta mada alivyosema. Hali ya baridi na vyakula pale watu wanatiana masaa 24.
Kwanin Dar isiongoze kwa UKIMWI wakat ndio mkoa unaopokea kila aina ya wageni..?
Wanaume magovi ni rahisi sana kupata maambukiz, Njombe-Iringa ni mkoa wenye wanume wengi magovi kuliko mkoa wowote ule Tanzania... Njombe Iringa ndio mkoa wenye mabango mengi ya TOHARA...
Kwahiyo imani potofu kuhusu tohara ndiyo imechangia ongezeko kubwa la HIV...
 
Kabisaaaa alafu wee umeambikizwa ngoma unakaaje kizembe zembe lazima na wewe uondoke na wengine kama 20 hivi. Yaani mpaka siku unakata roho hamna kitu cha maana kwenye mwili wako

Mkuu kweli "Unatembelea Ring" au unachangamsha Genge? Miaka 16 bila ARV au wewe ni carrier?
 
Mama yako aliacha dawa
Naandika uzi huu huku nikiwakumbuka wengi waliokufa na gonjwa la hatari la UKIMWI kule kwetu Iringa Mafinga kwenye misitu mbao mji wa biashara mji wenye viwanda vidogo vidogo vingi vya mbao mji wa majani ya Chaibora.

Mimi nilizaliwa mwaka 1990 DSM, baadae mwaka 1995 tukahamia mafinga mjini kikazi Mafinga ikiwa bado changa sana, mwaka 1997 nikiwa na miaka saba ndo nilipoanza kusikia hii term UKIMWI.

Mama yangu alikuwa anafanya kazi hospital ya Mafinga kama nurse pale sasa mara nyingi alikuwa anakuja na viperurushi navisoma nashangaa UKIMWI ni nini.

Jamani huu ugonjwa kama hujaoana mgonjwa UKIMWI anavyokufa huwezi elewa pia utaendelea kupiga kavu, lazima ushuhudie kama week mgonjwa kabla haja kata roho ndo utajua why HIV is king of all diseases hakuna kama HIV maana linaalika magonjwa yote. HIV/AIDS NI MFALME WA MAGONJWA sio utani.

Nisipoteze muda kifo cha kwanza nilihushudia jirani yetu alikuwa mwalimu alianza mume alikonda mwaka 1997, maskini afu walikuwa na watoto mapacha waliachwa bila wazazi asee jamaa alikonda kiasi hata mimi mtoto mdogo enzi hizo niliogopa na watu walikuwa hawataki kumgusa kabisa.

Kifo cha pili ba mkubwa wangu huyo yeye hakuchukua hata round alikuwa mlevi na UKIMIW wa enzi hizo ni miezi mitatu tunazika.

Haya sasa baada hapo tukahama mtaa tukamia mtaa mpya mtaa wa mikosi mkosi mkubwa hadi naandika uzi kwa uchungu mkubwa ni tulihamia ule mtaa mwaka 2003 hadi ninavyoongea 80% ya ule mtaa wamekufa na AIDS ule mtaa jamani wafanya wa Serikali walijenga sana nyumba maana serikali ilipima na kuwaanzia kwa bei nzuri wafanyakazi wengi wakahamia huko na kujenga majumba kumbe wamehamia mtaa mtoa roho mtaa na majanga yake.

Tulianza jirani mwanajeshi huyo tunafika akavuta ila mke wake hadi leo yupo anakula ARV, kanali yule tulizika tukiwa tumehamia ule mtaa week tu.

Upande mwingine alikuwa ni hakimu yule aliishi ishi akaja na kuvuta mama wa watu alikuwa na roho nzuri nahisi sijui nae UKIMWI alitoa wapi.

Kule idara ya maji dada mmoja mchaga alikuwa mtaani kwetu nae hivi she was beautiful japo nilikuwa mdogo huyo alikufa hata mtoto hakuacha alicha nyumba tu.

Kuna jirani yetu yeye pamoja na mke wameeacha mtoto wao mvuta bangi nao hivi huyu alikuwa fundi wa magari alijenga bonge la jumba mke alikuwa mzuri sana.

Pia upande wa juu kwa mbele mwanajeshi mmoja yeye na mke walikuwaga na baa walipishana tu miaka ule mtaa jamani sina hamu HIV iliwapiga fasta ikaacha watoto wakijilea.

Kuna mwamba pia pale kitaa alikuwa usalama wa taifa yeye ndo alikufa yeye na mdogo wake, huyo ni hivi mdogo wake alikula mke wa kaka yake nae akapata kaka yake anavyokufa akamwambia kama uliniabia mke wangu tutaonana very soon walikuwa wote watatu na mke juu wakaacha nyumba na katoto kachanga sijui kako wapi.

Haya dada mmoja mzuri sana alikuwa alijenga kijumba chake kipya kabisa akifanya kazi halmashauri nae kufika tu mafinga uzuri ulimponza tukazika akapenda hela za mpasua mbao mmoja tajiri miaka hiyo sijui yuko wapi alikuwa mweupe handsome alikuwa akiindesha shangingi miaka hiyo.

Wadau mtaaa ni mkubwa mno ule 80% ya zile nyumba zimejengwa wajenzi wake HIV iliwabeba.

Kila siku tukawa tunazika majirani tukijua kwetu salama 2012 babangu nae sijui alitoa wapi ila nilifuatialia nasikia alipata miaka ya 90 nae tukazika, sikuwa na mahusiano mazuri na dingi hivyo hata msiba niliona normal tu nikamuuliza maza akasema si unajua mimi na baba ako tuliachana mmi mzima.

Basi miaka ikaenda hadi mwaka 2018 nilikuwa nimetoka zangu China nikaenda Iringa kumpa hi maza, mara kuingia chumbani nakuta ARV kasahau kitandani asee nililia sana nikamuuliza akaniambia samahani niliwaficha wanangu nikambatia kwa uchungu mkubwa sana siku kesho yake nikarudi Dar nikisema why why mama angu nurse nae anaondoka.

2020 akaanza kuumwa kumbe nae aliishia nao kimya kimya toka miaka 2000 mwanzoni, 2021 kuiukweli HIV/AIDS hapa ilionesha uwezo wake ilimua mama yangu kikatili mno siwezi simulia.

Basi wadau nasema kutoka moyo ule mtaa wetu 80% nyumba zimebaki za urithi tu siwezi taja mtaa ila una jina la herufi tu, kama uko mafinga utakuwa umeshaujua ni kwa kishua sana.

Research niliyofanya why UKIMWI uliua sana mafinga ni padogo pia na walio kufa sana ni wafanyakazi serikali ilikuwa ikileta wafanyakazi miaka ile ya 90 wanaambukizana sana bila kujua so wafanyakazi wengi mafinga miaka 90 kuna 2000 mwanzoni walikufa na HIV wengi ni wageni kutoka mikoa mingine including my mom.

Kuna makaburi yanaitwa MET 50% half ya marehemu pale watu wa UKIMWI wa miaka 90.

RIP To those beautiful souls, nimesimulia machache sana kuhusu mafinga na HIV, ni mengi mno nimeacha na niliyoshuhudia toka 1996.

Nilihama sijawahi kanyaga tena hata nyumba tuliuza kwa hasira maana majirani wote wamekufa now naishi Dar kama business man.

Huwa sipigi demu bila kupima pia mtumiaji mzuri wa condom.

Uzi wa leo asubuhi asanteni ila Mafinga never forget japo napapenda sana. Familia ilihamia kikazi mji ule kumbe tulienda mazikoni, kuweni makini na Mafinga wafanyakazi mnaoenda hapo, bahati yenu kumetulia ila miaka ile asee hapana.
yako
 
Ila kuna kitu kimefichwa kwenye AIDS ikitokea kwenye familia mmoja akaupata trust me lazima na wenzie aidha Wawili Au watatu watapata,ni kitu kama laana hivi but anyway naendelea na tafiti

Logic ni kwamba kuna vitu vinavyosababisha maambukizi due to sharing pasipo kujua! Dawa za meno hizi sharing nazo ni JAU ,kisu unakata kitunguu umejikata akaja naye mwingine akatumia akajikata.....Majembe ya kulima ,unalima umejikata akaja ndugu yako naye nalima anajikata ingawa ni rarely kwa maambukizi ya design hayo.
 
Sawa wapo ila sio kwamba wanaletwa vyuoni kwa lengo la kusambaza ukimwi boss

Sijasema mimi kwamba wameletwa kwa ajili ya kusambaza ,mimi nachojua kwamba kuna "WATOTO WA MAMA SALMA" vyuoni wamejaa TELE na hata ROMA alishawahi kuimba na kuwahasa wanafunzi wawe makini na "WATOTO WA MAMA SALMA" ,UDSM nakumbuka kulikuwa na FUSP na pia kuna tetesi jamaa mmoja alikuwa anasema kwamba kuna Demu ana ngoma na yeye alikuwa FUSP.(Female Undergraduate Scholarship Program).
 
Logic ni kwamba kuna vitu vinavyosababisha maambukizi due to sharing pasipo kujua! Dawa za meno hizi sharing nazo ni JAU ,kisu unakata kitunguu umejikata akaja naye mwingine akatumia akajikata.....Majembe ya kulima ,unalima umejikata akaja ndugu yako naye nalima anajikata ingawa ni rarely kwa maambukizi ya design hayo.

Yani mkuu hawa ndugu unaweza kukuta hawaishi pamoja kila mtu ana maisha yake sehemu nyingine ila sasa mmoja akipata mara na dada yake mkoa mwingine kule anao na mwingine tena hvyo yani jaribu kuchunguza
 
Back
Top Bottom