Sitosahau yaliyonipata kijijini Kwamsisi

Sitosahau yaliyonipata kijijini Kwamsisi

images - 2023-05-22T025235.726.jpg
 
SEHEMU YA 3

Mwalimu mkuu alituita kikao kilikuwa ni kikao kizito kujadili ujumbe ulioletwa na mzazi mmoja kwenye karatasi iliyokuwa imefungwa kwenye bahasha ya khaki alionekana kuwa akitetemeka na hakuwa sawa kisaikolojia, mimi nilikuwa ndio kwanza nikisahihisha madaftari huku nikibadilishana maongezi na mwalimu huyu wa kike aliyetokea kuwa karibu sana na mimi nilishtuka kumuona mwalimu mkuu akiwa kwenye hali ile.

"Walimu habari za mchana?" Tulikuwa walimu wanne wote tulitahamaki na hakuna hata mmoja aliye jibu wote tulikaa kimya. Siti akajibu, "nzuri." Sauti yake ikasikika kwa wote nasi tukarudia tena "nzuri." "Inaweza kuwa ni nzuri kwenu au la mmejibu kwa mazowea tu lakini kuna vita kali sana inayoendelea kati yetu haswa kwa nyinyi walimu wageni, inaonekana mmeshindwa kabisa kuheshimu wazee wa kijiji hiki, mzee Sa-Masimba ameleta barua hii amemtuma mwanaye ailete barua hii imenitisha kidogo kuisoma japo sijaielewa lakini ina alama ya damu.

"Alama ya damu?!" wote tulihamaki. "Ndio ni damu ya halisi kabisa ni kidoti kimewekwa juu ya bahasha kikiwa kimechovywa kama na kidole cha mkono, inaonekana kuna mtu anawindwa hapa je ni nani anayewindwa na kwanini?" alihoji mwalimu mkuu.

Barua ilisomeka, "Ndugu mwalimu mkuu hongera kwa kupata wafanyakazi wapya lakini sidhani kama vijana hao uliwafunza juu ya mila za kwetu, kuheshimu wazee na kuto jiingiza kwa namna yoyote na mipango ya kujaribu kupambana na wazee wa kimila, kama hiyo haitoshi kutengeneza wigo na kujiona kuwa huingiliki kwetu sisi tunahesabia kwamba ni dharau. Kama wameshindwa kutuheshimu japo kwa salamu mpaka kufikia hatua ya kupambana na sisi ki chwawi hakika hatuta waacha salama." ilimalizika shemu ya barua hiyo.

Nakumbuka siku hiyo tuliwaruhusu wanafunzi mapema sana ilikuwa kama mchana wa saa nane hivi. Mimi nilijua fika ndiyo mlengwa mkuu hivyo niliogopa sana tulitembea mpaka kwenye nyumba ya Mzee Samasimba tulivyo karibia tu tulipiga magoti huku tukitembea kwa magoti mpaka tulipoufikia mlango wa nyumba yake, mwalimu mkuu akiwa ametangulia mbele. Mzee mwenyewe hatuku mkuta basi wakatumwa watoto kwenda kumwita alikuja huku akiwa amevaa msuli wake kiunoni aliambatana na vijana wengine wawili mmoja alimtazama sana Siti kisha akaendelea mpaka wakaingia ndani mzee alisimama pale nje mkewe akamletea kigoda(kiti cha kukalia), akakaa kutusikiliza.

Mwalimu mkuu alikuwa ametangulia mbele aliongea naye kwa lugha ya Kizigua na mwisho aliinama sana huku akimwomba msamaha. Kwakweli nikiri wazi kwamba sikuwahi kushuhudia mchawi akiabudiwa kama siku hiyo, huyu mzee inasemekana alikuwa moja kati ya wazee wenye kauli sana pale kijijini, mambo mengi yalikwama endapo tu yeye asinge shirikishwa na kukubaliana. Ilifika zamu yangu ya kumwomba msamaha kwani tulimwendea kwa zamu, niliinama na kupiga magoti na kusema shikamoo mzee Masimba mimi ni mgeni hapa kijijini naomba unisamehe kama nilikukwaza kwa namna yoyote, sikumpa mkono kama wenzangu walivyofanya niliogopa kuchukuliwa nyota.

Tuliondoka baada ya kupakwa usembe(unga mweupe) usoni na kichwani na wale vijana wake, tulidhalilishwa sana siku hiyo hamna siku nilichukia kazi hii ya ualimu kama siku hiyo tulirudi nyumbani kila mtu akiwa kimya hamsemeshi mwenzake, nilitembea huku nikiwa na mawazo mengi macho yangu yakitazama chini huku machozi yakinilengelenga. "Kwanini binadamu anaabudiwa kama Mungu!" niliwaza moyoni ilikuwa yapata majira ya saa kumi nambili jioni ikikaribia saa moja usiku, nilishtuka kumuona Siti akiwa amenishika bega la kulia kwa nyuma niligeuka na kumtazama.

"Kwahiyo ndio unaenda nyumbani, uende salama ila uwe makini, hapa ndio Kwamsisi uache ubrazameni uheshimu watu." Kumbe ile hali yangu ya kujitengetenga na kutosalimia watu iliwaudhi wengi pia kujiweka karibu na mzee Kingalu ilikuwa ni hatari kwangu niliogopa kuiendea ile njia inayokwenda nyumbani, nilipokumbuka lile jicho alilonikata mzee Masimba nilipogoma kumpa mkono wa msamaha kwa kuwa sikutaka kushikana mkono na mchawi. Basi nikajua kuwa usiku huo lazima atanijilia nyumbani kwangu.

ITAENDELEA...
Ushauri ongezea maneno ya kutosha story n fupi fupi kutoka muendelezo mmoja kwenda me mwingine....ila ipo vzr stori yako mkuu
 
Back
Top Bottom