Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Siyo kenge wa kitoto, yaani ni kenge msenge [emoji23][emoji23]Naungana na hawa jamaa huyu ni kenge
[emoji1787][emoji1787]Naungana na hawa jamaa huyu ni kenge
KaishiwaItakua uongo,katunga stori.
Hatari sanaSEHEMU YA 4
"Sitti sikuachi tuondoke wote." "Hapana kwanini unanifuata unadhani kwamba mzee atanielewa?" Mzee akimaanisha yule mganga mkuu anayekaa naye pale nyumbani, mueleze matatizo yangu huwenda akanisaidia. "Unadhani basi ninaimani sana na mambo haya ya kishirikina?" Sitti alijifanya kwamba hana imani sana na waganga lakini mimi moyoni mwangu nilijua fika kwamba yeye anaweza kunisaidia juu ya jambo hili kwa hivyo nilikata shauri la kumfuata mpaka pale alipokuwa akiishi. Kagiza ndio kalikuwa kakianza kuingia na unavyojuwa hali kijijini giza linawahi kuingia haraka na usiku huwa ni mrefu na wa kutisha mno.
Nilimshika Sitti mkono mpaka pale alipokuwa akiishi tulifika ilibidi aniache nje kwanza barazani ili aende akaongee na yule Mzee Mganga. Ni mganga aliyekuwa maarufu sana hapo kijijini sito mtaja kwa jina ili kuficha hadhi yake lakini kila siku hayakuacha kupaki magari yasiyopungua matano ya wateja waliokuwa wakihitaji huduma yake, nilifika nikasikia kuna mteja alikuwa akimalizia kumtibu niliketi barazani kwenye benchi na mara kidogo niliitwa na kuingia ndani, Siti alinitambulisha na baada ya utambulisho niliona yule mganga akitazama kwenye kioo chake na kisha baadaye akaongea kwa upole.
"Kuna watu wanakufuatilia, na hata hapa ulipo wapo mimi nimewaona?" "Wako wangapi?!" niling'aka kwa mshtuko. wapo wawili nilihisi huwenda kuwa ni wale vijana wa mzee Samasimba ndio wametumwa kunifuatilia, ni kweli Mganga alinieleza kuwa hao vijana wametumwa na mzee fulani ambaye hato mtaja jina na lengo lao ni kuangalia nyendo zangu na kisha kumpelekea yule mchawi taarifa. "Wewe huwezi kuwaona kwasababu huna nguvu za kuwaona," alisema kwa upole na kwa utulivu mno.
Nilikuwa nipo ndani kwenye chumba maalum cha uganga, koroboi iliyokuwa hapo chumbani ndiyo iliyokuwa ikitoa mwanga kwa wakati ule. Chumba kilitapakaa harufu ya udi ambapo mganga alikuwa ndio kwanza anaanza kupandisha maruhani yake alisimama akaanza kutetemeka mwili mzima mithili ya mtu aliyepigwa na shoti ya umeme. "Enyi wazee na mizimu ya wakulu njooni mumuokoe huyu m'bwanga, asije kudhulika na walimwengu wenye roho mbaya. aliongea kwa sauti kali sana kisha kuchukua tunguli yake akiisha kuitikisa sana akaipuliza na hapo ikatokea sauti kama ya filimbi. Aliizungusha kichwani kwangu na kuniwekea kichwani kwa dakika kadhaa kisha kuitoa na kuivaa shingoni kwani ilikuwa na ukamba wake.
Huyo mganga alikuwa amejifunga kaniki kwa mtindo wa lubega tu na kiunoni alifunga mkanda wa shanga za makombe ya baharini. Chumba chake kilijaa zana za kazi basi alichukua kikamba kama bangili yenye mafundofundo akanifunga mkononi ilikuwa ni kama hirizi ndogo, kisha akanipaka dawa kidogo kutoka kwenye ile tunguli na kunishika mkono kutoka nje huku akiwa ameshikilia pembe ndefu pamoja na mwengo (kama mkia wa ng'ombe) alizunguka nyumba mara nyingi huku akiimba na kisha akaniambia nimfuate nyuma twende nyumbani kwangu kuzuza. (kukagua usalama wa nyumba yangu).
Nilimfuata nyuma alikuwa akikimbia kwa kasi japo sio sana, niseme tu labda ni kile kihirizi alicho nifunga ama ile dawa aliyonipaka usoni kwani kuanzia hapo nilianza kuona mambo ya ajabu mno na yakutisha. Niliweza kuona mwanga kama vile kuna taa za umeme kijiji chote pia mandhari ya kijiji ilibadilika ikawa ni yakuvutia mno ni kama vile macho yangu yalipigwa kiini macho. Niliwaona watu wakiwa katika maumbo ya ajabu ajabu wengine wakitembea huku wakiwa uchi wa mnyama!
Kila tulikopita niliona vitu ambavyo nisingeweza kuviona kwa macho ya kawaida wale vijana walikuwa wakitufuatilia kwa nyuma baada ya muda sikuwaona tena. Tulitembea usiku na baadaye kuingia kwenye njia ya kuelekea mashambani ni njia ya mkato kuelekea nyumbani kwangu lakini njia hii hupitia kwenye makaburi ya kijiji. Ghafla nilimuona yule mganga akipunguza mwendo na hapo akatembea kwa mwendo wa kunyata, alinisubiri mimi nilikuwa nyuma nikimfuata, jasho lilikuwa limenitoka mpaka kulowesha nguo yangu ya ndani, niliingiwa na woga mkubwa. Alinishika mkono tukatembea kidogo kuyakaribia makaburi tukachuchumaa chini ya mbuyu, nilistaajabu nilicho kiona.
Mwanga mkali wa moto uliokuwa umekokwa hapo makaburini wachawi walikuwa wakicheza kwa furaha huku wakiuzunguka moto ule. Mara nikamuona Mzee Samasimba akija huku akiwa amepanda juu ya mnyama fisi, wote walitulia kumsikiliza, niliwaona pia wale vijana waliokuwa wakitufuatilia wakiwa pamoja naye. Aliongea mengi ambayo sikuyasikia kwani alitumia lugha ya asili (kizigua) mwisho nilisikia jina langu na la Mzee Kingalu yakitajwa mara nyingi sana sikuelewa lugha iliyokuwa ikitumika nilimuona yule Mzee akilia sana huku akiongea kwa uchungu. Ijapokuwa alikuwa akiheshimika na wachawi wenzake lakini safari hii ilionekana kama aliudhika mno.
Wachawi hawana kazi, maranyingi hutafuta visababu tu ili kuanzisha ugomvi, ni watu wanaopenda kuheshimiwa na kuabudiwa kama Mungu bila kujua kwamba hapa duniani tunapita tu. Ndivyo ilivyokuwa kwa jamii ile niliyo kutana nayo amahakika nilijuta sana kuifahamu jamii ile na tamaduni zake. "Hapa ndipo sherehe na vikao vya kichawi hufanyika, inaonekana leo hawatokula nyama ya mtu ila kuna mtu wanamtafutia sababu, ni ama wewe au mzee Kingalu lakini mwenzako ni gwiji wa mambo haya wewe pangupakavu tia mchuzi watakuramba kama karata!" alisema yule mganga kwa sauti ya kunong'ona mwisho aliniambia tuondoke tunaondokaje aliniambia nimshike upindo wa ile kaniki na mara tukatokea mbele ya nyumba yangu.
"Kwa leo hatutoweza kufanya hili zoezi, lala kesho ukitoka kazini upitie nyumbani." Akimaanisha zoezi la kukagua nyumba na kuizindika, sikumjibu nilielekea mlangoni kwangu, niliufungua mlango na kuingia ndani kisha kuwasha kibatari nilipakaa ile dawa niliyopewa jana na mzee Kingalu utosini ilinisaidia kuzuia nguvu za kichawi, lakini ile hirizi niliyopewa na Mganga wala sikuivua. Nilizima kibatari na kulala ilikuwa yapata majira ya saa sita usiku. Niliomba pakuche haraka ili niwe salama. Sikusikia tatizo lolote kwa usiku huu ila baadaye nilisikia sauti ya bundi akilia juu ya bati langu alilia sana mpaka nikapitiwa na usingizi nilimsikia akilia kwa mbali na kupotea.
ITAENDELEA...
Sitosahau yaliyonipata kijijini Kwamsisi-5
Hahaaa, hata mi sikuwa najua kama inaendelea.1.Simulizi uchwara watu wameikimbia
2.Hakuna hata mtu mmoja aliyekufata pm
3.Wewe ni zezeta
4.Simulizi zako utakuwa unasoma mwenyewe na ukoo wenu lakini hapa JF ushaula wa chuya
5.Kama ulitegema hapa JF upige pesa badala yake unajikuta umeula wa chuya
6.Wewe ni zumbukuku
Hiki kipande cha mwisho kama vile kimezidi sukari
Anayeroga ni huyo huyo....asiwachafue wengineKuna watu ni wabishi sana,Kuna mwanafamilia kwetu ni mchngaji lakini ana mganga wake anaemtibu na kumuweka sawa,ananambiaga dada hakuna watu tunarogwa kama wachungaji,kwaio msibishe sana jamani,ushirikina upo,na sio kila anaemtaja Mungu kasimama na imani,wengine kanisanin na misikitini ni sehemu ya kutafuta ridhki tu kama wewe inavyoamka kwenda kibaruani
....SEHEMU YA 10
"Haiwezi kuwa kirahisi huyu kijana ametuingilia vya kutosha sasa haina budi tumfanyizie!" Mzee Samasimba na vijana wake Mbwana na Jumanne waliketi kwenye kikao kizito wakinijadili mimi. Hao vijana walikuwa wakiogopwa sana pale kijijini, mabingwa wa kuroga kuanzia zongo mpaka kutupiana mashakizi. Mashakizi ni majini yanayotumwa kukusababishia kifo kisichotarajiwa, mfano unaweza kupata ajali ya basi ukafa kumbe sababu ni za kichawi na hii inatokana na mashakizi utakayo tumiwa.
Taarifa za vikao vyao nilizipata kwakuwa nilikuwa nikioteshwa kila kitu walichokifanya niliona mchezo mzima na hapo nikapanga namna ya kujiokoa. Siku hii usiku niliota ndoto ya kutisha, nimesafiri kwenda mjini Tanga kikazi wakati wa chakula watu wengi tulikuwa tumekaa pembezoni ya maegesho ya magari ya mizigo, lilikuwepo lori la mizigo lililokuwa limepaki hapo kwahiyo sisi tulikuwa tumekaa kwa pembeni yake kufumba na kufumbua niliona lile kontena likichomoka na kutuangukia na kutufunika watu wote tuliokuwepo mahali pale, nilishtuka kutoka ndotoni.
Ni ndoto ambayo ilinisumbua sana ingawa sikumwambia mtu yeyote na baada ya wiki nilipokea barua ya mwaliko wa kuhudhuria semina ya walimu wa masomo ya sayansi katika jiji la Tanga na kweli nilipofika niliyaona mazingira kama yale niliona lori la mizigo likiwa limeegeshwa sehemu ambayo waalimu walikuwa wakigawiwa chakula, nilihisi kitu hakiko sawa nami sikusogelea kabisa eneo hilo mara baada ya kuchukua chakula nilikaa mbali ya eneo hilo huku nikishuhudia jambo litakaloweza kutokea.
Kufumba na kufumbua niliona lile kontena likianguka kwa haraka na kuwafunika walimu wote waliokuwapo pale kwa chini wengi walijeruhiwa na baadhi yao kupoteza maisha niliogopa sana nikamshukuru Mungu kwa kuniepusha na jambo hilo. Baada ya tukio hilo nilishangaa nilipopigiwa simu na watu ninaowafahamu kutoka kule kijijini wakiniambia kwamba taarifa zimesambaa kuwa mimi ni mmoja wa walimu waliofariki kwenye ajali hiyo, nilishangaa! Baada ya kufanya uchunguzi niliambiwa watu waliokuwa wakisambaza taarifa hiyo hawakuwa wengine bali ni wale vijana wa mzee Samasimba Jumanne na Mbwana.
Nilirudi nikafika kijijini usiku. Sitti alikuwa na kawaida ya kuja kunipokea pindi nitokapo nje ya mji na siku hii nilimletea zawadi aliyokuwa akiipenda, lotion ya Swetheart pamoja na perfume ya Kulthum. Nilitembea mpaka nyumbani kwangu na kuingia ndani, nilisikia miguno ya kimapenzi ikitokea ndani ya nyumba yangu."Kuna nini tena humu?!" Nilishtuka kwasababu funguo za nyumba yangu nilimkabidhi Sitti nilivyo ondoka kwenda mjini Tanga. Niliporudi sikuona umuhimu wa kumjulisha kwamba ninarudi nilitembea taratibu mpaka nyumbani kwangu na baada ya kusikia sauti hizo nilichungulia kupitia dirishani, kuna mambo ya kiutu uzima yalikuwa yakiendelea chumbani kwangu.
Sitaki kuamini kile nilicho kishuhudia usiku ule, ilikuwa ni kweli na wala haikuwa ndoto kama nilivyotaraji iwe. Sitti alikuwa akivunja amri ya sitta na Mbwana tena mbaya zaidi alikuwa akifanya kitendo hicho ndani ya nyumba yangu kwenye kitanda changu. Niligonga mlango kwa nguvu wala hawakufungua, nikaufungua kwa funguo za akiba nilizokuwa nazo. "Lahaula lakwata!" Niliwakuta wakiwa kama walivyo zaliwa wakivunja amri ya sita juu ya kitanda changu. "Sitti ni wewe ama ninaota!" Walishtuka, "Hee Soka, ni wewe ama ni mzimu wako?!" wote wakawa wakinitazama.
"Nilijua umesha fariki kwenye ajali kumbe bado u mzima!" Walikukuruka wakashindwa kuachiana nilichukua fimbo nikawatandika haswa nilimtandika zaidi Mbwana kwasababu nilikuwa na hasira naye lakini alijaribu kukukuruka hakuweza kutoka kwani nilikuwa nimezindika kichawi. Baada ya kuwapa kipigo hevi na kuridhika ndipo nilichomoa kisu kwenye ala niliyokuwa nimeificha kwenye kona ya chumba changu basi wakaachiana. Sikutaka kuwaona kabisa mbele ya macho yangu, niliwafukuza. Pamoja na uchawi wake wote, Mbwana alikuwa mdogo kama piritoni kwasababu ukifumaniwa huwezi kuwa na nguvu zozote, hata kama ukiwa na nguvu za kichawi unashindwa kuzitumia ili kujitetea.
Japo nilimpenda Sitti na kujitesa kwa ajili yake lakini nilikuja kuamini kwamba wanawake sio watu wa kuwawekea mdhamana. "Sitti nilimuamini mpaka kudiriki kumuachia funguo ya nyumba yangu lakini leo hii ameamua kunifanyia usaliti wa wazi kabisa," nilijisemea mwenyewe kwani niliumia sana moyoni. Sikutaka kumwambia mtu yeyote juu ya jambo hili nilijua itakuwa aibu kubwa ila akilini niliapa kulipa kisasi.
Siku hiyo sikulala kitandani nilikuwa nimekaa pale nje kwenye kizingiti nikiwaza sana mpaka usingizi uliponipitia na cha ajabu nilishtuka usingizini nikiwa nimelala kitandani kwangu milango yote ikiwa imefungwa. Nilishtuka kusikia harufu kali ya marashi ikiwa imesambaa kwenye kile chumba na hapo nikamuona mwanamke mrembo mweupe pe' na mwenye nywele ndefu zilizofika mpaka kwenye kiuno chake na alikuwa na macho maangavu yaliyoingia ndani.
Alikuwa amesimama mbele yangu akinitazama huku yupo uchi wa mnyama. "Ondoka kwangu kaa mbali na mimi, kwani wewe ni nani nilimhoji!" "Naitwa Maimuna nimetoka kwenye kina kirefu cha bahari nimekupenda sana jinsi ulivyo na pia nimependa ujasiri wako, nilimtazama mwanamke yule kuanzia juu mpaka chini nilistaajabu nilipoziona kwato zake mithili ya farasi zikiwa zimechomoka kwenye miguu yake nikapatwa na kigugumizi.
Yule kiumbe akaondoka, nilimtazama akitembea vishindo vya viatu virefu vilisikika vikipotelea mbali ya upeo wa akili yangu na sauti ya mlango ukafungwa kwa kishindo kikuu! Nilishtuka kwenye ndoto ile na jasho jingi lilikuwa limenitoka mpaka kulowesha mashuka, nikweli nilikuwa nimelala kitandani kwangu na milango yote ikiwa imefungwa sikuelewa kivipi yule kiumbe alipita mpaka kuweza kuingia na kutoka ndani ya nyumba yangu. Baadaye nilikuja kutambua kuwa majini ni viumbe wenye uwezo mkubwa wa kuweza kupenya ama kupita kwenye maeneo yenye vizuizi vya kila aina kwa sababu kikawaida viumbe hawa hawana mwili wa kibinadamu na huweza kuvaa umbo na mwili wa kiumbe chochote kile wakitakacho.
ITAENDELEA...
Sitosahau yaliyonipata kijijini Kwamsisi-11