Siwaelewi Jaji Mkuu, Mwanasheria Mkuu, TLS, Tume ya Haki za Binadamu

Siwaelewi Jaji Mkuu, Mwanasheria Mkuu, TLS, Tume ya Haki za Binadamu

Bashiru atasema huo ni utani tu Rais hakuwa serious, yeye kwake mavi ya.... Anaita keki
 
Umesema vema, ila hapo mwisho umechemka! Usituletee ukatoliki kwenye mambo ya kitaifa.
Mi nadhani hajaleta ukatoliki. Lakini inafahamika hii ni moja ya taasisi kubwa, na anayeongoza ni muumini wao.

Labda wakitoa tamko linaweza kumstua kidogo kuwa asijiamini sana.

Unadhani kanisa likisema huyu hatufai atatoboa?
 
Kinachowaweka kimya ni Ugali, pia hakuna wa kujitoa sadaka kwasasa zaidi ya wananchi wenyewe!
Shida pia Watanzania hatuji tambui. Maana hii ilitosha kumnyima kura zote ili tupate rais atakae apa kulinda katiba ya nchi bila ubaguzi kama huyu bwana wa Ccm
 
Kwa kweli hili ni tatizo, huu ni ubaguzi wa wazi kabisa cha kusikitisha hakuna mtu anayejali.
 
UHURU, HAKI, MAENDELEO YA WATU. Kwake yeye vyote hivyo vitatu vinakosekana kwani watanzania wasio na chama chao hawana UHURU wa kuchagua chama cha kuwaongoza, hawana HAKI ya kupata maendeleo kama watachagua chama kingine na hivyohawata kuwa na MAENDELEO yao (kama watu) kwa sababu tu watakuwa wamechagua chama cha upinzani.

Watanzania bila kujali vyama vyao wanatakiwa walete mabadiliko kwa kutumia sanduku la kula kwani kila mtu analipa kodi hivyo ni haki yake kupatiwa maendeleo na chama chochote kitakachoingia madarakani.
 
Huyo chalii sio mtanzania ndio maana kauli zake zimejaa chuki visasi roho mbaya ubaguzi uchawi
 
Yawezrkana katika historia yetu hatujawa kupata kiongozi wa ajabu kama awamu hii.

Ameapa kuwatendei haki wananchi wote halafu anatamka wazi kuwa hatafuata katiba bali atawabagua watu kwa misingi ya vyama!!

Ni ajabu sana. Nchi yetu sasa anatawaliwa na kiongozi mbaguzi ambaye anajivunia ubaguzi. Inatia hasira, inatia kinyaa na kukera kwelikweli.
 
huduma za jamii ni haki za walipa kodi sio hisani ya rais. tuchague chadema tupate serikali za majimbo.
 
Kwasababu akili zako haziko sawa
Sky kwa Mujibu wa katiba yupo sawa anaeamua maendeleo yaende wapi na yasiende wapi ni Rais, kila siku Lisu anatupa hili somo ndiyo maana anasema hataki kuwa Rais kama marais waliotangulia. Jamaa hajakosea hata kidogo na akili zake zipo timamu.

Kazi ni kwetu wananchi tuendelee na rais mbaguzi au tumpatie kura mgombea atakaetupa katiba bora inayompa mwananchi fursa ya kuhoji maendeleo ya eneo lake. Tusiwe "rais tunaomba fedha za barabara" wakati kodi tunalipa wote bila kubagua chama, kanda, dini wala kabila.
"Ni yeye" 2020.
 
Back
Top Bottom