Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Usijali ndo maana watu kama sisi tupo kupeana uzoefu. Tunafundishana coz we learn from each other.Ahsante kwa kunirekebisha, mimi si mtaalam sana wa lugha.
hadithi ya mwenzako inakuuma, tunga yakoKuna maneno unaongeza sana chumvi. But pia huwezi kulia maneno hayo sijui mtetezi wangu amekufa nitatetewa na nani..... Hayo ni maneno ya ufalah. Mwanaume hawezi lia hivyo so rekebisha. Pia unapotunga angalia maneno ya kutumia na usiweke chumvi sana. Maana naona yaani unazidisha hata uhalisia. Pamoja na kuwa wasomaji wanapenda stories za uchawi. Too much is harmful.
SEHEMU YA 6
Halikuwa jambo gumu kutambua kuwa Mzee Kingalu aliuwawa kwa njia za kishirikina. Nilivyoutazama mwili wake bila shaka alikuwa amechukuliwa msukule. Muonekano wa ule mwili ulitosha kudhihirisha kwamba, marehemu alikufa kwa njia isiyo ya kawaida. Nilivaa bangili yangu ya mkononi (kikamba cheusi chenye mafundofundo), ni ile hirizi niliyokuwa nimepewa na yule mganga mkuu wa kijiji (jina kapuni) ambaye alinijuza kwamba endapo nitaivaa hiyo basi nitakuwa na uwezo wa kuona vitu ambavyo binadamu wa kawaida hawezi kuviona.
Niliivaa na kukaa kitako nikiwa nimetulia, bila kutarajia macho yangu yalifunguka, nikauona ulimwengu mwingine usio onekana kwa macho ya kawaida, viumbe wasio onekana walionekana. Kulikuwa na watu wengi zaidi ya wale walio onekana kwa macho ya kawaida wengi wao walikuwa ni misukule na wachawi. Misukule walikuwa wachafu wenye nywele ndefu na kucha ndefu wakivaa mavazi yaliyo chakaa sana, hao walionekana kwenye ulimwengu wa roho na wala sio ulimwengu wa mwili, mimi niliweza kuwaona kwa msaada wa ile bangili niliyopewa na mganga.
Kisha nikaona mzee Kingalu akiamka kutoka pale kitandani alipokuwa amelala alikuwa akiamshwa na moja ya wale vijana wa mzee Samasimba. Ni yule kijana aliyemkata jicho Sitti ile siku tulivyoenda kumuomba msamaha mzee Samasimba. Baadaye nilikuja kutambua kuwa anaitwa Mbwana, ni mtaalamu sana wa mambo ya kishirikina akiwa ndio mtendaji mkuu wa kazi za mzee Kingalu, ilikuwa ni ngumu kumuona kwa macho ya kawaida.
Mwili wa mzee Kingalu uliamka pale kitandani kuna mwingine ulibakia! Akawa ameshikwa mkono anatolewa nje huku akichechemea, watu walimshangilia sana walikuwa ni watu wasio onekana, hapo nje palikuwa na fisi aliyekuwa ameshatandwa tayari. Usafiri wa fisi hupendwa kutumiwa sana na wachawi wanasema ni usafiri wa haraka kuliko hata usafiri wa ndege. Basi yule kijana akamweka Mzee Kingalu kwa mbele na yeye akakaa kwa nyuma huku akiwa amemshikilia ili asianguke kwani kwa wakati huo yule mzee alikuwa hajitambui kabisa.
Wale watu waliondoka na kupotelea kusiko julikana nilitazama pale kitandani kwa makini, niliuona ule mwili ukiwa bado umelala pale pale kitandani lakini kwahiyo ule uliyotoka ulikuwa ni kama kivuli wala mimi sikuelewa kwa maana uliamka na kusimama lakini bado niliuona mwili mwingine palepale kitandani ukiwa umelala! Ni watu wachache tu wenye nguvu za kuona vitu visivyo onekana ndio walikuwa na uwezo wa kuona namna tukio lile lilivyo tokea.
Nilivua ile bangili kwa kuhofia kujulikana kwani muda wote nilikuwa na hofu nilipotazama wale viumbe wasio onekana. Wapo wachawi wengine hukutazama na kujaribu kukutisha kuona kama unawaona basi ukishtuka tu maisha yako utayawezka rehani, watakumaliza tu ili kuzuia usije ukawatangaza kwa watu. Nilivua ile hirizi mfano wa bangili hapo nikawa nimerudi kwenye hali yangu ya kawaida nilijiapiza kuwa sito kaa mbali na mwili wa marehemu ili nione nini kitakacho weza kutokea.
Ulifika muda wa kuosha mwili na mimi nilijitolea kuuosha mwili wa marehemu, tulichimba ufuo ndani ya nyumba ya mzee Kingalu na kumsafisha mwili kwa taratibu za dini ya kiislamu, haikupita muda nilimuona Mzee masimba akiingia ndani ya kile chumba kimiujiza kupitia pembe ya chumba. Aliingiza mkono kwenye shimo tulilochimba akachukua kitu fulani, ni kitu kilichotoka ndani ya mwili wa marehemu ilikuwa ni hirizi na hiyo ilikuwa ni muhimu katika kukamilisha kuurudisha mwili wa marehemu kwenye hali yake ya kawaida ilikuwa ni kama address code. Nilimshika mkono tuka shindana nguvu nilimtegua mguu na kufanikiwa kuipokonya kile kitu kilichotoka kwenye mwili wa marehemu sikujali kufa kwa wakati huo.
Mzee Masimba alipotea kimiujiza, "Kwanini alikuwa anataka hiki kitu?" Nilikitazama kilikuwa bado kinapumua, ni kama moyo ulivyokuwa unadunda nikakiweka mfukoni tukauandaa mwili tayari kwa kuzikwa, mimi niliaminiwa sana na hii familia ingawa nilikuwa mtu wa imani tofauti nilipewa ruhusa ya kuwa karibu ya mwili wa marehemu ikiwemo kuuosha na kuuzika tulikwenda makaburini kuuzika wanawake tuliwaacha nyumbani lakini niliporudi sikumkuta Sitti nilichanganyikiwa!
ITAENDELEA...
Umeanza🙄🙄🙄🤦🤦😀Hao walimu hukuweza kuwapiga hata picha tuwaone? Je alikuwepo wa kike? Alikuwa na shape nzuri? Story yote hii hujaweza kuweka hata picha mbili tatu ndugu mtunzi?
Mi mwenyewe sielewi ilikuwaje, wakati mwingine ni kama miujiza tu. Ahsante kwa kufuatilia.Ulivua ile bangili yenye nguvu ya kukusaidia kuona vitu visivyoonekana kwa macho ya kawaida…
Then akaingia Mzee kimiujiza ukafanikiwa kumuona na ukapambana nae asichukue kitu kilichokuwa kinapumua mithili ya moyo….
Make the story clear Chief[emoji3166][emoji3166]
Ulivua ile bangili yenye nguvu ya kukusaidia kuona vitu visivyoonekana kwa macho ya kawaida…
Then akaingia Mzee kimiujiza ukafanikiwa kumuona na ukapambana nae asichukue kitu kilichokuwa kinapumua mithili ya moyo….
Make the story clear Chief[emoji3166][emoji3166]
Duh mkuu una ujasiri sana na wachawi wanaogopa watu jasiri wasioogopa!SEHEMU YA 6