Siwezi kuingia barabarani kwaajili ya kumpambania Lissu au Mbowe aingie Ikulu

Wee CCM kaa kimya!
 
Wewe Umefanya nini mpaka Sasa au ndio nyumbu muoga
Suala la msingi ni kwamba wewe pigania yule unayedhani anafaa kwenda ikulu na mwingine/wengine wapiganie yule wanayedhani anafaa kwenda ikulu. Zingine zote ni porojo za kutafuta "attention."
 
Ni kosa kubwa kuwasaidia wana siasa kazi yao ,kila mtu afanye kazi aliyoichagua ,mimi siwezi kwenda mkutano wa hadhara kumsikiliza mwanasiasa ,habari zake ntakutana nazo mtandaoni ,niko busy nafanya kazi niliyochagua.Kuhusu kuandamana ndio sitaki kusikia.NAUNGA MKONO HOJA, wanasiasa wakimaliza press wanaandikiana posho
 
Even wenyewe hawataki wapiganiwe. Wanataka mjipiganie, wkt vijana wa kemya na bangladesh wanahangaika hawakuwa na mwanasiasa akiwaongoza, mpaka leo hakuna mwanasiasa
Walipigana wenyewe,, sasa wewe endelea kuamini mwanasiasa atakueletea mabadiliko
Shida ipo pale siasa inapogeuka ajira ya kudumu.
Maokoto ndani ya siasa ndio kansa inayovitafuna vyama vya siasa.

Mfano mzuri ni Laila Odinga, kila uchaguzi anadai kaibiwa kura,anaitisha maadamano,wananchi kwa wingi wanaingia barabarani,polisi inapambana vikali na waandamanaji,mamia wanajeruhiwa na wengine wanapoteza maisha.

Baadae Laila huyo huyo anakuja na handshake wanamuingiza kwenye serikali kinyemela, anapewa mpunga mwingi wa kumfunga mdomo,lakini waliomuunga mkono wakapigwa wakaumizwa,wakafungwa na wengine kupoteza maisha wanaambulia patupu.

Mwanasiasa mtaji wake mkuu ni watu yaani wafuasi.Hasa pale anapotaka kushindikiza mamlaka.
Akishapata hayo mamlaka sio mwenzenu tena.Na akiona mnamzonga anatengeza machawa,mchezo umekwisha.
 
Sawa unachoweza ni kuingia barabarani ili kuuza Bandari zetu na maliasili zingine.
 
Halafu Lissu alisema watoto wake ni wamarekani na lema familia yake iko Canada. Wakawalete watoto wao waandamane kwa faida ya baba zao.
 
Watanzania Wengi hamjui lolote kuhusu nchi yenu na viongozi wanajua hilo hivyo nyie tulieni muendelee kugumia kitakuja kizazi kingine sio hiki chenu hicho kizazi kikija miaka 300 ijayo kitajenga nchi hii viongozi watajua hawa wanatuona na wanaeleewa hawatakubali ujinga ujinga.

Nyie wa sasa hamjui kitu na hata hao wapinzani hivi mtu mwenye akili ataandamana kisa Mbowe??? Mbowe sio mpinzani hivi nyie hamuelewi nn??? Mbowe hajawahi kuwa mpinzani anaitumia chadema kama duka lake binafsi. MTU mwingine akiinuka kidogo humfanyie Fitna na kumuondoa kwa kutumia machawa wake.
Hata sasa Wakina Lissu awataondoa .
 
Hata hao wapinzani hawakuhitaji wala hawana muda na wewe.
 
Wewe ni MAITI hata kabla hujapigwa risasi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…