Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
[emoji23]Usikute KWAMSISI ndo nyumbani Kwa Shetani
Kwamsisi itakua jirani na Chato.Usikute KWAMSISI ndo nyumbani Kwa Shetani
Alikuwa kwa RMOMUENDELEZO SEHEMU YA 2
"Ngo ngo ngo!" Mlango wa nyumba yangu ulikuwa ukigongwa. "Ni nani mwenzangu?" niliuliza. "Ni mimi mzee Kingalu nina shida na wewe mara moja!" Nilitoka na kushangaa kwa nje kulikuwa na mwanga mkali sana wa jua, kumbe ilikuwa ni saa nne asubuhi, nimechelewa kazini isivyo kawaida yangu. Mzee Kingalu alikuwa ameongozana na mwenyekiti wa Kijiji, niliwasalimia huku nikionyesha wasiwasi mkubwa, wala hawakujibu salamu hiyo walinidakisha kwa maneno.
"Kijana wewe ni mwalimu wetu na umeletwa ili uwasaidie watoto wetu kielimu, hatuwezi kuvumilia watu wachache wasio kuwa na nia njema waweze kukukatisha tamaa na kukuharibia maisha yako ya sasa na ya baadaye, tumepata taarifa kuwa ile kinga tuliyokupa imeporwa, je kuna ukweli gani kwenye hili?"
Wamewezaje kufahamu kwamba ile kinga imeporwa ijapokuwa sikuwaambia, niliwaza moyoni. "Ndio!" Nilijibu na nikawaelezea kuhusu ile ndoto niliyoiota usiku wa jana kuamkia siku hii ya leo.
"Ndio swala hilo tunalijua, kuna wazee walikuja kwako usiku huu kwa lengo la kukudhuru sisi tulifanya juhudi kubwa kuwazuia na ndio maana tupo hapa saa hii kwa sababu hatupendi kukukosa," alimalizia mzee Kingalu kisha kuingiza mkono wake kwenye mkoba mweusi aliokuja nao na kutoa kichupa cheusi. Alinipa kichupa cheusi chenye mafuta yaliyochanganywa na mavumba fulani, mafuta hayo yalikuwa ni mafuta ya mbarika na mavumba ni majivu ya mchanganyiko wa vingira fulani vya kichawi. alinishauri niwe napaka utosini kila usiku ninapotaka kulala.
Nilijiandaa haraka na kuelekea shuleni nilipofika wala hakuna mtu yeyote aliyeniuliza kitu chochote ama kushangazwa na kuchelewa kwangu kazini kwa sababu ilikuwa ni jambo la kawaida kwa wafanyakazi kuchelewa, mimi sikutaka kujiingiza kwenye mkumbo huo ni siku hii tu nilichelewa bila hata mwenyewe kutarajia.
Mwalimu mwenzangu wa kike aliyeitwa Siti ndiye pekee aliyenihoji na nilimpa jibu moja tu la mkato kwamba aniache kidogo kwani kichwa changu hakipo sawa kwa wakati ule, nashukuru alinielewa. Alinitia moyo sana binti yule, alikuwa ndiye rafiki yangu kwa wakati ule kwani hata ki umri tulikuwa hatujapishana sana tofauti na walimu wengine waliokuwa ni watu wazima kutuzidi sisi. "Soka wewe ni mtoto wa kiume, hapa kijijini umekuja kikazi japo ninakuonea huruma lakini huna budi kujifunga mkanda."
Nilimsikiliza na kuwaza moyoni, mbona haya maswahibu mwenzangu hayampati? Baadaye nilikuja kugundua kuwa yeye mahali napoishi ni nyumba ya Mganga mkuu wa kienyeji pale kijijini, na alikabidhiwa pale na baba yake mzazi kwahiyo wachawi wengi wa pale kijijini Kwamsisi walikuwa wakiogopa kumfanya chochote.
ITAENDELEA...
Kuna maneno unaongeza sana chumvi. But pia huwezi kulia maneno hayo sijui mtetezi wangu amekufa nitatetewa na nani..... Hayo ni maneno ya ufalah. Mwanaume hawezi lia hivyo so rekebisha. Pia unapotunga angalia maneno ya kutumia na usiweke chumvi sana. Maana naona yaani unazidisha hata uhalisia. Pamoja na kuwa wasomaji wanapenda stories za uchawi. Too much is harmful.SEHEMU YA 5
Ilikuwa ni siku ya Ijumaa kama ilivyo ada niliamka asubuhi sana kwa msaada wa kengele ya simu yangu. Nilijiandaa tayari kwa ajili ya kuingia kazini, sikutaka kuchelewa kama ilivyokuwa siku iliyopita. Nilifika shuleni majira ya saa kuminambili na ushee nilikuwa mtu wa kwanza kufika pale shuleni, sikuwakuta watoto bado kulikuwa na kigiza cha asubuhi. Nilishangazwa na nilicho kikuta, mwalimu mkuu wa shule akiwa pamoja na walimu wengine wawili (jumla walikuwa walimu watatu) walikuwa wamelala katika kiwanja cha mstarini huku wakiwa wapo uchi wa mnyama mimi niliwashuhudia, isingekuwa mimi kuwahi basi huwenda wangeaibika sana mbele ya wanafunzi wote. Ni mimi na Sitti pekee ndio tuliosalimika, ijapo tulikuwa wageni lakini tulishakuwa makonkodi haswa wagumu kuingilika!
Niliwashtua walimu wenzangu waliokuwa wamelala huku wakiwa wamenyolewa kidogo kichwani. Wachawi walichukua kiasi kidogo cha nywele zao, walikurupuka na kushtuka sana walipoona kumbe wamelazwa kwenye mazingira yale ya shule wakaanza kutimua mbio kila mtu na njia yake, inaonekana ule msamaha tulioutoa jana haukutosha kumfanya mzee Samasimba kutusamehe kabisa. Maana kwa picha hii niliyoiona bila shaka yule mzee atakuwa anahusika kwa zaidi ya asilimia mia moja.
Baada ya muda wanafunzi wachache walikuwa wakiingia shuleni, baadhi ya wanafunzi ni watoto wa wachawi pia kwahiyo michezo yote waliyokuwa wakituchezea walikuwa wakiijua. Walikuwa wakishirikiana na wazazi wao kutuchezea michezo hiyo, japo nikiri kwamba tangu nilivyo ripoti katika shule hii sikuwahi kushuhudia sana watoto wakichapwa kwasababu ilikuwa ukimchapa mtoto wa mtu basi utaingia kwenye matatizo makubwa na jamii ya wazazi wao.
Kuna hadithi kwamba yupo mwalimu mmoja alikuwa akiwachapa sana wanafunzi hapo kwanza naye alikiona cha mtema kuni (alizinyonyoa nywele zake kisha akazila!) Baada ya tukio hilo fimbo kwa watoto imekuwa historia hapo shuleni, ijapo mimi hushika kwa lengo la kuwatishia tu. Wengi wetu tunakomaa na ule usemi wa ukinisikiliza usipo nisikiliza haunipunguzii mshahara wangu! Tulifanya kazi tu kutimiza wajibu.
Kwahiyo watoto wengine walijua kinacho endelea na walifika mapema ili kuhakikisha kama wale walimu bado wamelala pale ili wawaaibishe kwa kupiga kelele kuwaita wanafunzi wenzao, lakini haikuwa hivyo, walivyofika walinikuta mimi nikiwa nimefura kwa hasira. niliwahesabia namba na haraka haraka kila mwanafunzi alipewa eneo lake la kufanya usafi, ninauhakika kuwa leo lazima wapeleke ripoti kwa wazazi wao na hii inaweza kuongeza chuki dhidi yangu.
Wale walimu wenzangu walianza kuingia kazini mmoja mmoja na mpaka walipofika wote walikuwa wamechoka sana, ilionekana kama walifanyishwa shughuli kubwa jana yake, nyingi huwa ni za mashambani ama za kubebeshwa vitu vizito, na unafanya bila kujitambua unakuwa kama ndondocha kwa muda mfupi, wachawi wana mambo sana!! Tulianza kufundisha nakufikia saanne muda wa mapumziko tulisika ngoma ikipigwa kwa sauti dum dum dum...! Hii ni sauti ya hatari ni lazima ikitokea hivi kuna tukio kubwa limetokea, ngoma iliendelea kupigwa na mara kijana aliyetumwa kuja shuleni kutoka ofisi za kijiji alifika akiwa anahema sana.
Nimetumwa na mwenyekiti kwamba kunamsiba umetokea huko Mahameni! Mahameni ulikuwa ni mji wa zamani ambapo wanakijiji walihama enzi za vijiji vya ujamaa na kutengeneza kijiji cha Kwamsisi lakini walikuwepo baadhi ya watu waliokuwa wakiendelea kuishi huko. Mzee Kingalu amefariki kwa kuangukiwa na ukuta wa nyumba yake. "Unasema?!" niling'aka kwa mshtuko. "Ndio hivyo, kwahiyo mwalimu mkuu atume wawakilishi." Niliangua kilio cha kwikwi. "Haiwezekani nasema haiwezekani wamemuuwa mzee wetu." Nilikuwa na uchungu mkubwa, kati ya wazee wengi wa pale kijijini ni huyu tu ndiye niliyeelewana naye alikuwa mzee mpenda maendeleo alijitoa kunisaidia kwa hali na mali.
"Pole sana Soka, tunauelewa ukaribu wako na mzee Kingalu huna budi kuukaza moyo," walimu wenzangu walizidi kunipa moyo akiwemo Sitti aliyekuwa habanduki pembeni yangu. "Ninawapa ruhusa nyinyi wawili ili muende kutuwakilisha kwenye msiba huu," tulitoka tukiwa tunatembea haraka haraka kuelekea kitongoji cha Mahameni hapakuwa mbali kutoka eneo la shule, ni mwendo kama wa nusu saa kwa kutembea kwa miguu. Kijiji chote kilizizima, mzee Kingalu alikuwa ni moja ya wazee walioheshimika sana pale kijijini, ingawa alikuwa pia na uchawi wa kurithi, kwani uchawi ni kama mila kwenye jamii ya wazigua, alirithi mkoba huu kutoka kwa mababu zake.
Tulifika na hapo Sitti akaanza kuangusha kilio si unajua wanawake tena mimi nilijikaza kisabuni. Watu walikuwa ni wengi wakiimba nyimbo za maombolezo hata wale wachawi nilio waona jana usiku wakipanga mikakati dhidi yangu na mzee Kingalu nao niliwaona wakibubujikwa na machozi. Tuliingia moja kwa moja kwenye ile nyumba ya Msonge iliyokuwa na msiba. Niliingia ndani na kumkuta Wana-Kingalu (Mkewe) akiwa na huzuni nyingi nilimpa pole naye akanikumbatia kwa huzuni, alikuwa ni bibi mtu mzima. Niliingia chumbani kuutazama mwili wa mzee, "nyumba aliyoangukiwa na ukuta ndio ile pale alikuwa amejipumzisha kitandani." nilionyeshwa nyumba nyingine kwenye boma ya ukoo wake.
niliingia kwenda kuutazama mwili wa marehemu, walikuwa wamemlaza kwenye kitanda cha supatu (kamba za kusukwa na minyaa), mwili haukuwa na majeraha kabisa ingawa ulikuwa ukivuja damu puani na mdomoni na ulikuwa umevimba kiasi. Hapo nilishindwa kujizuia nikaangua kilio. "Mtetezi wangu sasa hayupo nitawezaje kuishi kwenye hichi kijiji kilichojaa vitimbi na mauzauza ya kila aina?!"
Walinichukua na kunisogeza pembeni nilimuona Sitti akiwa amekaa sehemu tofauti akijumuika na wanawake wenzake. Kinacho fuata ni mwili kuoshwa na kisha kuzikwa kwa taratibu zote za dini ya kiislamu. Usishangae mchawi kuzikwa kidini kwani hawa wachawi huwa wanajivika sura ya udini uliokubuhu na lengo kuu ni ili wasiweze kushtukiwa ama kuhisiwa kama ni watu wabaya. Mfano Mzee Masimba alikuwa ni mtu wa swala tano akiwa pia ni mmoja wa viongozi wa msikiti mkuu wa Kwamsisi.
ITAENDELEA...
(Usiache kutoa maoni.)
U re too critical the story is realKuna maneno unaongeza sana chumvi. But pia huwezi kulia maneno hayo sijui mtetezi wangu amekufa nitatetewa na nani..... Hayo ni maneno ya ufalah. Mwanaume hawezi lia hivyo so rekebisha. Pia unapotunga angalia maneno ya kutumia na usiweke chumvi sana. Maana naona yaani unazidisha hata uhalisia. Pamoja na kuwa wasomaji wanapenda stories za uchawi. Too much is harmful.
Achana watu kama haoU re too critical the story is real
Ohooooooooo chap chap, asanteeeGari lishatoka, chukua boda uliwahi mzani.
Usiporejea ntakukutukana kila siku!
Mim nlienda kumzoa mume wangu huko kwa msisi eneo linaitwa BICHWA NG'OMBE alikaa miezi miwili hajarejea alifuata mbao.
Nikamkuta anaishi na kibibi kuliko mama yake.
Ishukuriwe damu ya YESU
Asante mwaya😍