Siwezi kumpa rafiki yangu connection ya kazi mahali ninapofanya kazi

Siwezi kumpa rafiki yangu connection ya kazi mahali ninapofanya kazi

NetMaster

JF-Expert Member
Joined
Sep 12, 2022
Posts
1,454
Reaction score
4,925
Sitaki unafiki, ntampa rafiki konekshen ya kazi kwa masharti mawil tu:

1. Nikisikia kuna nafasi ndani ya sehemu nayofanya kazi ila haiingiliani na ofisi ama kitengo changu ninatoa koneksheni, mfano mimi nipo ofisi ya ufundi kuna nafasi ya ufagiaji ama udaktari nitasaidia, nafasi hizi muingiliano haupo ama ni mdogo sana, siwezi kutoa koneksheni uje tuwe ofisi moja ama uwe na kazi tunayoingiliana mfano mimi kupokea maelekezo yako au kinyume, NEVER!

2. Nikisikia kuna nafasi sehemu nyingine nitatoa msaidia hata kama kazi zetu zitafanana. Tofauti na hivyo, Bora nimpe mtu ninaemfahamu tu Ila sio rafiki yangu.

SABABU:

- Ni hatari kuwa sehemu moja na rafiki anaejua siri zako na madhaifu mengi, ukiunganisha jinsi nae anavyoitamani nafasi yako ili apokee mshahara kama wako, anaweza kutumia hivi vitu kuchukua nafasi yako,

- Mmoja wenu anapandishwa cheo mara kwa mara ila mwengine kabaki pale pale inaweza kuzaa chuki moyoni japo kuchekeana kinafki usoni.
 
Sitaki unafiki, nikisikia kuna nafasi ndani ya sehemu nayofanyia kazi lakini ni ofisi tofauti na yangu ama nikisikia kuna nafasi sehemu nyingine nitatoa msaidia kadri ya uwezo wangu.

ilà tukae ofisi moja hapana kwakweli, sitaweza kufanya hivyo , Bora nimpe mtu ninaemfahamu tu Ila sio rafiki yangu
Hujasema sbb mkuu
 
mimi niliwahi kufanya kazi kituo kimoja na bw mkubwa!(alikuwa na cheo kikubwa pale)
Aisee! Nilikosa marafiki wakifkiri labda nitakuwa chawa.. Mazngra niliyaona magumu sana
Wanakuona snichi 😂 😂
 
Kama mna vyeo tofauti chokochoko hazikosi! Ila atwambie kilichomkuta tu
Utakula nae na kunywa nae na bili utalipa lakini yeye anaweza kutafsiri unapokea mshahara mkubwa na posho kbao zaidi yake.

Hapo anaanza kuitamani nafasi yako na anaweza kukufanyia figisu akupore hio nafasi.
 
utakula nae na kunywa nae na bili utalipa lakini yeye anaweza kutafsiri unapokea mshahara mkubwa na posho kbao zaidi yake.

hapo anaanza kuitamani nafasi yako na anaweza kukufanyia figisu akupore hio nafasi.
Nilikuwa nikijiulza kwanini watu wana miradi mikubwa lakini ameajiri watu wa nje huku ndg zake hawana ajira?! aah jibu lilikuja automaticaly.
 
Urafiki wa wanawake ni urafiki wa mashaka sana. Ila kiumeni hizi changamoto ni nadra sana.

Kiukweli mimi rafiki yangu kukiwa na mchongo nilipo na najua kabisa hapa ana fit chapu namuunganisha maana zamani tulikua tuna share hadi mademu na life linaenda iwe hizi dili za kupwa na kujaa.

Agiza kabisa togwa nakulipia [emoji28]
 
Urafiki wa wanawake ni urafiki wa mashaka sana. Ila kiumeni hizi changamoto ni nadra sana.

Kiukweli mimi rafiki yangu kukiwa na mchongo nilipo na najua kabisa hapa ana fit chapu namuunganisha maana zamani tulikua tuna share hadi mademu na life linaenda iwe hizi dili za kupwa na kujaa.
Umeongea kiume sana, mi dili likiwepo na nina mwamba ana-fit tena hata awe konki zaidi yangu lazima nimshitue.

Uanaume ni kuinuana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Imenitokea aysee....rafiki yangu kabxaa kanifanyia connection...nmepata mchongo tuko sehem moja....cha ajabu hizi wk mbili tatu kaamua kunichunia tu bila sababu...hata salam.ndo ya kulazimisha sanaa...nmejarbu kuchunguza nmebaini kuwa anadhan mi ndo napeleka siri zake kwa bosi cz wameleta boss mpya na hawaelewani kabxaa...sas nlikuwa najaribu tu ku please kuwa ajifanye kuwa chini tu cz hizi taasis binafsi mtu akiamua kukupiga chini wala haulizi mara mbili due ugomv wao ulifika hatua mbya zaid hadi kutokusalimiana.....sasa jamaa kaamua kuninunia na cwez hata kumuuliza kulikon due anachofikiria siwez kufanya huo ujinga kwan tumetoka mbali sanaa....imenibid tu na mimi nipige kimya hadi nione hatma yake ni nin
 
Kwa kuongezea tu ni kwamba, siku zote rafiki wa kweli anapatikana kazini. Ukifanya kazi na mtu na hajawahi hata kuwaza kukufanyia figisu ili ufukuzwe kazi kisha uje kufa kwa njaa, hakika huyo ni rafiki wa maana sana. Keep him close.
 
Uchawi sio lazima upae na ungo usiku, hata hayo mawazo yako ni uchawi tosha.

Hii yote inadhihirisha jinsi usivyojiamini, yule rafiki unayemsaidia wewe ndie atakaye wasaidia wengine hata kama sio wewe direct.

Hivo watu wema ndo wanashea "blessings"

Unapom-lift mtu in another way na wewe unakuwa lifted.

Kumbuka: kipimo unachompimia mwenzio nawe ndo utapimiwa hichohicho au kitasukwasukwa(kitajazwa) iwe ni mema au mabaya.
 
Nadhani ni aina ya marafiki waliokuzunguka.
Hata mimi kuna marafiki siwezi wapa mchongo hata kama wanafit kulingana na hulka zao, hawachelewi kukudhuru ama lah kuanza kukupeleleza ili ayajue madhaifu yako na ayafurahie.

Ndo ivo tunaishi nao tu ivo ivo kibingwa na ndo wana sometimes mnainuana kibishi.
 
Marafiki ni ma snitch mi kuna mmoja alikuwa ananichora kaja kufanya mishe kama yangu tunagombea wateja
 
Back
Top Bottom