Extrovert
JF-Expert Member
- Feb 29, 2016
- 70,785
- 186,690
Sitaki kumfata Membe bwanaSasa mkuu kwanini usifuatilie utajiri huo wa mzee? Au unaogopa kuchimbua?🤣🤣
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Sitaki kumfata Membe bwanaSasa mkuu kwanini usifuatilie utajiri huo wa mzee? Au unaogopa kuchimbua?🤣🤣
Ukihitaji story zangu nifuate PM nitakuletea ama kukutumia popote ulipo.
Umequote kutoka wapi hii?Tahadhali
Mwandishi huyu ni mhuni siyo mwandishi Bali no mhuni ambae anauza kazi za watu Mimi kanipa listi ya riwaya alizoandika kumbe zote nishazisoma ni riwaya za akina Patrick CK zuki gadu pamoja na wakina Daniel mwaseba ambazo zote nishazisoma hivo muwe makini anauza riwaya za watu siyo zake
Wewe ni tapeli na tunakuchukulia hatua uondolewe humu ndani... unataka kujifaidisha na kazi za watu wengine. Hii aikubaliki .Umequote kutoka wapi hii?
Acha uhuni na kuuza kazi za watuUmequote kutoka wapi hii?
Reputable ya konyo umewahi kuandika jambo gan zur humuUmekosa kazi, na rafiki yako chizi maarifa. I am reputable and known writer of JF.
Mambo mazitoSEHEMU YA 7
Niliporudi kutoka kwenye kuupumzisha mwili sikumkuta Sitti pale alipokuwa amekaa. Nilijaribu kumuulizia ila kila niliyemuuliza alisema hajawahi kuona mtu kama huyo, kwani niliwalezea kwa jinsi alivyokuwa amevaa na kwa jinsi alivyokuwa akionekana, walibaki kunishangaa tu niliogopa kurudi nyumbani bila yeye nilikaa pale msibani mpaka watu wote wakamalizika kuondoka. Nami nikakata shauri la kuondoka eneo lile la tukio nilipokuwa nikiondoka nilisikia sauti ya mtu akiniita kwa jina langu ilikuwa ni sauti ya wana Kingalu. "Mwanangu Soka!" niligeuka nikamfuata.
Nilimtazama mwanamama huyu aliyekuwa amesha zeeka haswa ngozi yake iliyokunjamana na sura yake kukosa nuru. "Bila shaka unamtafuta rafiki yako Sitti?" aliniuliza. "Umejuaje mama, ni kweli namtafuta kwa maana ninajua asingeweza kuondoka bila ya kuniaga." "Unaikumbuka hii?" ananionyesha khanga aliyokuwa amejitanda. "Imeokotwa huko mtoni walipokwenda kuteka maji." (ni kawaida kwa wanawake kushiriki kazi kwenye eneo la msiba), "Kuna watu wameiokota," kisha alinikabidhi niliichukua ile khanga kuna fundo lilifungwa nikalifungua nikakutana na kikaratasi chakavu kimeandikwa.
"Kwako Mwalimu Soka, ukipokea barua hii utambue kuwa rafiki yako Sitti yupo kwenye mikono salama, lakini uhai wake uko mikononi mwako, endapo tu utatuletea ile hirizi ya Simba, tuna kupa sikumbili za kusubiri, ukishindwa kufanya hivyo uhai wa huyu binti utakuwa mashakani, ni mimi Mbwana." ilimaliza sehemu ya barua hiyo.
Yule kijana alikuwa na dawa ya kupumbaza wasichana awatakao, dawa huitwa ndele. Humsogelea msichana akiwa amepaka mafuta yake ya mvuto usoni, humpiga na kifimbo chake kidogo utosini na yule msichana humfuata mwenyewe popote aendapo, nahisi alitumia mbinu hii kumuiba Sitti.
"Hirizi ya Simba?!" nilishtuka nikaingiza mkono mfukoni kujipapasa na kuitoa kile kitu nilichokitoa kwenye mwili wa marehemu wakati wa kumuosha na kisha nikakitazama kwa sekunde kadhaa, bado kilikuwa kina pumua. "Bila shaka hii ndio yenyewe na kwanini hasa wanaitaka?" Nilikuja kugundua kwamba hirizi ya Simba ni moja kati ya mazindiko makubwa sana ya wachawi pia hutumika na viongozi wakubwa wa serikalini ili kuwafanya waogopwe na kila mtu, pia ukiwa nayo hii ni kinga dhidi ya wachawi.
Kumbe ndio maana mzee Kingalu alikuwa akiogopwa na kuheshimiwa na kila mtu na ndio maana kwenye msiba wake ilipigwa ngoma, sikila mtu akifa hupigwa ngoma ni kwa watu wachache wenye hadhi fulani na heshima fulani mbele ya jamii. Kwahiyo Mzee Kingalu alikuwa na kauli ya mwisho juu ya maamuzi yoyote pale Kijijini, labda hii ilitokana na kumiliki hirizi hii ya simba. Niliondoka kuelekea nyumbani kwangu huku macho yakiwa yanatazama chini niliichukua ile khanga ya Sitti nikaizungusha shingoni, ile barua niliifunga palepale ilipokuwa.
Nilifika nyumbani saa moja kasorobo hivi usiku niliwakuta walimu wenzangu wakinisubiri kwa hofu, nilivyo waona wamekaa pale nje kibarazani nilikaza mwendo kuwawahi kwani niliona kama nachelewa kuwafikia, nilifika nikaanza kulia niliwaeleza yote yaliyotokea na jinsi Sitti alivyopotea kimiujiza tulijadiliana kila mtu alitoa wazo lake, wapo waliosema kwamba tupige simu wilayani ili watume polisi kuja kuwakamata wahusika wote lakini wazo hili lilipingwa vikali na mwalimu mkuu.
Inaonekana kama aliogopa kibarua chake kuota nyasi ama labda aliwaogopa wazee wa Kwamsisi, kufanya jambo lolote bila kuwahusisha wao ni kujihatarishia maisha yako nilimwachia mwalimu mkuu ile khanga yenye ile barua mimi nikaingia ndani ili kujipumzisha kwakuwa nilikuwa nimechoka sana sikutaka hata kula kwani hamu ya kula sikuwa nayo kwa usiku ule, pia mchana nilikula msibani. Nilisali kabla ya kulala na kumuombea Sitti awe mzima huko aliko.
Nilipitiwa na usingizi nikiwa bado nimepiga magoti pale kitandani, nilishtuliwa na sauti ya mtu aliyekuwa akigonga mlango wangu, baadaye akahamia dirishani dirisha lilikuwa na wavu na pazia tu. "Soka Soka..!" sauti ya mtetemo ilisikika nilifungua pazia kutazama nje mbalamwezi ilikuwa ikiangaza kila upande sauti ilisikika tena, "Soka Soka, kwanini mliuzika mwili wangu mapema?" Nilifikicha macho kutazama mzimu wa Mzee Kingalu ulikuwa ukinitazama kutoka dirishani sura ni yakwake lakini macho yalikuwa yaking'aa sana kama yale ya paka.
"Kwani we' walikupeleka wapi?" nilimhoji. "Walinipeleka nyumbani kwa mzee Samasimba wanataka kunifanya msukule." ulijibu ule mzimu wa Mzee Kingalu. "Umewezaje kufika hapa?" "Nimetoroka." niliogopa nikawa nikitetemeka mwili mzima jasho likiwa linanitoka nikashtuka usingizini na kutazama pazia lilikuwa limefunguliwa na wala sikuona kitu chochote pale dirishani inamaana nilikuwa naota? Niliamka pale nilipokuwa nimepiga magoti nikalala vizuri na kujinyoosha kitandani.
ITAENDELEA...
Sitosahau yaliyonipata kijijini Kwamsisi-8
Sema hii n stori ya kutunga bhnMambo mazito
Hili jamaa kichwa ngumuHabari, wale walionifuata PM kwa ajili ya muendelezo wa story watambue, haitakuwa free kuna mchango kidogo wa vocha, pia kuna story mpya inakuja hapa very soon kuanzia kesho. jitahidi kutumia lugha ya staha unapo comment sio kwasababu unatumia fake ID ndio utiririke matusi heshima kitu cha bure.
Kuandika vitabu kusikuvimbishe kichwa sababu vitabu sio ishu tena kila popoma anajiandikia na kuchapa tu. So, unaweza kuwa na kitabu na ukawa popoma tuUsinifundishe uandishi, wewe kama unajua kukosoa si uandike story yako hata moja tuione, mimi ni mwandishi wa vitabu, sio hizi episode za JF. Kwa wanaojua umuhimu wa uandishi wamesha nifuata PM, watu kama wewe hawanisumbui, ushauri peleka angaza.
Unatapatapa sana dogo reputable writerSEHEMU YA 10
"Haiwezi kuwa kirahisi huyu kijana ametuingilia vya kutosha sasa haina budi tumfanyizie!" Mzee Samasimba na vijana wake Mbwana na Jumanne waliketi kwenye kikao kizito wakinijadili mimi. Hao vijana walikuwa wakiogopwa sana pale kijijini, mabingwa wa kuroga kuanzia zongo mpaka kutupiana mashakizi. Mashakizi ni majini yanayotumwa kukusababishia kifo kisichotarajiwa, mfano unaweza kupata ajali ya basi ukafa kumbe sababu ni za kichawi na hii inatokana na mashakizi utakayo tumiwa.
Taarifa za vikao vyao nilizipata kwakuwa nilikuwa nikioteshwa kila kitu walichokifanya niliona mchezo mzima na hapo nikapanga namna ya kujiokoa. Siku hii usiku niliota ndoto ya kutisha, nimesafiri kwenda mjini Tanga kikazi wakati wa chakula watu wengi tulikuwa tumekaa pembezoni ya maegesho ya magari ya mizigo, lilikuwepo lori la mizigo lililokuwa limepaki hapo kwahiyo sisi tulikuwa tumekaa kwa pembeni yake kufumba na kufumbua niliona lile kontena likichomoka na kutuangukia na kutufunika watu wote tuliokuwepo mahali pale, nilishtuka kutoka ndotoni.
Ni ndoto ambayo ilinisumbua sana ingawa sikumwambia mtu yeyote na baada ya wiki nilipokea barua ya mwaliko wa kuhudhuria semina ya walimu wa masomo ya sayansi katika jiji la Tanga na kweli nilipofika niliyaona mazingira kama yale niliona lori la mizigo likiwa limeegeshwa sehemu ambayo waalimu walikuwa wakigawiwa chakula, nilihisi kitu hakiko sawa nami sikusogelea kabisa eneo hilo mara baada ya kuchukua chakula nilikaa mbali ya eneo hilo huku nikishuhudia jambo litakaloweza kutokea.
Kufumba na kufumbua niliona lile kontena likianguka kwa haraka na kuwafunika walimu wote waliokuwapo pale kwa chini wengi walijeruhiwa na baadhi yao kupoteza maisha niliogopa sana nikamshukuru Mungu kwa kuniepusha na jambo hilo. Baada ya tukio hilo nilishangaa nilipopigiwa simu na watu ninaowafahamu kutoka kule kijijini wakiniambia kwamba taarifa zimesambaa kuwa mimi ni mmoja wa walimu waliofariki kwenye ajali hiyo, nilishangaa! Baada ya kufanya uchunguzi niliambiwa watu waliokuwa wakisambaza taarifa hiyo hawakuwa wengine bali ni wale vijana wa mzee Samasimba Jumanne na Mbwana.
Nilirudi nikafika kijijini usiku. Sitti alikuwa na kawaida ya kuja kunipokea pindi nitokapo nje ya mji na siku hii nilimletea zawadi aliyokuwa akiipenda, lotion ya Swetheart pamoja na perfume ya Kulthum. Nilitembea mpaka nyumbani kwangu na kuingia ndani, nilisikia miguno ya kimapenzi ikitokea ndani ya nyumba yangu."Kuna nini tena humu?!" Nilishtuka kwasababu funguo za nyumba yangu nilimkabidhi Sitti nilivyo ondoka kwenda mjini Tanga. Niliporudi sikuona umuhimu wa kumjulisha kwamba ninarudi nilitembea taratibu mpaka nyumbani kwangu na baada ya kusikia sauti hizo nilichungulia kupitia dirishani, kuna mambo ya kiutu uzima yalikuwa yakiendelea chumbani kwangu.
Sitaki kuamini kile nilicho kishuhudia usiku ule, ilikuwa ni kweli na wala haikuwa ndoto kama nilivyotaraji iwe. Sitti alikuwa akivunja amri ya sitta na Mbwana tena mbaya zaidi alikuwa akifanya kitendo hicho ndani ya nyumba yangu kwenye kitanda changu. Niligonga mlango kwa nguvu wala hawakufungua, nikaufungua kwa funguo za akiba nilizokuwa nazo. "Lahaula lakwata!" Niliwakuta wakiwa kama walivyo zaliwa wakivunja amri ya sita juu ya kitanda changu. "Sitti ni wewe ama ninaota!" Walishtuka, "Hee Soka, ni wewe ama ni mzimu wako?!" wote wakawa wakinitazama.
"Nilijua umesha fariki kwenye ajali kumbe bado u mzima!" Walikukuruka wakashindwa kuachiana nilichukua fimbo nikawatandika haswa nilimtandika zaidi Mbwana kwasababu nilikuwa na hasira naye lakini alijaribu kukukuruka hakuweza kutoka kwani nilikuwa nimezindika kichawi. Baada ya kuwapa kipigo hevi na kuridhika ndipo nilichomoa kisu kwenye ala niliyokuwa nimeificha kwenye kona ya chumba changu basi wakaachiana. Sikutaka kuwaona kabisa mbele ya macho yangu, niliwafukuza. Pamoja na uchawi wake wote, Mbwana alikuwa mdogo kama piritoni kwasababu ukifumaniwa huwezi kuwa na nguvu zozote, hata kama ukiwa na nguvu za kichawi unashindwa kuzitumia ili kujitetea.
Japo nilimpenda Sitti na kujitesa kwa ajili yake lakini nilikuja kuamini kwamba wanawake sio watu wa kuwawekea mdhamana. "Sitti nilimuamini mpaka kudiriki kumuachia funguo ya nyumba yangu lakini leo hii ameamua kunifanyia usaliti wa wazi kabisa," nilijisemea mwenyewe kwani niliumia sana moyoni. Sikutaka kumwambia mtu yeyote juu ya jambo hili nilijua itakuwa aibu kubwa ila akilini niliapa kulipa kisasi.
Siku hiyo sikulala kitandani nilikuwa nimekaa pale nje kwenye kizingiti nikiwaza sana mpaka usingizi uliponipitia na cha ajabu nilishtuka usingizini nikiwa nimelala kitandani kwangu milango yote ikiwa imefungwa. Nilishtuka kusikia harufu kali ya marashi ikiwa imesambaa kwenye kile chumba na hapo nikamuona mwanamke mrembo mweupe pe' na mwenye nywele ndefu zilizofika mpaka kwenye kiuno chake na alikuwa na macho maangavu yaliyoingia ndani.
Alikuwa amesimama mbele yangu akinitazama huku yupo uchi wa mnyama. "Ondoka kwangu kaa mbali na mimi, kwani wewe ni nani nilimhoji!" "Naitwa Maimuna nimetoka kwenye kina kirefu cha bahari nimekupenda sana jinsi ulivyo na pia nimependa ujasiri wako, nilimtazama mwanamke yule kuanzia juu mpaka chini nilistaajabu nilipoziona kwato zake mithili ya farasi zikiwa zimechomoka kwenye miguu yake nikapatwa na kigugumizi.
Yule kiumbe akaondoka, nilimtazama akitembea vishindo vya viatu virefu vilisikika vikipotelea mbali ya upeo wa akili yangu na sauti ya mlango ukafungwa kwa kishindo kikuu! Nilishtuka kwenye ndoto ile na jasho jingi lilikuwa limenitoka mpaka kulowesha mashuka, nikweli nilikuwa nimelala kitandani kwangu na milango yote ikiwa imefungwa sikuelewa kivipi yule kiumbe alipita mpaka kuweza kuingia na kutoka ndani ya nyumba yangu. Baadaye nilikuja kutambua kuwa majini ni viumbe wenye uwezo mkubwa wa kuweza kupenya ama kupita kwenye maeneo yenye vizuizi vya kila aina kwa sababu kikawaida viumbe hawa hawana mwili wa kibinadamu na huweza kuvaa umbo na mwili wa kiumbe chochote kile wakitakacho.
ITAENDELEA...