Siungi mkono wanaomtukana Rais Samia!

Siungi mkono wanaomtukana Rais Samia!

Tabia ya binadamu huwa ni ya ajabu.
Ukimuokoa mtu toka mtoni, halafu kule mbele ya safari mtu huyo akipata shida basi bado anaweza kukutusi, akisahau kabisa kuwa nafasi hiyo ya kutusi anaitumia vibaya maana asingefanya hivyo, kama asngevuka mto.

Nabii Musa aliwatoa utumwani wana wa Israel na kuwavusha hadi bahari ya shamu.
Bado walipofika Jangwani, walipopata njaa kali, karibu wamsulubu Nabii Musa kuwa walikuwa wanakula na kushiba utumwani, na ni kwa nini Nabii amewaleta jangwani kufa na njaa.

Hiyo ndio tabia ya binadamu, hakumbuki fadhila zako ukiteleza.

Namwaomba Mama Samia aendelee kuwa mvumilivu, kuteleza si kuanguka.

Lakini wanaomtukana mama Samia wanakosea sana, na ni watu wa kuonywa na kuhurumiwa kwa kukosa maadili yapasayo mtu.
Nimepita kwa rafiki yangu mmoja nikakuta hiki kitabu, kimenifunua mengi!
View attachment 2705150

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Viongozi wanaoingia madarakani kwa kunajisi chaguzi za nchi ni zaidi ya matusi. Tunaposema chaguzi za nchi ziheshimiwe ni pamoja na kuwa na haki ya kuheshimiwa. Sio unaingia madarakani kwa njia zisizo za heshima, kisha utake heshima.
Kama waliona chaguzi hazikuwa na haki wangeenda mahakaman
 
Mahakama zipi, hizi hizi zenye kesi ya kina Mdee mwaka wa pili huu hakuna hukumu, wakati kesi ya urais hapo Kenya ambayo ni kubwa kuliko hii ya kina Mdee imeisha muda mrefu na hukumu tayari? Ama hujui unaongea nini dogo?
 
Tabia ya binadamu huwa ni ya ajabu.
Ukimuokoa mtu toka mtoni, halafu kule mbele ya safari mtu huyo akipata shida basi bado anaweza kukutusi, akisahau kabisa kuwa nafasi hiyo ya kutusi anaitumia vibaya maana asingefanya hivyo, kama asngevuka mto.

Nabii Musa aliwatoa utumwani wana wa Israel na kuwavusha hadi bahari ya shamu.
Bado walipofika Jangwani, walipopata njaa kali, karibu wamsulubu Nabii Musa kuwa walikuwa wanakula na kushiba utumwani, na ni kwa nini Nabii amewaleta jangwani kufa na njaa.

Hiyo ndio tabia ya binadamu, hakumbuki fadhila zako ukiteleza.

Namwaomba Mama Samia aendelee kuwa mvumilivu, kuteleza si kuanguka.

Lakini wanaomtukana mama Samia wanakosea sana, na ni watu wa kuonywa na kuhurumiwa kwa kukosa maadili yapasayo mtu.
Nimepita kwa rafiki yangu mmoja nikakuta hiki kitabu, kimenifunua mengi!
View attachment 2705150
Wanaomkosea heshima Mama Samia wanajificha kwa kigezo cha kutoa maoni yao kuhusu suala zima la bandari.

Hayati JPM wasingethubutu kumvunjia heshima kama wanavyomfanyia huyu SSH, na wanajua nini kingewakuta kwa kufungua midomo yao na kuropoka hovyo dhidi ya mamlaka halali ya rais wa nchi.
 
Wanaotukana si wastaarabu, watu wasio na dira!
 
Back
Top Bottom