jaywacnza
JF-Expert Member
- Sep 15, 2012
- 997
- 1,151
Unatakiwa kujibu hoja ya msingi usikurupuke mbona maelezo yangu hapo yanajieleza. kama watumishi wa Mungu ni nini wajibu wako hasa unaowafanya waitwe viongozi wa dini? Je wamekuwa viongozi wa Siasa? Au ndo maana siku hizi wanasiasa wengi wametoka makanisani kuitwa wachungaji mpaka wabunge nk. Mkuu wanatakiwa kutimiza wajibu wao wa kuhubiri neno la Mungu (Ndo maana YESU alivyotaka kupaa kwenda mbinguni aliwaambia wafuasi wake (wanafunzi) kuwa enedeni duniani kote mkawahubiri watu na atakae amini mtambatiza kwa jina la Baba, Mwana na roho mtakatifu) na si vinginevyo. Hayo matatizo yaliyomo makanisani wewe huyaoni? kila siku wachungaji na Mapadri wanakamatwa ugoni, mbona sijasikia wakitoa waraka wa kupinga hayo? Au kwako wewe jambo baya ni KATIBA tu na hayo mengine (uashereati, uzinzi, uongo, wizi, kutopendana baina ya viongozi wa dini moja na nyingine) ni kawaida kwa watumishi wa Mungu?
Sasa suala la kutengeneza katiba si la kisiasa tu, linajumuhisha nyanja zote mpk din, wa wap ww?